Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 10/8 uku. 3
  • Ukosefu wa Usalama—Tatizo la Tufeni Pote

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ukosefu wa Usalama—Tatizo la Tufeni Pote
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mahangaiko Katika Ulaya
  • Usalama wa Kibinafsi
  • Je, Ulaya Itaungana Kweli?
    Amkeni!—2000
  • Maadili Yakoje Leo?
    Amkeni!—2000
  • Kutafuta Maisha Yenye Usalama
    Amkeni!—1998
  • Maisha Yenye Usalama wa Kudumu
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 10/8 uku. 3

Ukosefu wa Usalama—Tatizo la Tufeni Pote

JE, NYAKATI fulani wewe huhisi kwamba maisha yako na mtindo-maisha wako waweza kudhuriwa kwa urahisi na hauna uhakika? Si wewe peke yako. Mamilioni ya watu huhisi hivyo. Bila kuzuiwa na mipaka ya kitaifa, kidini, au kijamii, ukosefu wa usalama unaenea kama maradhi, ukiwaathiri watu kutoka Moscow hadi Manhattan.

Kulingana na kamusi moja, wakati maisha yetu yakosapo usalama, “tunakuwa na hofu na usumbufu.” Hangaiko ni mzigo wa kihisia-moyo ambao hutokeza mkazo unaoweza kuharibu afya yetu. Lakini kwa nini sisi huhangaika na kukosa usalama?

Mahangaiko Katika Ulaya

Katika Muungano wa Ulaya (EU), mtu 1 kati ya watu 6 huishi katika umaskini wa kupindukia, watu milioni 18 hawana kazi za kuajiriwa, na wengine wasiohesabika wanaishi wakiwa na hofu ya kupoteza kazi zao. Katika nchi kadhaa za EU, wazazi wanaogopeshwa na tisho linalokabili watoto wao la kutendwa vibaya na watu wanaovutiwa na watoto kingono. Katika nchi moja ya EU, watu 2 kati ya 3 wanahangaishwa na tisho la uhalifu. Wakazi wengine wa EU wanahisi hofu iliyoongezeka kwa sababu ya uharibifu wa vitu, ugaidi, na uchafuzi.

Maisha na riziki zimo hatarini si kwa sababu ya upotovu wa kijamii tu bali pia kwa sababu ya misiba ya asili. Kwa kielelezo, katika mwaka wa 1997 na 1998, mvua nyingi sana, maporomoko ya matope, na chamchela ziliharibu sehemu za Marekani. Katika mwaka wa 1997, mafuriko yalikumba Ulaya ya Kati wakati mito Oder na Neisse ilipofurika. Kulingana na gazeti la kila juma la Poland Polityka, maeneo makubwa ya kilimo yaligharikishwa, vilevile majiji 86 na miji na vijiji vipatavyo 900. Familia zipatazo 50,000 zilipoteza mazao yao, na karibu watu 50 wakapoteza uhai wao. Na mapema katika mwaka wa 1998 maporomoko ya matope yaliua makumi ya watu katika kusini mwa Italia.

Usalama wa Kibinafsi

Lakini je, hatuna uhakikisho wa kwamba maisha ni salama zaidi ya yalivyokuwa miaka kumi iliyopita? Je, kuisha kwa vita baridi hakukumaanisha kupunguzwa kwa majeshi? Ndiyo, huenda usalama wa kitaifa ukawa umeboreka. Hata hivyo, usalama wa kibinafsi huathiriwa na mambo yanayotokea nyumbani na barabarani. Tukipoteza kazi yetu au tukishuku kwamba kuna jambazi au mwenye kunajisi watoto anavizia huko nje, tunakuwa na hangaiko na kukosa usalama hata kama silaha zilizoharibiwa ni nyingi kadiri gani.

Watu wengine wanakabilianaje na ukosefu wa uhakika wa maisha? La maana zaidi, je, kuna njia ya kufanya maisha ya kila mtu—kutia ndani yako—yadumu yakiwa salama? Hoja hizi zitazungumziwa katika makala mbili zitakazofuata.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

UN PHOTO 186705/J. Isaac

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

FAO photo/B. Imevbore

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki