Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 6/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 6/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Uwezo wa Kusikia Nataka kuwashukuru kwa ile makala “Uwezo Wako wa Kusikia—Zawadi ya Kuthaminiwa Sana.” (Septemba 22, 1997) Kabla ya kusoma makala hiyo, nilifikiri kwamba najua sana utendaji wa sikio na jinsi tunavyosikia. Lakini, sikutambua jinsi ambavyo sikufahamu mambo mengi. Ule mchoro ulio katika ukurasa wa 23 ulikuwa mzuri ajabu! Nimeshangaa kwa kufikiri kwingi na jitihada nyingi zilizofanywa ili kutokeza mchoro huo wa sikio. Na nimeshangaa hata zaidi kwa hekima ya Yule aliyefanyiza sikio!

A. S., Marekani

Mimi na rafiki yangu ni wataalamu wa kitiba, na tunaamini kwa unyoofu kwamba katika miaka yetu mingi ya masomo ya kilimwengu, hatujapata kusoma makala ambayo inafafanua sikio kwa usahili na kwa usahihi sana kama hiyo. Makala hiyo inatufanya tukubaliane na maneno ya Zaburi 139:14: “Nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.”

M. B. na Z. B., Venezuela

Mimi nilikuwa mhasiriwa wa dereva mlevi. Baada ya kupoteza fahamu kwa mwezi mmoja, niliamka bila uwezo wa kusikia. Baada ya miaka 18 bado siwezi kusikia vizuri, lakini kwa msaada wa vifaa vya kusaidia kusikia, sasa ninaweza kusikia kwa kiwango fulani. Makala hii ya wakati unaofaa inasaidia sana wale ambao wanaweza kusikia wawahurumie wale ambao wana matatizo ya kusikia.

K. C., Marekani

Kilimanjaro Nilifurahia sana kusoma makala “Kilimanjaro—Kilele cha Afrika.” (Septemba 8, 1997) Niliona Mlima Kilimanjaro mnamo Januari 1994 nilipohudhuria mkusanyiko wa kimataifa wa Mashahidi wa Yehova nchini Kenya. Nilivutiwa kwelikweli na mwono wake nikamshukuru Yehova kwa ajili ya uumbaji wake wa ajabu akiwa Muumba wetu mwenye upendo.

E. J., Marekani

Si Sehemu ya Ulimwengu Nilipenda sana makala “Maoni ya Biblia: ‘Si Sehemu ya Ulimwengu’—Yamaanisha Nini?” (Septemba 8, 1997) Baada ya kuisoma, niliamua kuacha kutumia neno “walimwengu” ninaporejezea watu ambao si Wakristo. Kwani, miaka 30 iliyopita, mimi mwenyewe sikuwa Mkristo. Ikiwa mtu ambaye alinionyesha Biblia kwa mara ya kwanza angekuwa na mtazamo wenye kiburi, basi huenda ningalikataa kuzungumza na Shahidi yeyote tena!

B. G., Marekani

Walaghai Sikuchukua wakati wa kusoma ule mfululizo wenye kichwa “Jihadhari na Walaghai!” nilipopokea mara ya kwanza toleo la Septemba 22, 1997. Kesho yake, sisi wanne tulilaghaiwa na dereva mmoja wa teksi aliyeonekana kuwa mwenye urafiki kwa sababu hatukujua jiji hilo. Tulifanywa tulipe pesa nyingi sana na kushukishwa mbali sana na mahali tulipotaka kwenda. Laiti tungalitumia maneno ya Mithali 14:15, yaliyonukuliwa mwishoni mwa hizo makala: “Mjinga huamini kila neno; bali mwenye busara huangalia sana aendavyo”!

J. P., Filipino

Krusedi Nilikuwa nikifanya utafiti fulani juu ya Krusedi nilipopokea toleo la Oktoba 8, 1997, lenye makala “Zile Krusedi—‘Uwongo Wenye Msiba.’” Kwa kweli sisi hupokea habari kwa wakati ufaao! Nilikumbushwa juu ya umaana wa kusoma magazeti mara tu niyapokeapo.

T. K., Finland

Paradiso Isiyo na Taabu Nina umri wa miaka tisa, na nataka kuwashukuru kwa makala “Paradiso Isiyo na Taabu—Karibuni Itakuwa Halisi.” (Oktoba 8, 1997) Makala hiyo ilinigusa moyo sana kwa kuwa babangu alisafiri nje ya mji, na usiku mimi na mamangu tumekuwa na woga wa hata kufungua dirisha kwa sababu huenda mtu akaingia katika nyumba. Basi nilifarijika niliposoma jinsi Yehova anavyoahidi kuondoa uhalifu na ujeuri wote.

D. M., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki