Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 8/8 uku. 31
  • Miayo ya Wanyama wa Pori

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Miayo ya Wanyama wa Pori
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2012
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2002
  • Mtazame Kiboko Mwenye Nguvu Ajabu!
    Amkeni!—2003
  • Ustahimilivu—Kutoka Mwisho Mmoja Hadi Ule Mwingine
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 8/8 uku. 31

Miayo ya Wanyama wa Pori

Mtu apigapo miayo hadharani, watu waweza kufikiri kuwa hana heshima — au angalau ni mchovu kupita kiasi. Japo kanuni za adabu, kwa kweli kupiga miayo kuna kusudi lenye manufaa. Kupiga miayo ni kuvuta hewa kusikokusudiwa. Kwa kawaida sisi hupiga miayo jioni wakati ambapo tumechoshwa na utendaji mbalimbali wa siku au asubuhi baada ya kuamka. Mwayo mkubwa hutuongezea oksijeni na waweza kutuburudisha kwa kipindi kifupi; mara nyingi huwa sehemu ya kuamka.

Lakini je, ulijua kwamba wanyama pia hupiga miayo, ijapokuwa si kwa ajili ya hewa safi sikuzote? Sababu inayowafanya wafanye hivyo ni yenye kuvutia sana. Kwa kielelezo, nyakati nyingine tumbili hupiga miayo ili kuwasilisha ujumbe. Mdomo uliofunguliwa wazi na wonyesho wenye kutisha wa meno ni njia ya kutoa onyo kwa tumbili dume aliye mpinzani au mnyama anayetaka kumshambulia. Ujumbe ni: ‘Ninaweza kuuma vibaya. Kaa mbali!’

Imeonekana pia kwamba paka wa kuwinda wa nyanda za Afrika hujinyoosha na kupiga miayo kabla ya kwenda kuwinda. Sawa na wanadamu, mwayo wa paka humsaidia kisaikolojia—kuingiza hewa ya ziada mapafuni. Huo huongeza oksijeni katika damu. Kisha moyo huisukuma haraka kwenye sehemu nyingine za mwili, ukitokeza nguvu ya papo hapo kwa ajili ya mbio fupifupi za kukimbiza wanyama.

Kwani, hata samaki wameonekana wakipiga miayo! Kitabu Inside the Animal World husema kuhusu samaki ambaye nyakati nyingine “hupiga miayo kama matayarisho ya kwenda haraka. . . . Samaki aweza pia kupiga miayo anaposisimuka au amwonapo adui au aonapo chakula, pindi zote mwendo wa haraka uhitajiwapo.”

Huenda mwayo wenye kuvutia zaidi ya yote ni ule wa kiboko, au Behemothi. Kiumbe huyu mkubwa aweza kufungua mdomo wake mkubwa mno kufikia kiwango cha kushtua cha digrii 150! Mwayo humwezesha kiboko dume aliye mzee kuonyesha kila mmoja katika kidimbwi cha viboko ni nani aliye bwana-mkubwa. Pia hutumika kama onyo kali kwa yeyote athubutuye kupitia eneo lake la mto.

Kwa hiyo ingawa hautazamishi kama mngurumo wa simba, mwayo—uwe ni mwayo wa usingizi, mwayo wa kutisha, au mwayo wa kuongeza nguvu tu—hutimiza kusudi lenye manufaa. Ni kielelezo kingine zaidi cha ubunifu wa kushangaza wa Mbuni wa wanyama!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki