Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 5/8 uku. 31
  • Hesabu Gharama za Kuhama!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hesabu Gharama za Kuhama!
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Ni Lazima Tuhame?
    Amkeni!—1994
  • Je, Unaweza ‘Kuvuka Uingie Makedonia’?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2011
  • Je, Nikaishi Ng’ambo?
    Amkeni!—2000
  • “Toka Katika Bara Lako na Kutoka kwa Watu wa Ukoo Wako”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 5/8 uku. 31

Hesabu Gharama za Kuhama!

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA AFRIKA KUSINI

JE, UNAFIKIRIA kuhamia nchi nyingine? Je, umehesabu gharama? Hatumaanishi gharama za kifedha tu. Kwani, watu wengi hufikiria kuhama kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi tu. Twamaanisha gharama zisizojulikana ambazo hudhihirika tu baada ya kuhama kihalisi. Wakati huo kwa kawaida huwa ni kuchelewa mno kurudi nyumbani. Mambo yafuatayo hayakukusudiwa kukutisha, bali yanafaa kuchunguzwa:

“Kujifunza lugha mpya hutaka unyenyekevu na jitihada. Ni jambo linalovunja moyo kwa mtu mzima kupata kwamba hata watoto wadogo wafikiri yeye ni wa ajabu kwa sababu hawawezi kumwelewa. Kuendelea kukosea kipumbavu na ukichekwa wakati wote kwa sababu ya makosa yako ni jaribu kubwa sana kwa heshima ya wengi. Maisha ni ya upweke sana kwa wageni ambao hawawezi kuongea lugha ya wenyeji.”—Rosemary, mishonari katika Japani.

Labda wahisi kwamba wewe binafsi unajua lugha hiyo kiasi cha kutosha. Lakini, je, una hakika kwamba familia yako yote yajua lugha hiyo kiasi cha kwamba itafurahi kuhama?

Kutakuwa na matokeo gani kwa familia ikiwa baadhi ya washiriki walazimishwa kuhama dhidi ya mapenzi yao? “Baadhi ya wanawake [kutoka Mexico],” lasema gazeti Psychology of Women Quarterly, “hawakuombwa maoni katika kuhama na hawakutaka kuhama, wala hawakupenda kubaki Marekani baada ya kuhama.” Chini ya hali kama hizo, kuhama kwa lazima kwaweza kuharibu umoja wa familia. Lakini namna gani ikiwa mleta-riziki ahama peke yake?

Ilikadiriwa katika kitabu Population, Migration, and Urbanization in Africa kwamba katika sehemu moja ya mashambani ya kusini mwa Afrika, zaidi ya asilimia 50 ya “wanaume watu wazima hawaishi nyumbani wakati wowote ule.” Kutokuwapo huku kwaweza kuibia familia uradhi na uthabiti. Pia hutokeza uwezekano wa wenzi wa ndoa kuingia katika ukosefu wa adili. Ni bora kama nini iwapo familia, ikiwa yaamua kuhama au la, yadumu pamoja! Umoja wa familia ni kitu ambacho fedha haiwezi kununua.

Kisha, kuna mzigo wenye kulemea wa kukabiliana na ubaguzi. “Nilipohamia Uingereza ndipo nilipogundua tatizo la ‘ubaguzi wa rangi,’” akumbuka mhamiaji mmoja kutoka India. “[Utambuzi] huo ulitisha. Mshtuko wenye kuumiza. Nilitaka kurudi nyumbani, kuachana kabisa na mambo hayo.”—The Un-melting Pot.

Hivyo kabla ya kuhama, jiulize: ‘Je, kuna njia nyingine? Hatuwezi kufanya mabadiliko nyumbani? Je, kuhamia nchi nyingine kutafaa?’ Kwaweza kufaa au la, lakini kabla hujaamua, fikiria shauri hili zuri kutoka kwa Yesu: “Ni nani kati yenu atakaye kujenga mnara asiyeketi kwanza na kupiga hesabu ya gharama, ili aone kama ana kiasi cha kutosha kuukamilisha?”—Luka 14:28.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki