Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 5/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Watoto Wako Salama Wakiwa na Mbwa Wako?
    Amkeni!—1997
  • Jinsi ya Kumzoeza Mbwa Wako
    Amkeni!—2004
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 5/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Ugonjwa Hisia zangu ziliguswa na ile makala “Vijana Huuliza . . . Naweza Kukabilianaje na Kuwa Mgonjwa Sana?” (Juni 22, 1997) Navutiwa na Jason, Ashley, na Carmen kwa jinsi wanavyoshughulika vizuri sana na ugonjwa wao.

R. D., Ufaransa

Shauri mnalotoa kwa kweli ni lenye kutumika, lenye kuchochea, na lenye matokeo. Nilitiwa moyo hasa na simulizi la Ashley. Mimi ni mhudumu wa wakati wote wa Mashahidi wa Yehova. Wazo la kwamba kuna watu ambao wangekuwa na hamu sana ya kuingia katika utumishi wa wakati wote lakini wasioweza kwa sababu ya afya limenitia moyo kuvumilia licha ya magumu niliyo nayo.

D. I., Albania

Tangu nilipojua kwamba nina maradhi ya Crohn, nimelazwa hospitali zaidi ya mara kumi na kuhitaji kufanyiwa upasuaji mara mbili. Hata hivyo, kwa miaka minne iliyopita, nimetumika katika eneo lisilofanyiwa kazi hapa katika nchi ya kigeni. Na ingawa bado afya yangu si kamili, imeboreka kwa njia ya ajabu sana. Makala hizo zilikuwa kitia-moyo kikubwa sana kwangu.

G. H., Ekuado

Wanyama wa Pori Wanaotoweka Ninajifunza zuolojia, na ule mfululizo “Ni Nani Atakayeokoa Wanyama Wetu?” kwa kweli uligusa hisia zangu. (Julai 8, 1997) Natumaini kwamba watu wasomao makala hizi hutambua jinsi ambavyo pupa na ukatili imeathiri spishi nyingi.

G. H., Marekani

Nikiwa mpenda-wanyama wa pori mwenye shauku, nilipendezwa kusoma makala zenu. Bustani za wanyama zinafanya kazi nyingi ili kusaidia spishi zilizohatarishwa. Lakini ikiwa bustani za wanyama ndilo tumaini la mwisho kwa wanyama wa pori, basi kwa hakika wanyama wa pori wako taabani. Kuwaondoa wanyama kutoka kwenye mazingira yao ya asili na kuwalea katika bustani za jiji sio kitatuzi.

M. T., Kanada

Ingawa jitihada kama hizo za kuhifadhi zastahili pongezi, twaamini kwamba kitatuzi cha kudumu katika kusimamia raslimali za dunia ni Ufalme wa Mungu. (Isaya 11:9)—Mhariri.

Usalama wa Mnyama Rafiki Ningependa kuwashukuru kwa ajili ya makala “Je, Watoto Wako Salama Wakiwa na Mbwa Wako?” (Julai 8, 1997) Nimekuwa mtaalamu wa kufunza mbwa kwa miaka 18 na sikuzote nimekuwa nikikazia umuhimu wa kuzoeza na kuchukua daraka la kibinafsi. Nilifurahi kwa mshangao kusoma makala hii yenye kuelimisha na kufurahi kuona kwamba mfunzi aliyehojiwa hutumia namna ileile ya mazoezi tunayotumia. Ninatumaini kwamba watu wote walio na mbwa watasoma na kutumia shauri hili.

B. C., Marekani

Ningependa kuongeza hoja moja: Kwa kuongozwa na silika, mbwa huitikia chakula kwa wepesi. Mtoto anayepunga soseji katika mkate au peremende huku akitembea na kupita mbele ya mbwa aweza kuwa shabaha. Mbwa hakusudii kuwa mkali, lakini aweza kurukia chakula hicho, na wakati hili linapofanyika, aume mkono wa mtoto. Wazazi wanashauriwa vema kuchukua daraka lao kwa habari hii.

K. S., Marekani

Twathamini uchunguzi huu wa ziada.—Mhariri.

Mitindo-Maisha Yenye Kudhuru Afya Nilithamini makala “Mitindo-Maisha Yenye Kudhuru Afya—Inagharimu Kadiri Gani?” (Julai 22, 1997) Nikiwa kijana Mkristo, nakabili vishawishi vingi. Lakini makala hizi kwa kweli zilifanya nione kwamba kwa kufuata kanuni za Biblia, tunaepuka maradhi na majeraha.

R. K., Marekani

Ngoma Zinazozungumza Baada ya kusoma ile makala ya kustaajabisha “Je, Kweli Ngoma za Kiafrika Huzungumza?” (Julai 22, 1997), nilimwendea babu yangu, mwenye umri wa miaka mia, ili kujaribu kuhakikisha ukweli wa hadithi hiyo. Aliithibitisha kikamili, na nilivutiwa sana!

G. M. O., Nigeria

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki