Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 4/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wayunitaria Wakubali Ndoa ya Wagoni-Jinsia-Moja
  • Kuamua Kimbele Jinsia ya Mtoto
  • Mazungumzo ya Kitoto Yenye Kudhuru
  • China Kupunguza Uchafuzi wa Maji
  • Maharamia “Watakatifu”
  • Mamalia Wako Hatarini Zaidi Kuliko Ndege
  • Programu ya Kusoma Yasaidia Kupunguza Uhalifu
  • Olimpiki na Umaskini
  • Mapumziko Marefu ya Kwenda Kunywa Kahawa
  • Mimea Itokezayo Joto
  • Waeneza Evanjeli Wakiri Kasoro
  • Spishi Zilizo Hatarini mwa Kutoweka—Mweneo wa Hilo Tatizo
    Amkeni!—1996
  • Kahawa Bora—Kutoka Kwenye Mbuni Hadi Kwenye Kikombe Chako
    Amkeni!—1999
  • Kahawa ya Kona Yenye Ladha Nzuri
    Amkeni!—2005
  • Ongezeko la Watoto Wanaozaliwa kwa Njia Zisizo za Asili
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 4/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Wayunitaria Wakubali Ndoa ya Wagoni-Jinsia-Moja

Kanisa la Wayunitaria limekuwa dini ya kwanza ya Marekani kukubali kirasmi ndoa za jinsia-moja, laripoti Christian Century. Wajumbe waliokuwa wakihudhuria mkusanyiko wa kila mwaka walipiga kura kwa kukubali kwa dhati “kutangaza ustahili wa ndoa kati ya watu wawili waliopatana.” Gazeti hilo la kidini lasema kwamba “chini ya sheria za kanisa, kila moja la makutaniko 1,040 ya kanisa hilo laweza kujiamulia kama litakubali ndoa ya wagoni-jinsia-moja na misago na kama litaandaa arusi hizo.”

Kuamua Kimbele Jinsia ya Mtoto

Kulingana na gazeti Popular Science, “yawezekana sasa kuamua kimbele jinsia ya mtoto kwa kuainisha shahawa ya baba, kwa kuwa ni aina ya shahawa iamuayo jinsia.” Kwanza, shahawa yatiwa rangi kwa rangi memetevu. Kisha, mwali wa leza watumiwa kutambulisha shahawa X (ya kike) kutokana na Y (ya kiume). Kompyuta husoma tofauti ya wangavu, na kifaa cha maabara ambacho kwa kawaida ‘hutumiwa kwa upimaji wa damu hutoa chaji chanya ya kiumeme kwa shahawa X na chaji hasi kwa shahawa Y. Kisha shahawa zaainishwa kutumia ncha ya chaji ya umeme iliyo kinyume ili kuzivutia.’ Kulingana na mwanasayansi aliyevumbua ufundi huo kwa ajili ya biashara ya ufugaji, uainishaji huo ni sahihi kwa asilimia 90 hivi. Kisha baadaye, shahawa zilizoteuliwa hutumiwa kutungisha chembe yai, na “viinitete vya jinsia zinazotakikana na kisha zinapandwa kwenye mji wa mimba.” Hata hivyo, hadi kufikia wakati huu ni uzawa mmoja tu wa kibinadamu umetokezwa kwa utaratibu huu.

Mazungumzo ya Kitoto Yenye Kudhuru

Jitihada za mapema za watoto za kuzungumza mara nyingi huonwa kuwa zenye kuvutia sana, na wazazi wengi huitikia kwa shauku kwa mazungumzo yao wenyewe ya kitoto. Hata hivyo, hilo laweza kufanya maendeleo ya usemi wa mtoto yawe hatarini, aandika mtaalamu wa usemi wa Brazili Eliane Regina Carrasco katika gazeti Veja. Wazazi warudiapo matamshi yaliyokosewa ya mtoto, kufanya hivyo “hukazia namna ya usemi ambao si sahihi,” asema Carrasco. Yeye asema kwamba hilo laweza kusababisha matatizo ya usemi. Laweza pia kuathiri mahusiano ya kijamii ya mtoto, yeye aongeza. “Mara nyingi, watoto hao hujitenga, huwa waoga, na wasiohisi usalama, wakiepuka hali ambazo kwazo wao hulazimika kujiacha wapatwe na [kejeli].” Ni jambo la kawaida kwa watoto wadogo kutamka maneno isivyofaa, na si jambo la lazima kuwasahihisha daima, asema Carrasco. Lakini ni jambo la muhimu kuwazungumzia kwa njia sahihi na kujaribu kukumbuka kwamba “wao wana akili na wana uwezo wa kujifunza.”

China Kupunguza Uchafuzi wa Maji

“Uchafuzi wa maji ni tatizo kubwa sana katika China, na kupunguza uchafuzi wa maji ni kazi ya uharaka sana,” asema msemaji wa Shirika la Kitaifa la China la Ulinzi wa Kimazingira. Kwa hivyo serikali ya China inachukua hatua za kupunguza uchafuzi wa maji katika mito na maziwa ya China yaliyochafuliwa sana, laripoti gazeti China Today. Kwa kielelezo, ili kudhibiti uchafu unaoingia mojawapo mito ya nchi hiyo uliochafuliwa sana, Mto Huaihe, serikali “imefunga viwanda vidogo 999 vya kutengeneza karatasi katika bonde la Huaihe.” Watu wapatao milioni 154 huishi katika Bonde la Huaihe, ambalo ni mojawapo maeneo makubwa ya China ya kutokeza nafaka na nishati.

Maharamia “Watakatifu”

Katika jitihada za “kujisitawisha upya likiwa kanisa la kitaifa,” Kanisa Othodoksi ya Rumania “limeanzisha kampeni ya kihila ya kuharibia sifa dini nyinginezo,” laripoti jarida Compass Direct katika makala iliyoandikwa na Willy Fautré. Fautré aongeza: “Viongozi wakuu na makasisi wenyeji wa kanisa Othodoksi katika Rumania” wamepanga vikundi kadhaa “vihangaishe vikundi vichache vya kidini na kuvinyima haki za msingi za kidini.” Akiwaita watangazaji wa kievanjeli wa redio kuwa “wachafuaji wa imani ya wazazi wetu wa kale,” askofu mkuu wa Suceava na Rădăuţi walimwandikia msimamizi wa baraza linalosimamia matangazo ya redio na televisheni katika Rumania, wakisema: “Twakuomba uwakomeshe au uweke mipaka, kwa sababu hawana aibu kabisa na wameazimia kugeuza watu imani katika bara letu wenyewe.”

Mamalia Wako Hatarini Zaidi Kuliko Ndege

“Mamalia wako katika hatari kubwa zaidi ya kutoweka hata kuliko ndege,” laripoti gazeti New Scientist. Habari hizi, zinazotegemea tarakimu zilizotolewa na Orodha Nyekundu ya Muungano wa Ulimwenguni wa Uhifadhi, hufunua kwamba ingawa asilimia 11 za spishi za ndege yakabiliwa na kutoweka tufeni pote, asimilia 25 ya spishi za mamalia sasa zimo hatarini. Primata ndicho kikundi kilicho hatarini kuliko vyote, kikiwa na asilimia 46 ya spishi zilizo hatarini mwa kutoweka. Kisha kuna walawadudu ambao ni asilimia 36, wakifuatwa na nguruwe-mwitu na kulungu wakiwa asilimia 33. Kikundi cha ndege kilicho hatarini zaidi ni korongo, asilimia 26 ikiwa hatarini mwa kutoweka. Sababu moja ya kiwango cha juu ya mamalia kutoweka ni kwamba, tofauti na ndege, wao hawawezi kuhama kwa urahisi kwenda kwenye eneo tofauti makao yao yaharibikapo.

Programu ya Kusoma Yasaidia Kupunguza Uhalifu

Katika Bradford, Uingereza, programu inayodhaminiwa na serikali inayonuiwa kuboresha uwezo wa usomaji wa watoto wa shule ina matokeo yenye kutazamisha, laripoti gazeti la habari la Uingereza The Independent. Programu hiyo ya kusoma haijasaidia tu kuboresha stadi za kusoma pia imepata sifa kwa kusaidia kupunguza uhalifu! “Tumehusianisha idadi ya vijana wanaovunja nyumba moja kwa moja na idadi ya wanafunzi wanaohepa shule,” asema John Watson, mkuu wa Ushirika wa Usomaji Bora. “Watoto wakiweza kusoma yaelekea watapendezwa zaidi na kinachotendeka shuleni na kutohepa sana shule. Kwa sababu hawako barabarani basi haielekei sana kwamba watakuwa wakivunja nyumba.”

Olimpiki na Umaskini

“Idadi ya medali zipatwazo na nchi fulani kwenye Olimpiki na kiwango cha fedha kilichowekewa majengo hayo na udhamini wa michezo ya Olimpiki huzusha maswali kuhusu ujitoaji wa ulimwengu kumaliza umaskini,” laripoti ENI Bulletin, la Uswisi. “Hii si kusema kwamba tusisherehekee ubora na kushangilia matendo yasiyo ya kawaida ya ustadi na uvumilivu wa kibinadamu,” asema Greg Foot, kutoka shirika la World Vision la Australia. “Lakini,” yeye aongeza, “ni lazima tuulize ikiwa tunasawazisha mambo kweli wakati tutumiapo kiasi kingi sana cha fedha katika kukamilisha ulaji wa wanariadha wetu bora huku mamilioni ya majirani wetu hawana chakula cha kutosha hata kupata nguvu za kuweza kutembea.” Inakadiriwa kwamba katika kipindi cha majuma mawili ya mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Atlanta, watoto 490,000 walikufa kwa njaa na maradhi yawezayo kuzuiwa ulimwenguni pote.

Mapumziko Marefu ya Kwenda Kunywa Kahawa

Waajiriwa fulani kwa kweli hufanya kisafari cha kipekee kwenda kupata kikombe cha kahawa cha saa nne. Kwa hakika, wengi hutoka kabisa mahali pao pa kazi. Kukiwa na baa za kahawa zenye kuandaa kahawa iliyoundwa na wataalamu wa kahawa, wafanyakazi wanakimbia kutoka ofisini ili kwenda kupata aina yao waipendayo ya kahawa. Likiwa tokeo, “badala ya kuwa na mapumziko ya kunywa kahawa kazini, watu wanatoroka kwenda kunywa kahawa kwenye baa za kahawa,” lasema The Wall Street Journal. Lakini waajiri wanahangaikia urefu wa visafari vya kwenda kwenye majumba ya kahawa. Katika jitihada za kukomesha wimbi hilo la mashabiki wa kahawa wenye kutoweka, hilo Journal lasema, mashirika fulani ya kibiashara yanashinda hali hiyo kwa kuweka mashine zazo zenyewe za kutengenezea kahawa aina ya cappuccino.

Mimea Itokezayo Joto

Watafiti wawili wa Australia wamepata kwamba maua aina ya lotus yana uwezo wenye kustaajabisha wa kusawazisha halijoto yayo yenyewe. Hapo mbeleni, ni wanyama wenye damu moto pekee waliofikiriwa kuwa na uwezo huu. Wakifanya kazi katika Bustani za Kibotania za Adelaide, Dakt. Roger Seymour na Dakt. Paul Schultze-Motel walishikanisha kifaa chenye kuitikia uamshi kwa maua yenye kuchanuka ya lotus ili kurekodi halijoto yayo na vitabia vinginevyo. Walipata nini? Hata wakati ambapo halijoto ilishuka kufikia digrii 10, halijoto ya machanuo ya lotus ilibaki kati ya digrii 30 na 35 Selsiasi. Watafiti bado hawajapata elezo la hali hii. Hata hivyo, kulingana na The New York Times, Dakt. Hanna Skubatz, mwanabiokemia wa mimea kwenye Chuo Kikuu cha Washington, Marekani, alisema kwamba “utokezaji wa joto [miongoni mwa mimea] kwa hakika huenda umeenea sana, isipokuwa ni vigumu tu kuutambua.”

Waeneza Evanjeli Wakiri Kasoro

“Waeneza evanjeli wa ulimwengu wa leo wanapoteza uaminifu wao kwa Biblia, mwelekeo wa kiadili, na bidii ya kimishonari,” lataarifu “Julisho Rasmi la Cambridge la Muungano wa Waeneza Evanjeli Wenye Kuungama.” Uchambuzi huu mkali ulitoka wapi? Labda kutoka kwa kikundi cha kanisa adui? La, ulitoka kwa waeneza evanjeli wenyewe. Hati hiyo ilitolewa na zaidi ya viongozi 100 wa waeneza evanjeli ambao walikutana hivi majuzi katika Cambridge, Massachusetts. Waandishi wa hati hiyo walikubali kwamba wao na viongozi wa kidini walihitaji “kutubu kwa sababu ya utayari wao wa kutawalwa na vitabia vya utamaduni upendwao na wengi.” Hati hiyo pia ilikiri kwamba “njia za kuandaa tiba, mbinu za mauzo, na msukumo wa ulimwengu wa vitumbuizo mara nyingi huwa na uvutano mwingi juu ya kile kanisa hutaka, jinsi ambavyo linafanya kazi na kile kanisa huandaa, kuliko jinsi ambavyo Neno la Mungu huwa na uvutano.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki