Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 3/8 kur. 3-4
  • Waweza Kuitumaini Sayansi Kadiri Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Waweza Kuitumaini Sayansi Kadiri Gani?
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuinuka kwa Sayansi
  • Sayansi—Jitihada Inayoendelea ya Ainabinadamu ya Kutafuta Kweli
    Amkeni!—1993
  • Kupatanisha Sayansi na Dini
    Amkeni!—2002
  • Mashahidi wa Yehova Wana Maoni Gani Kuhusu Sayansi?
    Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi Kuhusu Mashahidi wa Yehova
  • Sayansi Isemapo Unasikilizaje?
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 3/8 kur. 3-4

Waweza Kuitumaini Sayansi Kadiri Gani?

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA AUSTRALIA

WATU wengi kwa kweli husifu sayansi kwa kustaajabia, kwa sababu ya matimizo yake mengi katika tiba, uhandisi, uwasiliano, na nyanja nyinginezo. Uvumbuzi mbalimbali wa kisayansi umeathiri karibu maisha ya watu wote wanaoishi leo. Wanasayansi wengi wametoa maisha yao yote kwa sayansi, na jitihada za sayansi zenye kufuatia haki na zinazokusudiwa kuboresha maisha zastahili kupongezwa. Kwa hakika, mtungaji Tony Morton afikia hatua ya kusema kwamba “bila shaka sayansi ni mojawapo ya nguzo za ustaarabu wa kisasa.”

Lakini katika sehemu zote za maisha, kuna uhitaji wa usawaziko katika kukadiria thamani halisi ya mambo, na eneo la sayansi limetiwa ndani. Ili kutusaidia kudumisha mwelekeo wenye usawaziko kama huo, hebu tuchunguze maneno ya mwandikaji mwingine, ambaye hasifu sana fungu la sayansi katika maisha zetu. Lewis Wolpert, katika kitabu chake The Unnatural Nature of Science, aandika: “Uchunguzi huthibitisha kwamba kuna upendezi zaidi katika sayansi, nayo inasifiwa kwa kustaajabu, na pia kuna itikadi isiyofaa kwamba sayansi yaweza kuondoa matatizo yote; lakini wengine pia, wana hofu ya ndani sana na uhasama . . . Wanasayansi huonwa kuwa wataalamu wasio na shauku, wenye usiri, na wasiojali.”

Kuinuka kwa Sayansi

Sikuzote kuna kujasiria katika kufanya uvumbuzi mpya. Lakini kadiri uvumbuzi mpya uthibitishavyo kwamba kujasiria hufaa, uhakika wa umma katika sayansi huongezeka. Kwa kadiri fulani, sayansi inapofurahia utukufu wa mafanikio ya wakati uliopita, imejasiria zaidi na zaidi, na watu wengi wenye kicho na shauku wamekuja kuiona sayansi kuwa suluhisho la matatizo ya binadamu. Tokeo ni kwamba watu wengi huhusisha maneno “sayansi” na “kisayansi” na kweli kabisa.

Kichapo American Studies chatoa maoni haya: “Kuanzia miaka ya 1920, na zaidi katika miaka ya 1930, mwanasayansi katika koti jeupe la maabara aliwahakikishia wateja kuwa bidhaa moja ilikuwa bora zaidi ‘kisayansi’ kuliko nyinginezo. Uhariri wa jarida la Nation la 1928 uliomboleza kwamba ‘sentensi inayoanza kwa “Sayansi husema” kwa ujumla itasuluhisha bishano lolote katika kikusanyiko cha jamii, au kuuza bidhaa yoyote kuanzia na dawa ya meno hadi friji.’”

Lakini je, sikuzote sayansi husema kweli kabisa? Katika muda wote wa historia uvumbuzi wa kihistoria umekuwa na wapinzani wenye bidii. Vipingamizi fulani vilivyozushwa havikuwa na msingi; vingine vilionekana kuwa na msingi mzuri. Kwa kielelezo, uvumbuzi wa Galileo, ulizusha ghadhabu ya Kanisa Katoliki. Na nadharia za kisayansi kuhusu chanzo cha binadamu ulitokeza uhasama kwa misingi ya kisayansi na ya Kibiblia. Kwa hiyo haishangazi kuwa kila uvumbuzi mpya wa kisayansi huvutia waungaji mkono na wapingaji.

Mithali moja ya zamani ya Kilatini husema: “Sayansi [au, ujuzi] haina adui ila wasio na ujuzi.” Hata hivyo, hiyo si kweli tena kwa sababu leo sayansi inashambuliwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote—na si na wasio na ujuzi. Sasa yaonekana kwamba ingawa wakati mmoja ilionekana kuwa isiyoweza kushambulika na wengi, sasa sayansi inashambuliwa na watu fulani ambao wakati mmoja walikuwa wakiiunga mkono. Idadi inayoongezeka ya wanaoiunga mkono wanaweza kusemwa kuwa wamekuwa mahakimu wake, baraza lake la mahakama, na mfishaji wake. Vituo vikubwa vya kujifunzia sayansi mara nyingi sasa huwa viwanja vya mapambano. Sababu moja ya ole huo ni kuwa udanganyifu na ufisadi wa wakati uliopita wa baadhi ya wataalamu hao wa kisayansi sasa umejulikana.

Hivyo, swali hili laulizwa mara nyingi zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote, Je, kweli sayansi yote yaweza kutumainiwa? Makala ifuatayo yaorodhesha baadhi ya sababu zinazofanya idadi inayoongezeka ya watu wazushe swali hili.

[Blabu/Picha katika ukurasa wa 4]

Je, sikuzote sayansi husema kweli kabisa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki