Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 7/8 uku. 31
  • Wakati Kufa Kumaanishapo Kufa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakati Kufa Kumaanishapo Kufa
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Inakuwaje kwa Wapendwa Wetu Waliokufa?
    Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele
  • Kuna Sababu ya Kuwaogopa Wafu?
    Amkeni!—2009
  • Jizoeze Imani Ili Upate Uhai wa Milele
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kuna Tumaini Gani kwa Wapendwa Waliokufa?
    Kuna Tumaini Gani kwa Wapendwa Waliokufa?
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 7/8 uku. 31

Wakati Kufa Kumaanishapo Kufa

“Maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa; kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.”—Mhubiri 9:4, 5.

WATU wengi wana itikadi fulani isiyo dhahiri kuhusu kuendelea kuishi kwa nafsi baada ya kifo au watu kuendelea kuishi katika maumbo mengine mapya. Wengine hata huamini kwamba mtu aweza kurudi kuishi tena baada ya kifo. Hivi karibuni Thomas Lynch, msimamizi wa mazishi, aliulizwa maoni yake kuhusu maisha baada ya kufa. Alisema hivi: “Watu ambao hupata maono kabla tu ya kufa hawakurudi kutoka kwa wafu—walifikiriwa tu kuwa walikufa kwa sababu hatukuweza kutambua dalili za kuwa walikuwa hai. Kwa sababu ‘ukifa’ huwezi kurudi.”—The New York Times Magazine.

Kwa maelfu ya miaka Biblia imetaarifu ukweli kuhusu habari hii. “Ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa; kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.” (Mhubiri 9:4, 5) Unaweza kuthibitisha ukweli huo kwa urahisi kwa kuzuru kifupi tu makaburi ya kale.

Je, hilo lamaanisha kwamba hakuna tumaini lolote kwa waliokufa? Bila shaka Biblia haina msingi wowote wa kuitikadi nafsi isiyoweza kufa ambayo huendelea kuishi baada ya kifo. (Mwanzo 2:7; Ezekieli 18:4, 20) Hata hivyo, Yesu Kristo alihubiri juu ya ufufuo kwenye uhai katika dunia iliyo paradiso itakayorudishwa. Mfuasi wake Myahudi Martha, ambaye ndugu yake Lazaro alikuwa amekufa muda mfupi, aliamini katika ufufuo, kwa kuwa alisema hivi kuhusu Lazaro: “Najua atafufuliwa katika ufufuo siku ya mwisho.” (Yohana 11:24) Yesu akamjibu: “Mimi ndio ufufuo na uhai. Yeye ambaye hudhihirisha imani katika mimi, hata ingawa afa, atakuja kwenye uhai; na kila mtu aliye hai na hudhihirisha imani katika mimi hatakufa hata kidogo kabisa. Je, unaamini hili?” (Yohana 11:25, 26) Mapema alikuwa amesema hivi: “Msistaajabie hili, kwa sababu saa inakuja ambayo katika hiyo wote wale waliomo ndani ya makaburi ya ukumbusho watasikia sauti yake na kutoka, wale waliofanya mambo mema kwenye ufufuo wa uhai, wale waliozoea kufanya mambo maovu kwenye ufufuo wa hukumu.” Lakini ona kwamba Yesu hakutaja nafsi isiyoweza kufa!—Yohana 5:28, 29; Luka 23:43.

[Blabu katika ukurasa wa 31]

“‘Ukifa’ huwezi kurudi.” Thomas Lynch, msimamizi wa mazishi

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki