Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 3/8 kur. 19-21
  • Popocatepetl—Volkeno ya Mexico ya Kifahari, Itishayo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Popocatepetl—Volkeno ya Mexico ya Kifahari, Itishayo
  • Amkeni!—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Historia ya Hiyo Volkeno
  • Volkeno Yaanza Kutenda
  • Kutembelea “Mlima wa Moto”
    Amkeni!—2005
  • Volkeno—Je, Umo Hatarini?
    Amkeni!—1996
  • Jinsi Tulivyoponyoka Mlipuko wa Volkano Wenye Kuogofya!
    Amkeni!—2002
  • Visiwa Vinavyojengwa
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 3/8 kur. 19-21

Popocatepetl—Volkeno ya Mexico ya Kifahari, Itishayo

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA MEXICO

JE, UNGEPENDA kuishi kandokando ya volkeno yenye kuvutia hata hivyo yenye kutisha? Labda ungefikiria hilo kwa uangalifu sana. Hata hivyo, hii ni hali halisi kwa maelfu ya watu ambao huishi katika miji iliyo kandokando ya volkeno ya kifahari ya Popocatepetl, katika Mexico.

Historia ya Hiyo Volkeno

Jina layo katika Kinahuatl humaanisha “Mlima” au “Kilima Kitoacho Moshi.” Volkeno hiyo ina kimo cha meta 5,452 na iko katika milima ya Sierra Nevada, katika jimbo la Puebla, karibu na mipaka ya majimbo ya Mexico na Morelos. Ina umbo la pia zuri na la kifahari na huwa na theluji juu yayo wakati wote mwakani. Kwa kipindi cha miaka mingi, volkeno hii yenye kuvutia imetatiza maisha za wakazi wa mashambani wa eneo hilo kwa kulipuka mara zipatazo 16 kati ya 1347 na 1927. Hata hivyo, hakuna mmoja wa milipuko hii uliokuwa mkubwa.

Volkeno hiyo iko kati ya maeneo mawili makubwa ya majiji: jiji la Puebla, lililo kilometa 44 upande wa mashariki na jiji la Mexico, lililo kilometa 70 upande wa kaskazini-magharibi. Kwa kuongezea, katika jimbo la Puebla, kuna miji 307, kukiwa na jumla ya idadi ya watu 400,000, walio karibu na volkeno hiyo. Ingawa ni kweli kwamba si wote wa watu hawa walio katika maeneo yenye hatari kubwa, pigo la kiuchumi na kijamii liwezalo kuletwa na mlipuko mkubwa wa Popocatepetl laweza kuwa baya sana kwa eneo hilo.

Mwishoni mwa mwaka wa 1994, kulikuwa na ongezeko kubwa katika utendaji wa volkeno hiyo—kufikia kiwango cha kwamba onyo lilitolewa na watu wakaanza kuhamishwa mara moja. Kufikia Desemba 21, 1994, angalau matundu matatu yalionekana kwenye sehemu ya chini ya kreta, ambayo yalikuwa yakitoa gesi na mvuke. Mmwagiko wa majivu, ambao ulienea kote kufikia jiji la Puebla, ulifikia tani 5,000. Kisha serikali ikaanzisha programu ya kuhamisha watu wapatao 50,000, ambao kati yao 30,000 walipata malazi katika makao salama.

Mashahidi wa Yehova pia waliitikia kwa kuandaa makao kwa wale wenye uhitaji. (Linganisha Matendo 4:32-35.) Ripoti kutoka halmashauri ya kutoa msaada ya Mashahidi yasema: “Japo wakati wenyewe na uharaka wa hali hiyo, itikio la akina ndugu wa jiji la Puebla na viunga vyalo lilikuwa lenye kutokeza. Mipango ilifanywa ili kupatia watu zaidi ya 600 malazi. Kituo kimoja cha televisheni kilisema: ‘Mashahidi wa Yehova walitenda kwa uharaka sana. Walihamisha ndugu zao kutoka eneo la hatari mara moja.’”

Volkeno Yaanza Kutenda

Kulingana na habari rasmi, Jumanne, Machi 5, 1996, saa 9:50 usiku, ongezeko la ghafula lilionekana katika utendaji wa mitetemeko ya volkeno, labda iliyohusiana na kufunguliwa kwa vijia vikubwa vilivyofunguliwa na gesi na mvuke kutokana na utendaji wa Desemba 21, 1994. Picha na habari zilizopatikana zilithibitisha kwamba vijia hivi vilikuwa vimezibwa na jivu, ambalo lilisababisha msongo wa ndani wa volkeno hiyo. Msongo huu nao hatimaye ukafungua tena vijia hivyo.

Gazeti la habari El Universal, la Jumanne, Aprili 9, 1996, lilisema: “Popocatepetl ilikuwa na mmwagiko wa lava katika kreta, kwa hiyo wanasayansi na wenye mamlaka kutoka Shirika la Kulinda Raia wako macho, kwa sababu ya ongezeko la utendaji wa volkeno hiyo.” Ripoti hiyo ilitaja kwamba mabadiliko hayo “hufanyiza umbo la ‘kuba’ ambalo litasababisha ‘vijia’ vya Popocatepetl kujaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, jambo ambalo laweza kusababisha mmwagiko wa nje.”

Alhamisi, Mei 2, 1996, kwenye mkutano katika jiji la Puebla, hali ya volkeno ya Popocatepetl katika hatua yayo mpya ilizungumziwa. Dakt. Servando de la Cruz Reyna, mshiriki wa Institute of Geophysics of the National Autonomous University of Mexico, alisema: “Kiasili, hali hii mpya yasababisha hangaiko kubwa . . . Sikuzote kuna uwezekano kwamba volkeno hii itageuka kufikia hatua hatari zaidi. Hilo laweza kutokea, na hatulipingi hata kidogo.”

Watu wamelalamika kwamba hata ingawa serikali yaongea kuhusu programu za kuandaa makao na kuhamisha na kufanya mikutano ya kuandaa mwongozo kwa watu, uhalisi ni kwamba watu wanaoishi katika eneo hilo wanahisi kwamba hawajapata mwongozo wa wazi juu ya mambo ya kufanya volkeno hiyo ikilipuka. Kwa kielelezo, kwenye mkutano ambao umetajwa hapo juu, wawakilishi kadhaa kutoka miji ambayo iko karibu na volkeno hiyo walipinga kwamba hawakujua ni makao gani wapaswayo kuyaendea kukitukia msiba.

Maonyo kwamba volkeno hiyo imekuwa ikitoa yapasa kuchukuliwa kwa uzito. Watu wenye busara bila shaka watafanya kila kitu wawezacho ili kulinda maisha zao, hata kudhabihu vitu vya kimwili. Mashahidi wa Yehova wanaoishi katika eneo hilo wamekuwa wakijitayarisha kuhama eneo hilo uhitaji ukizuka. Halmashauri ya kutoa msaada imepewa mgawo kuzuru Mashahidi katika eneo hilo kwa ukawaida, kuwaongoza juu ya wapaswacho kufanya msiba ukitukia. Wengine ambao huishi karibu zaidi na eneo la hatari wametiwa moyo kuondoka eneo hilo wakati ungalipo, kwa kuwa wataalamu wa volkeno wameonya waziwazi kwamba volkeno hiyo ni hatari itishayo kutokea. Bila shaka, uamuzi huo waachiwa kila familia.

Kwa sasa, watu wanaoishi katika ujirani huo wa volkeno wanaishi maisha ya kawaida. Hata hivyo, akili ya kawaida inaelekeza kwamba watu hao wakae chonjo kwa onyo lolote kutoka kwa volkeno hiyo au kutoka kwa wenye mamlaka ambalo laweza kuashiria hali ya hatari. Si jambo la hekima kutojali maonyo ya volkeno Popocatepetl ya kifahari lakini itishayo.

[Sanduku katika ukurasa wa 20]

Mapendekezo Msiba Ukitukia

Kitovu cha Kitaifa cha Kinga ya Misiba kimeandaa orodha ya hatua zipaswazo kuchukuliwa kabla ya msiba kuzuka:

• Jua njia yako ya kutorokea. (Tafuta mahali palipo juu, si mabonde ambamo lava, maji, au udongo waweza kupitia)

• Uwe na sanduku tayari lililo na hati za kibinafsi, dawa, maji, mavazi ya kubadili (hasa mazito yawezayo kufunika mwili mzima), kofia, kitambaa cha mkononi cha kufunika pua na kinywa, tochi, redio, betri, na blanketi

• Fanya matayarisho na watu wa ukoo wawezao kuandaa malazi na hivyo kuepuka kutumia makao ya umma

• Chukua vitu vya lazima pekee. Usichukue wanyama-rafiki au wanyama

• Jua jinsi ya kupata makao ya umma

• Zima stima, gesi, na maji

• Uwe mtulivu

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki