Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 2/22 kur. 18-19
  • Waandishi wa Habari wa Urusi Wawasifu Mashahidi wa Yehova

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Waandishi wa Habari wa Urusi Wawasifu Mashahidi wa Yehova
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Mashahidi wa Yehova Nchini Urusi
    Amkeni!—1997
  • Moscow—Ukumbusho Wake wa Miaka 850
    Amkeni!—1997
  • ‘Ulimwengu Wetu Ungekuwa Tofauti’
    Amkeni!—2000
  • Ushindi wa Kisheria Baada ya Kupambana kwa Muda Mrefu!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 2/22 kur. 18-19

Waandishi wa Habari wa Urusi Wawasifu Mashahidi wa Yehova

MAJENGO ya ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova huko Urusi yaliwekwa wakfu Juni 21, 1997. Majengo haya yanatia ndani makao saba, Jumba la Ufalme kubwa, chumba cha kulia, na jengo kubwa la ofisi na bohari. Linapatikana karibu kilometa 40 kaskazini-magharibi ya St. Petersburg, katika kijiji cha Solnechnoye.

Programu ya kuwekwa wakfu ilipokea utangazaji mkubwa kupitia waandishi wa habari ambao walialikwa kuhudhuria. Mmoja wao aliandika katika Literaturnaya gazeta la Moscow, jarida lililo na nakala zinazogawanywa zaidi ya robo milioni: “Wazo la kwanza unapoliona huwa ni, Hapa pana mfano wa jengo lililo bora!”—Ona picha kwenye ukurasa wa 16 na 17.

Mwandishi, Sergey Sergiyenko, alieleza: “Kazi yote ilifanywa na Mashahidi wa Yehova: Kazi ya ujenzi ilifanywa hasa na watu kutoka Finland, Sweden, Denmark, Norway, na Ujerumani. Barabara safi za matufali; nyanja za nyasi zilizofyekwa vizuri; majengo yenye paa za vigae vilivyo na sura nzuri, madirisha makubwa, na milango ya vioo—hiki ni kituo cha usimamizi cha tengenezo la kidini la Mashahidi wa Yehova katika mkoa wa Urusi.”

Waandishi wa habari kutoka Moscow, iliyo zaidi ya kilometa 650 kusini-mashariki mwa ofisi ya tawi, walialikwa kwenye kuwekwa wakfu na wakaandaliwa usafiri. Walitalii majengo hayo wakiwa chini ya mwelekezo, na baadaye, kipindi cha maswali na majibu kilifuata, wakati ambapo viburudisho viliandaliwa. Kwa kutegemea oni lake, Bw. Sergiyenko aliandika:

“Mashahidi, kama usemavyo msemo, ni wenye kiasi na wasiojidai . . . Kunukuu msemo wa Kirusi ulio maarufu, ‘Mashahidi huishi kwenye [nyumba yao] kana kwamba kwenye kifua cha Yehova.’ . . . Bila ugeugeu ni wenye fadhili kwa watu wote, bila shaka, Mashahidi, huwajali ndugu zao kwa njia ya pekee.”

Makala iliyoandikwa na S. Dmitriyev ilitokea katika Moskovskaya Pravda, gazeti la kila siku lenye nakala zinazogawanywa karibu 400,000. Katika makala yake yenye kichwa “Unaweza Kujenga Ulimwengu Wako Mwenyewe kwa Mikono Yako Pekee,” mwandishi alifafanua:

“Baada ya tengenezo la kidini la Mashahidi kutambuliwa kisheria katika Urusi [katika 1991], swali lilitokea kuhusu ujenzi wa makao yao makuu. Walikuwa wakitafuta mahali karibu na Moscow wakati ambapo ripoti isiyotazamiwa ilipokuja kwamba eneo la kambi ya hapo zamani ya vijana karibu na St. Pete[rsburg] lilikuwa linauzwa. Shamba hilo lilinunuliwa, na wakaanza kujenga. . . .

“Mwaka mmoja na nusu uliopita, Januari 1, 1996, sehemu ya katikati ya kijiji cha Solnechnoye ikawa tawi rasmi la tengenezo hilo la kidini. Katikati ya mwezi wa Juni, kikundi cha waandishi wa habari wa Moscow kiliweza, kwa kutumia muda fulani katika St. Pete[rsburg], kuwa na fursa ya kujaribu kutambulisha, Hawa Mashahidi wa Yehova ni akina nani?”

Jibu la Bw. Dmitriyev lilikuwa gani? “Wao ni watu wa kawaida.” Na bado, wao ni tofauti, kama alivyoandika katika umalizio wa makala yake: “Wana amani miongoni mwao wenyewe, amani kuzunguka pote. Je, ni ndoto? Ndiyo. Na bado ipo.”

Mwandishi mwingine wa habari wa Moscow, Maksim Yerofeyev, akiandika kwa niaba ya Sobesednik, gazeti la habari lenye nakala zinazogawanywa zaidi ya 300,000, alionelea: “Uhusiano wote katika jumuiya hii ndogo umejengwa juu ya kanuni hii ifuatayo: Hakuna mtu yeyote anayelazimishwa kufanya kazi, na bado kila mtu anajitolea kufanya kazi.”

Baada ya kufafanua makazi anakoishi mratibu wa Halmashauri ya Tawi, Vasily Kalin, Bw. Yerofeyev alionelea: “Shirika letu lisiloaminika la ripota lilitaka kuzuru vyumba vingine lilivyochagua. Saizi na fanicha pamoja na vyombo vya makazi ya wakazi wale wengine kimsingi havikutofautiana na mpango wa kiasi uliokuwa katika chumba cha Vasily Kalin.”

Ripota mwingine, Anastasiya Nemets, aliandika makala “Kuwa na Amani ya Akili.” Kichwa kidogo cha habari kwa hicho kichwa kikuu katika Vechernyaya Moskva kilikuwa “Hili Ndilo Jambo Watu Wanalojifunza Katika Kijiji Kisicho cha Kawaida Kilicho Nje ya St. Pete[rsburg].”

Akifafanua mahali na sura ya majengo ya ofisi ya tawi, aliandika: “Kuzunguka pote kuna misitu na makonde ya majani. Ile Ghuba ya Finland haiko mbali sana. Hapa pana nyumba ndogo safi zilizojengwa kwa mtindo wa Ulaya, barabara safi zilizofagiliwa vizuri zenye kutiwa kibamba kwa matufali, na matuta ya maua yenye kupendeza.

“Viwanda vya kibiashara hujenga miji midogo ya namna hiyo kwa ajili ya ‘Warusi wenye utajiri.’ Hata hivyo, watu walio na mapato ya kiasi wanaishi katika kijiji hiki . . . Wanaishi kwa starehe, na lililo la maana zaidi, wanaishi kama marafiki. Hapa pana watu karibu 350 tu, kutoka pembe zote za dunia; mtu aweza kusikia lugha za namna mbalimbali zikisemwa—kutoka Kihispania na Kireno mpaka Kifinland na Kisweden.

“Kiasili, huu ni mfano mwakilishi uliozingiwa: Kijiji hiki kina maduka yake yenyewe ya kutokeza bidhaa na utengenezaji, ambapo inawezekana kutayarisha kitu chochote ambacho familia kubwa yenye kusema lugha nyingi inahitaji; wao hata wana kliniki yao wenyewe.”

Kwa kweli, kuwekwa wakfu kulikuwa sherehe yenye shangwe kwa wale 1,492 kutoka nchi 42 waliohudhuria huko Solnechnoye. Wengi waliokuwako walikuwa wale walio na umri mkubwa ambao walitumikia kwa miongo kadhaa wakati kazi ya kuhubiri ilipokuwa imepigwa marufuku. Je, waweza kuwazia mshangao uliotamkwa na shangwe ya hawa watumishi wa muda mrefu walipokuwa wakitalii majengo haya mazuri yaliyo katika kikao hiki kilicho kama bustani, cha eka 17? Inaeleweka kwamba wangefikiri walikuwa wanaota ndoto.

[Picha katika ukurasa wa 18]

Waandishi wa habari wakitalii majengo ya ofisi ya tawi

Kipindi cha maswali na majibu

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki