Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 11/8 kur. 10-11
  • Je, Kutakuwako Amani na Utulivu Wakati Wowote?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Kutakuwako Amani na Utulivu Wakati Wowote?
  • Amkeni!—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Vizuizi vya Kushinda
  • Mwisho wa Kelele?
  • Kelele—Yale Uwezayo Kufanya Kuihusu
    Amkeni!—1997
  • Kelele—Kisumbufu cha Kisasa
    Amkeni!—1997
  • Amani ya Kweli—Kutoka Chanzo Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Acha “Amani Ya Mungu” Ilinde Moyo Wako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 11/8 kur. 10-11

Je, Kutakuwako Amani na Utulivu Wakati Wowote?

WALIPOULIZWA walichotafuta kwa kwenda likizo katika nchi nyingine, karibu watalii Waingereza 3 kati ya kila 4 walijibu, “Amani na utulivu.” Lakini uchafuzi wa kelele ukiwa tatizo la ulimwenguni pote, wengi waamini kuwa amani na utulivu halisi ni hadithi ya kuwazika tu.

Yajapokuwa majaribio yenye bidii ili kupunguza uchafuzi wa kelele, huenda ukawaza ikiwa ni jambo lenye uhalisi kuamini kwamba kutakuwako na mafanikio kamili wakati wowote. Namna gani wengine wasioshiriki hangaiko lako?

Vizuizi vya Kushinda

Si rahisi kuongea na watu usiokubaliana nao kwa maoni na ni vigumu hata zaidi kuwafanya waelewe maoni yako. Wakati makundi ya matineja wenye kelele walipokusanyika nje ya jengo ambapo Ron aliishi, alichukua hatua ya kwanza kufanya urafiki nao. Akayajua majina yao. Hata aliwasaidia kurekebisha moja ya baiskeli zao. Tangu wakati huo, hajapata matatizo zaidi kutoka kwao.

Fikiria kisa cha Marjorie, mzazi aliye pekee wa binti tineja, ambaye huishi katika nyumba iliyo katikati ya majirani wenye kelele. Wapangaji walio juu yake hawana zulia kwenye sakafu yao. Kwa sababu hiyo, Marjorie hupata kwamba kelele za watoto wakikimbia sakafuni wakiwa na viatu vyenye magurudumu, wakidunda mpira, au hata kuruka kutoka kitandani humsumbua. Kwa kuongezea, mama yao huvaa viatu vyenye visigino virefu akiwa nyumbani. Marjorie alimwendea jirani yake kwa upole kumwomba apunguze kelele, lakini alikatishwa tamaa na kutoelewana katika lugha. Manispaa yao imejitolea kumtuma mkalimani kusaidia kutatua tatizo hilo, kwa hiyo Marjorie angojea marekebisho.

Anayeishi katika nyumba iliyo chini yake ni mwanamume ambaye hucheza muziki kwa sauti ya juu kati ya saa moja na saa mbili kila asubuhi, mdundo wa besi ukipiga daima. Alipomwendea mwanamume huyo kwa busara alipata jibu la kwamba aliuhitaji muziki wake ili ‘awe katika hali njema kwa ajili ya kazi yake.’ Majorie akabilianaje?

“Najitahidi kuwa mwenye kujidhibiti na mwenye subira,” Marjorie asema. “Nimeipanga upya programu yangu, na ninaketi kusoma ijapokuwa kuna kelele. Napata kwamba ninazama upesi katika kukisoma kitabu changu. Kisha siisikii kelele hiyo sana.”

Kwa upande ule mwingine, Heather, huishi katika jengo linaloelekeana na klabu ya usiku, ambayo baada ya usiku wenye kelele, hufungwa karibu saa kumi na mbili alfajiri. Hata ingawa hatimaye alilalamika kwa wenye mamlaka za kwao, machache yamefanywa ili kumaliza usumbufu huo.

Mwisho wa Kelele?

“Watu wengi huona ukimya wa kabisa kuwa kwenye kusumbua na wenye kutia woga sana,” aonelea Dakt. Ross Coles wa Taasisi ya Utafiti wa Kusikia ya Baraza la Utafiti wa Kitiba la Uingereza. Nyimbo tamu za ndege, kuvuma kwa uanana kwa mawimbi juu ya ukingo wenye mchanga, milio yenye msisimuko ya watoto—hizi na sauti nyinginezo hutufurahisha. Ingawa sasa huenda tukatamani kiasi fulani cha kitulizo cha kutokuwa na kelele, twafurahia kuwa na waandamani wenye kujenga wanaozungumza nasi. Mungu ameahidi amani na utulivu kwa watumishi wake waaminifu.

Katika Biblia mtunga-zaburi atangaza: “Wenye upole watairithi nchi, watajifurahisha kwa wingi wa amani.” (Zaburi 37:11) Serikali ya kimbingu ya Ufalme wa Mungu karibuni itayaingilia mambo ya kibinadamu. (Danieli 2:44) Kisha, chini ya utawala wa Kristo Yesu, kutakuwako “wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.”—Zaburi 72:7; Isaya 9:6, 7.

Waweza kuwa na uhakika kwamba kuingilia kati kwa Mungu kutaleta amani na utulivu ambao sisi sote twatamani, kama vile nabii wa Mungu, Isaya, alivyotabiri: “Kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. Na watu wangu watakaa . . . katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.”—Isaya 32:17, 18.

Hata sasa, waweza kupata amani na utulivu wa kiroho katika vikusanyiko vya Mashahidi wa Yehova katika eneo lako. Ingawa katika pindi fulani makumi ya maelfu yao hukusanyika pamoja ili kuabudu katika mikusanyiko mikubwa—na vikusanyiko hivi huwa kwa kweli vyenye ‘kelele vikiwa na wanaume, wanawake, na watoto’—sauti si yenye kusumbua bali yenye kupendeza. (Mika 2:12, NW) Pata kujionea mwenyewe kwa kukusanyika pamoja na Mashahidi katika eneo lako au kwa kuwaandikia kwa kutumia mojawapo ya anwani zilizo kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili ili uwasiliane nao. Furahia amani na utulivu halisi katika uandamani wao sasa na labda milele.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki