Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 4/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ugonjwa wa Malengelenge Katika Viungo vya Uzazi Waongezeka
  • Kanisa la Uingereza Ladidimia
  • Mume Amshtaki Mke kwa Kuvuta Sigareti
  • Ngamia-Mwitu wa Australia
  • Kutiwa Sumu ya Aseniki
  • Mama Wanaofanya Kazi
  • Kufilisika Kwawa Jambo la Kawaida
  • Mazoea ya Uvuvi Yenye Kuharibu
  • Maadili ya Matineja Katika Uingereza
  • Je, Kweli Abrahamu Alikuwa na Ngamia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Mahali Ngamia na Farasi Hurandaranda
    Amkeni!—2001
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1999
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 4/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Ugonjwa wa Malengelenge Katika Viungo vya Uzazi Waongezeka

“Ujapokuwa mkazo juu ya ngono salama ili kuzuia UKIMWI, ugonjwa wa malengelenge katika viungo vya uzazi umeongezeka mara tano tangu mwisho-mwisho wa miaka ya 1970 miongoni mwa matineja weupe” katika Marekani, yasema ripoti ya Associated Press. Hata hivyo, ilionwa kwamba magonjwa mengine yenye kuambukizwa kingono, kama vile kisonono, yalipungua katika kipindi hicho hicho. Kwa nini kulikuwa na ongezeko katika ugonjwa wa malengelenge? Miongoni mwa sababu zilikuwa ongezeko la ngono ya kabla ya ndoa na watu kuwa na wenzi wengi wa kufanya ngono nao. Sasa inakadiriwa kuwa Wamarekani milioni 45 wameambukizwa na virusi vya malengelenge katika viungo vya uzazi, na wengi wao hawajui. Virusi hivyo hutokeza vidonda mara kwa mara au kuwashwa katika sehemu za uzazi na wakati mwingine kuzunguka matako au kwenye mapaja.

Kanisa la Uingereza Ladidimia

Kadirio rasmi la hudhurio la Kanisa la Uingereza kila Jumapili ni milioni moja. Kwa faragha, makasisi wenye vyeo hukiri kwamba kunaweza kuwa na chini ya asilimia 25 ambayo huhudhuria makanisa yao. Hata hivyo, ukaguzi wa kisayansi huonyesha kwamba ushiriki wenye kina, wale wapokeao Komunyo, umepungua kufikia nusu milioni kwa mara ya kwanza. Kwa nini makasisi wako tayari kutia chumvi tarakimu zao za hudhurio? Kwa msingi, ili wazuie makanisa yao yasifungwe. Wakati hilo litokeapo, parokia huunganishwa pamoja, na makasisi wachache huhitajiwa. Kasisi mmoja wa parokia alikuwa mwenye kufuatia haki vya kutosha kusema: “Nina mwelekeo wa kutia chumvi hesabu ya wahudhuriaji. Inavunja moyo wakati watu wachache wahudhuriapo, kwa hiyo hunipa kitia-moyo kurekodi kwamba kwa kweli wengi zaidi walikuwapo,” laripoti The Sunday Times la London.

Mume Amshtaki Mke kwa Kuvuta Sigareti

Kwa zaidi ya miaka 20, Richard Thomas aliomba-omba na kusihi katika jitihada za kumfanya mke wake aache kuvuta sigareti, lakini hakufanikiwa. Kwa hiyo alimpeleka mahakamani. Bw. Thomas alisema kwamba alitaka serikali imlinde dhidi ya kupoteza upendo na utegemezo na uandamani wa mke aliyempenda. Tayari alikuwa amempoteza mama yake kwa sababu ya maradhi ya moyo, kisha baba yake aliugua mshtuko wa akili ambao ulimfanya alazwe kitandani kwa miaka saba. Wazazi wake wote wawili walikuwa wavutaji wa sigareti wa kupita kiasi, na alisema kwamba hakutaka kumpoteza mke wake kwa uraibu wa nikotini. Hata hivyo, kabla mahakama haijaweza kutoa uamuzi, Bw. Thomas alirudi akiwa na habari njema. “Mke wangu amekubali kuacha kuvuta sigareti,” akasema. Bi. Thomas alijiunga na kituo cha kutibu uraibu na akaweka nadhiri ya kuacha kuvuta sigareti kabisa. Kulingana na The New York Times, walipokuwa wakitoka katika chumba cha mahakama, Bwana na Bibi Thomas walikuwa wameshikana mikono.

Ngamia-Mwitu wa Australia

Ngamia waliingizwa Australia miaka mingi iliyopita wafanye kazi ya kutengeneza laini ya simu na reli kuvuka mbuga ya nchi isiyopendeza. Wakati mahali pa wanyama hawa wenye nguvu palipochukuliwa na malori, wengi wa Waafghani waliomiliki wanyama hao waliwaachilia waende mwituni badala ya kuwachinja. Ngamia hao walisitawi katika sehemu ya kati ya Australia iliyo kavu, na leo ngamia wapatao 200,000 wanapatikana hapo. Sasa watu wengi wanaamini kwamba ngamia waweza kuwa raslimali ya kitaifa yenye thamani, laripoti gazeti la habari The Australian. Tayari nyama ya ngamia inapatikana na wanunuzi fulani na inasemekana kuwa ni nyororo kama ya ng’ombe na kuwa na kiwango cha chini cha mafuta. Bidhaa nyingine za ngamia zinatia ndani ngozi iliyo tayari, maziwa, sufu, na mafuta kwa matumizi ya sabuni na vipodozi. Ngamia walio hai wanahitajika pia. Kulingana na Peter Seidel, wa Kiwanda cha Ngamia cha Australia ya Kati, “bustani nyingi za kimataifa za wanyama na mbuga za watalii zinataka ngamia wa Australia kwa sababu tuna kundi la ngamia wasiokuwa na maradhi.”

Kutiwa Sumu ya Aseniki

“Karibu watu milioni 15 wa Bangladesh na watu milioni 30 wa Bengal Magharibi, kutia ndani Calcutta, wamefunuliwa kwa sumu ya aseniki,” laripoti The Times of India. Tatizo hilo ni zaotuka la ongezeko kubwa la kutokeza nafaka. Wakati visima vyenye vina virefu vilipochimbwa kwa ajili ya kumwagilia maji mazao, aseniki ya kiasili iliyo katika ardhi iliingia ndani ya maji, na hatimaye ilipenya ndani ya visima vinavyotumiwa kwa ajili ya maji ya kunywa. Mtaalamu wa mazingira Willard Chappel, wa Chuo Kikuu cha Colorado, Marekani, hivi karibuni alizuru maeneo yaliyoathiriwa na kufafanua tatizo hilo kuwa “ndicho kisa cha kusumishwa kwa matungamo ya watu kilicho kikubwa zaidi ulimwenguni.” Tayari watu zaidi ya 200,000 wanataabishwa na vidonda vya ngozi, ishara ya kusumishwa na aseniki. “Inaonekana kuwa tulitatua tatizo la njaa (kupitia ongezeko la utoaji wa nafaka), na kutokeza taabu zaidi katika hatua hiyo,” akasema Ishak Ali, ofisa wa serikali kutoka Bangladesh.

Mama Wanaofanya Kazi

Katika mwaka wa 1991 Shirika la Kitaifa la Wanawake Wanaofanya Kazi lilikadiria kwamba “kufikia katikati ya miaka ya 1990, asilimia 65 ya wanawake [Wamarekani] walio na watoto ambao bado hawajaenda shule na asilimia 77 ya wale walio na watoto wenye umri wa kwenda shule watakuwa wamejiunga na kikosi cha wafanyakazi.” Utabiri wao ulikuwa sahihi jinsi gani? Katika mwaka wa 1996, kulingana na Shirika la Marekani la Sensa, asilimia 63 ya wanawake walio na watoto wenye umri unaopungua miaka mitano walikuwa wameajiriwa, laripoti The Washington Post. Kwa wanawake walio na watoto wenye umri wa kwenda shule, asilimia 78 kati yao ilikuwa mama wanaofanya kazi. Namna gani Ulaya? Kwa kutegemea habari iliyokusanywa na Ofisi ya Takwimu ya Muungano wa Ulaya, “uwiano wa mama wanaofanya kazi walio na watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 16” katika nchi za Ulaya katika mwaka wa 1995 ulikuwa Ureno asilimia 69, Austria 67, Ufaransa 63, Finland 63, Ubelgiji 62, Uingereza 59, Ujerumani 57, Uholanzi 51, Ugiriki 47, Luxembourg 45, Italia 43, Ireland 39, na Hispania 36.

Kufilisika Kwawa Jambo la Kawaida

Katika mwaka wa 1996 “Wamarekani milioni 1.2 waliovunja rekodi walijitangaza rasmi kuwa wamefilisika, ongezeko la asilimia 44 kutoka mwaka wa 1994,” lataarifu gazeti Newsweek. “Kufilisika kumekuwa jambo la kawaida sana hivi kwamba kumepoteza fedheha yake.” Ni nini linalochangia ongezeko la kufilisika? Sababu moja ni kwamba “wengi wanazidi kukubali kufilisika kuwa chaguo la mtindo-maisha mwingine tu,” lasema Newsweek. “Wadaiwa wanasema kwamba badiliko katika mtazamo linaongoza kwenye kutumiwa vibaya kwa hali ya kufilisika: uchunguzi mmoja unaonyesha kwamba asilimia 45 ya waliojitangaza rasmi kuwa wamefilisika wangeweza kulipia sehemu kubwa ya deni lao.” Lakini badala ya kuonyesha tamaa ya kulipa deni na kuwa na hisi ya aibu, wengi wasema tu, ‘Ninahitaji kuanza upya.’ Watu mmoja-mmoja wengi zaidi na zaidi wanaona mashirika yakijitangaza rasmi kuwa yamefilisika, na pia wanashawishwa na matangazo ya wanasheria yanayosema “tatua matatizo yako ya deni upesi na kwa urahisi!” Hesabu inapoendelea kuongezeka wakati uchumi unapositawi haraka, wataalamu wanahofia wanapofikiri ni nini linaloweza kutukia ikiwa soko la hisa litaporomoka au kushuka kwa uchumi.

Mazoea ya Uvuvi Yenye Kuharibu

Kundi la meli za kibiashara za uvuvi zinatega fedha ili kupata kifaa cha kusaka sakafu ya bahari katika kutafuta idadi ya samaki inayozidi kudidimia. Ili kuchota spishi ambazo hapo awali zilipuuzwa, kifaa hiki cha bonde la bahari, kinachojulikana kuwa zana inayoweza kwenda, hukokotwa kandokando ya sakafu ya bahari kwa vina vikubwa vinavyofikia meta 1,200. Tatizo ni kwamba idadi kubwa za “tube worms, wanyama wa jamii ya yavuyavu, anemone, hydrozoan, urchin, na walowezi wengine wa kilindi” wananaswa katika hatua hii na “kutupwa kama takataka,” laripoti Science News. Kuwaangamiza huongezea uhaba wa mikatale ya samaki. Kwa sababu wanyama hawa huandaa chakula na makao kwa samaki wadogo, Elliot Norse, mkurugenzi wa Chuo cha Biolojia ya Hifadhi ya Wanyama wa Baharini katika Redmond, Washington, Marekani, asema kwamba kuharibiwa kwa kao la majini kwa njia hii ya uvuvi kwaweza kulinganishwa na “kufyeka kabisa misitu ya nchi.”

Maadili ya Matineja Katika Uingereza

Ripoti ya hivi majuzi inadokeza kwamba mashirika ya kidini katika Uingereza yanashindwa kukaza kikiki katika matineja adili za kingono. Chuo Kikuu cha London kiliwauliza matineja 3,000 “kama ni kosa kiadili kwa wenzi wasiofunga ndoa ambao wamekuwa na uhusiano wa muda mrefu kufanya ngono.” Kama ilivyotarajiwa, karibu wote ambao walijieleza kuwa waatheisti au waagnosti walisema la. Hata hivyo, asilimia 85.4 ya Wakatoliki wa Kiroma na asilimia 80 ya Waanglikana pia walisema kwamba halikuwa kosa. Tarakimu zilifanana kwa dini nyingine nyingi, ambazo zilionwa kuwa kikundi kimoja-kimoja—kutia ndani Waislamu, Wayahudi, Wahindu, na wengineo. Ukaguzi huo “utatokeza habari zenye kuvunja moyo kwa wale walio makanisani ambao wanajaribu kutegemeza viwango vya kidesturi vya adili za kingono,” laeleza The Times la London.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki