Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 7/22 kur. 8-10
  • Je, kwa Kweli Wahitaji Internet?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, kwa Kweli Wahitaji Internet?
  • Amkeni!—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Uhitaji—Je, Umehesabu Gharama?
  • Usalama —Je, Faragha Yako Yahifadhiwa?
  • Je, Utaweza Kupata Wakati?
  • Je Unakosa Fursa?
  • Internet—Kwa Nini Utahadhari?
    Amkeni!—1997
  • Intaneti Kutumia kwa Hekima Kifaa cha Ulimwenguni Pote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Je, Kweli Ni Hatari Kuchumbiana Kwenye Intaneti?
    Amkeni!—2005
  • Internet—Ni Nini?
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 7/22 kur. 8-10

Je, kwa Kweli Wahitaji Internet?

JE, UTUMIE Internet? Bila shaka, hilo ni jambo la kibinafsi, ambalo wapaswa kulifikiria kwa uzito. Ni mambo gani yawezayo kuathiri uamuzi wako?

Uhitaji—Je, Umehesabu Gharama?

Sehemu kubwa ya mpanuko wa hivi majuzi wa Internet imetokezwa na jitihada kali za mauzo za ulimwengu wa biashara. Kwa wazi, nia yao ni kufanya watu waone kuwa wana uhitaji. Mara yasitawishapo huo uonwao kuwa uhitaji, mashirika fulani hutaka watu wawe washiriki au watoe ada ya kujiandikisha ya kila mwaka kwa habari au huduma ambazo mwanzoni ulizifikia bila gharama. Ada hii ni nyongeza kwa gharama zako za kila mwezi za Internet. Magazeti fulani ya habari yapatikanayo kupitia mfumo wa kompyuta ni kielelezo cha kawaida cha zoea hili.

Je, umekadiria gharama ya vifaa vya programu ya kompyuta ukilinganisha na uhitaji wako hususa? (Linganisha Luka 14:28.) Je, kuna maktaba au shule za umma ziwezazo kufikia Internet? Huenda kutumia vyanzo hivi vya habari mwanzoni kukakusaidia upime uhitaji wako bila kutumia fedha nyingi za mwanzoni kwa kompyuta ya kibinafsi na vifaa vinavyohusiana nayo. Huenda ikawa kwamba kuna mahali pafaapo pa umma ambapo Internet yaweza kutumiwa, kama ihitajiwavyo, hadi itakapokuwa wazi ni mara nyingi kadiri gani vyanzo hivyo vya habari vyahitajiwa hasa. Kumbuka kwamba Internet ilikuwapo kwa zaidi ya miongo miwili kabla ya umma kujua kwamba ipo, achilia mbali kuitumia!

Usalama —Je, Faragha Yako Yahifadhiwa?

Hangaiko jingine la msingi ni usiri. Kwa kielelezo, ujumbe wako wa E-mail wapasa kuonwa tu na wewe na yule unayempelekea. Hata hivyo, barua hiyo iwapo safarini, mtu au kikundi fulani chenye werevu na yawezekana kisicho na unyoofu chaweza kuzuia au kuchunguza barua yako. Ili kulinda ujumbe, watu fulani hutumia vifaa fulani vya programu za kompyuta vya E-mail ili kuvuruga sehemu za barua wanazotaka kuziweka kuwa siri kabla ya kupeleka barua. Kwenye mwisho ule mwingine, anayepokea barua hiyo ahitaji programu kama hiyo ya kompyuta ili kuondoa hali ya kuvurugwa ya ujumbe huo.

Hivi majuzi, mazungumzo mengi yamekazia mabadilishano ya kadi za mkopo na habari nyingine zipaswazo kuwekwa kuwa siri kwa utumizi wa kibiashara kwenye Internet. Ingawa uvumbuzi mkubwa watarajiwa kuimarisha usalama, mchanganuzi mashuhuri wa usalama wa kompyuta Dorothy Denning ataarifu hivi: “Haiwezekani kuwa na mifumo iliyo salama kabisa, lakini hatari yaweza kupunguzwa kwa kiwango kikubwa, labda kwa kiwango kinachotoshana na thamani ya habari iliyohifadhiwa kwenye mifumo hiyo na tisho kutoka kwa watalaamu wa programu za kompyuta na vilevile watu wenye uwezo wa kufikia habari zilizo siri.” Usalama kamili hauwezekani katika mfumo wowote wa kompyuta, iwe umeunganishwa kwenye Internet au haujaunganishwa.

Je, Utaweza Kupata Wakati?

Suala jingine la maana ni wakati wako. Itachukua muda gani kuweka na kujifunza vifaa vya kuvinjari Internet? Pia, mfunzi mmoja mwenye uzoefu wa Internet alitaja kwamba kupitia-pitia Internet “kwaweza kuwa mmojawapo utendaji wenye kuraibisha zaidi na wenye kutumia wakati mwingi sana kwa mtumizi mpya wa Internet.” Kwa nini iko hivyo?

Kuna habari nyingi sana zenye kupendeza na mambo mengi sana mapya ya kuvumbua. Kwa hakika, Internet ni mkusanyo mkubwa sana wa maktaba zilizo na hati zenye kuvutia macho. Kutazama na kusoma sehemu yake ndogo kwaweza kutumia saa nyingi za jioni hatua kwa hatua kabla hata ufikirie kwenda kulala. (Ona sanduku “Wakati Wako Una Thamani Kadiri Gani?” kwenye ukurasa wa 13.) Bila shaka, hilo halimaanishi kwamba watumizi wote wa Web hawajidhibiti. Hata hivyo, lingekuwa jambo la hekima kuweka vizuizi kwa wakati unaotumiwa na habari inayotafutwa katika kupitia-pitia Web—hasa kwa vijana. Familia nyingi hufanya vivyo hivyo na televisheni.a Kufanya hivyo kutahifadhi wakati uliowekwa kando wa utendaji wa familia na wa kiroho.—Kumbukumbu la Torati 6:6, 7; Mathayo 5:3.

Je Unakosa Fursa?

Baada ya muda fulani, tekinolojia ya Internet itaenea kabisa katika maeneo yanayoendelea ya ulimwengu. Hata hivyo, kumbuka watu waliotajwa mwanzoni mwa makala ya kwanza. Sehemu kubwa ya habari waliyopata ingeweza kupatikana kwa kutumia maktaba, simu, upelekaji wa barua wa kawaida, au magazeti ya habari. Bila shaka, baadhi ya njia hizo huenda zikahusisha wakati na gharama nyingi zaidi. Hata hivyo, kwa watu wengi duniani pote, njia hizi za kidesturi zaidi yamkini zitaendelea kwa muda fulani kuwa njia kuu ya uwasiliano.

[Maelezo ya Chini]

a Ona makala “Vijana Huuliza . . . Naweza Kuachaje Kutazama Sana Televisheni?” katika toleo la Amkeni! la Februari 22, 1985, (la Kiingereza).

[Picha katika ukurasa wa 9]

Kupitia-pitia “Internet” kwaweza kuwa mtego ikiwa kuna ukosefu wa kujidhibiti

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki