Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 5/8 kur. 14-15
  • “Upendo Haushindwi Kamwe”—Je, Wewe Hushindwa Kuuonyesha?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Upendo Haushindwi Kamwe”—Je, Wewe Hushindwa Kuuonyesha?
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Upendo (Agape)—Usivyo na Ulivyo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • “Endeleeni Kutembea Katika Upendo”
    Mkaribie Yehova
  • Upendo katika Matendo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • “Katika Hayo Lililo Kuu ni Upendo”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 5/8 kur. 14-15

“Upendo Haushindwi Kamwe”—Je, Wewe Hushindwa Kuuonyesha?

UPENDO ni nini? Kote ulimwenguni, kuna methali ambazo hukazia thamani ya upendo wa kweli. Methali ya Kizulu husema, “Upendo hauchagui ni unyasi upi utakaouangukia.” Katika Filipino watu husema, “Upendo ndiyo chumvi ya maisha.” Methali ya Kilebanoni hutaarifu, “Upendo huachilia kasoro lakini chuki hukuza kasoro.” Inayofanana na hiyo ni methali ya Ireland isemayo, “Upendo husitiri ubaya.” Watu wa Wales husema, “Upendo ni wenye nguvu kuliko jitu.” Watu wa Norway husema, “Kile kipendwacho huwa kizuri sikuzote.” Mwingereza aweza kusema, “Kiasi kidogo cha upendo ni chenye thamani kuliko sheria chungu nzima.” Katika Hispania kuna msemo, “Upendo wa kweli hudumu hadi kifo.”

Bila shaka, upendo wa kweli huthaminiwa kokote tuendako. Upendo uwezao kufanya tofauti ya kweli katika maisha ni ule uelezwao na mwandikaji wa Biblia Paulo: “Upendo ni wenye ustahimilivu na wenye fadhili. Upendo hauna wivu, haujigambi, haujitutumui, haujiendeshi bila adabu, hautafuti masilahi yao wenyewe, haupati kuwa wenye kuchokozeka. Hauweki hesabu ya ubaya. Haushangilii ukosefu wa uadilifu, bali hushangilia pamoja na kweli. Huhimili mambo yote, huamini mambo yote, hutumaini mambo yote, huvumilia mambo yote. Upendo haushindwi kamwe.”—1 Wakorintho 13:4-8.

Ndiyo, “upendo haushindwi kamwe.” Upendo huponya. Upendo huunganisha. Upendo huonyeshwa si kwa maneno tu bali kwa matendo yasiyo ya kibinafsi. Upendo una nia safi. Hivyo, Paulo pia aliandika: “Nami nikitoa mali zangu zote kulisha wengine, nami nikiutoa mwili wangu, ili nipate kujisifu, lakini sina upendo, sifaidiki hata kidogo.” Tukitoa dhabihu au kutoa zawadi ili kwamba tuonekane tu na wengine, basi machoni pa Mungu ni bure.—1 Wakorintho 13:3.

Yesu alisema hivi: “Wakati uendapo kutoa zawadi za rehema, usipulize tarumbeta mbele yako, kama vile wanafiki hufanya . . . ili wapate kutukuzwa na watu. Kwa kweli nawaambia nyinyi, Wanapata thawabu yao kwa ukamili. Lakini wewe, unapotoa zawadi za rehema, usiache mkono wako wa kushoto ujue lile ambalo mkono wako wa kuume unafanya.” Ndiyo, upendo haujisifu wala kujigamba.—Mathayo 6:2, 3.

Upendo usio na unafiki hautafuti mapendezi yake wenyewe. Upendo wa kweli hufanya mtu mwenye upendo aburudishe mkiwa naye. (Mathayo 11:28-30) Nukuu lifuatalo lisilotambulishwa laweza kutusaidia tufikiri kuhusu aina ya upendo tulionao kuelekea wengine: “Uadilifu bila upendo hutufanya tuwe wasio na fadhili. Imani bila upendo hutufanya tuwe washupavu. Uwezo bila upendo hutufanya tuwe wa kinyama. Wajibu bila upendo hutufanya tuwe wenye shingo ngumu kupita kiasi. Kuwa wenye utaratibu bila kuwa na upendo hutufanya tuwe wenye akili finyu.”

Watu wanaoishi tu kwa sheria wanaweza kuanguka katika mtego wa kuwa wasio na upendo. Sote twaweza kuwa wenye kujenga kadiri gani ikiwa tutaishi kulingana na shauri la Paulo: “Jivikeni wenyewe shauku nyororo za huruma, fadhili, hali ya akili ya kujishusha chini, upole, na ustahimilivu. Endeleeni kuchukuliana mtu na mwenzake na kusameheana kwa hiari mtu na mwenzake ikiwa yeyote ana sababu ya kulalamika dhidi ya mwingine. Kama vile Yehova alivyowasamehe nyinyi kwa hiari, fanyeni hivyo nyinyi pia. Lakini, zaidi ya mambo haya yote, jivikeni wenyewe upendo, kwa maana huo ni kifungo kikamilifu cha muungano.”—Wakolosai 3:12-14.

[Picha katika ukurasa wa 15]

Wakristo wa kweli huzoea upendo kama Yesu alivyoufundisha

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki