Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 7/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 7/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Usalama wa Mnyama Rafiki Katika makala “Je, Watoto Wako Salama Wakiwa na Mbwa Wako?” (Julai 8, 1997), mlipendekeza kuweka kitanda cha mbwa jikoni. Hata hivyo, katika makala zilizotangulia mlisema kwamba twapaswa kuepuka kuwa na wanyama rafiki katika sehemu za kutayarishia chakula kwa sababu za usafi wa kiafya.

R. H., Hispania

Twathamini oni hili. Makala yetu ilikuwa ikikazia usalama wa watoto, na haikushughulikia mambo ya usafi wa kiafya. Kwa hiyo tungependekeza wasomaji wachunguze makala “Fanya Ulaji Wako Uwe Salama” (Aprili 8, 1990), ambayo ilitaarifu hivi: “Wanyama vipenzi na wanyama wengineo wapasa kuzuiwa wawe mbali na maeneo ya kutayarishia chakula.” Labda kibanda cha mbwa kilicho nje au chumba kilicho nje ya jiko kingekuwa mahali panapofaa kulala mbwa.—Mhariri.

Maisha Huku Chini Nataka kutoa shukrani za kutoka moyoni kwa ajili ya makala yenye uchangamfu na vilevile yenye kusisimua kuhusu Australia, yenye kichwa “Maisha Ni Tofauti Huku Chini.” (Oktoba 8, 1997) Ijapokuwa nimesoma mambo mengi kuhusu nchi hii yenye kuvutia na kupendeza, makala yenu ilinisaidia kuelewa kwa nini twapaswa kuwa wenye shukrani kwa Yehova kwa ajili ya uumbaji huu wa kustaajabisha.

L. K., Ujerumani

Paradiso Isiyo na Taabu Nawashukuru sana kwa ajili ya mfululizo “Paradiso Isiyo na Taabu—Lini?” (Oktoba 8, 1997) Nyanya yangu alikufa kabla sijazaliwa. Alikufa kwa kansa. Lakini katika Paradiso, hakutakuwa na ugonjwa tena. Makala hii ilinitia moyo nidumu nikiwa mwaminifu ili niweze kumwona katika Paradiso.

M. J., Trinidad

Usingizi wa Wanyama Nataka kuwashukuru kwa ajili ya makala “Siri za Usingizi wa Wanyama.” (Oktoba 8, 1997) Ilichekesha—na nilijifunza ajabu fulani za uumbaji.

J. G., Puerto Riko.

Nina samaki kipenzi, na sikuzote nimetaka kujua ikiwa samaki hulala. Kwa hiyo nilifurahi kugundua kwamba nimwonapo akiwa ametulia, huwa anapumzika tu.

A. P. L. M., Brazili

Nyayo Zinazouma Yaonekana makala yenu “Msaada kwa Nyayo Zinazouma” (Oktoba 8, 1997) iliandikwa hasa kwa ajili ya wanawake. Hata hivyo, siku chache baada ya kusoma makala hiyo, mume wangu alilalamika kuumwa na nyayo—na amekuwa akilalamika hivyo kwa miaka saba. Nikikumbuka tuliyosoma kwenye makala hiyo, tulienda kwenye duka la viatu. Amini usiamini—alikuwa akivaa viatu vya saizi 8 ya kadiri na kumbe alihitaji saizi 9 pana! Tayari amepata nafuu, asante kwa Amkeni!

S. J., Marekani

Mimi husimama karibu siku nzima niwapo kazini, na nilianza kupatwa na matatizo kwa sababu ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu. Mwezi huu nimefanya upainia-msaidizi (mweneza-evanjeli wa nusu wakati), na kwa msaada wa makala hiyo nilinunua jozi tatu za viatu vinavyostarehesha. Asanteni kwa kupendezwa na afya yetu na kwa kuendelea kutuarifu.

C. L., Ujerumani

Vita na Watoto Asanteni sana kwa ajili ya mfululizo “Mambo Ambayo Vita Huwafanyia Watoto.” (Oktoba 22, 1997) Kwa kweli hutusaidia kuelewa jinsi tunavyohitaji sana Ufalme wa Yehova ili kukomesha matokeo mabaya ya vita. Kwa kweli zilikuwa makala zenye kuelimisha, zikituonyesha ukatili tusioujua ulio katika nchi nyinginezo.

Y. C., Uingereza

Sipendi kusoma juu ya kusumbuliwa kwa watoto. Hivi sasa nakaribia kulia. Hunichukiza kikweli kuona ulimwengu ukigeuka kuwa jamii ya wanadamu wasiojali. Nawapongeza kwa uwazi wenu katika kutoa makala hii yenye kuelimisha.

K. E., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki