Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 10/8 kur. 26-27
  • Mambo Mawili juu ya Msiba

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mambo Mawili juu ya Msiba
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Watu wa Yehova Wachukua Hatua
  • Matokeo Mazuri
  • Mambo Ambayo Kimbunga Andrew Hakingeweza Kuharibu
    Amkeni!—1993
  • Upendo wa Kikristo Kati ya Misiba Katika Mexico
    Amkeni!—1996
  • Waliokoka kwa Kutii Maonyo
    Amkeni!—2006
  • “Wale Wanaokusikiliza” Wataokolewa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 10/8 kur. 26-27

Mambo Mawili juu ya Msiba

Na mleta-habari wa Amkeni! katika Mexico

GODOFREDO na Gisela, wenzi waliofunga ndoa ambao ni Mashahidi wa Yehova, pamoja na watoto wao walikuwa ndani ya nyumba yao iliyojengwa kwa mbao zilizotandazwa lami wakati Kimbunga Pauline kilipokumba pwani ya Oaxaca, Mexico. Bati moja baada ya jingine liling’olewa na upepo. Hatimaye, wakati sehemu ya fremu tu ilipobaki, familia hiyo ilibaki bila makao kabisa.

Gisela akiwa amembeba mikononi mtoto mwenye umri wa miezi minane na watoto wengine watatu wakijishikilia kwenye mikono yake na ya Godofredo, waling’ang’ana na pepo zenye nguvu kwa muda uzidio saa mbili. Nyakati fulani, nguvu ya kimbunga ingewaangusha chini na kuwabingirisha sakafuni. Mwishowe, wote waliokoka.

Katika Acapulco, mmoja wa Mashahidi wa Yehova aliyeitwa Nelly alipoona maji yakija nyumbani mwake, aliamsha familia yake. Maji yalizidi kuongezeka kwa kasi sana, na kani ya mkondo ikamburuta Nelly chini ya maji, lakini binti yake akamtoa. Walijishikilia kwenye vyuma vya dirisha na kutazama tu maji yakipanda kufikia shingo zao wakiwa hawana namna. Kisha wakasikia sauti ya mtu ikiwaita. Alikuwa jirani yao; aliwasaidia kutoka na kisha kuwapeleka kwenye nyumba yao. Wakiwa kwa jirani, walitazama kwa hofu gari likivunjavunja kabisa nyumba waliyokuwa ndani yake dakika chache zilizotangulia.

Mnamo alasiri ya Jumatano, Oktoba 8, 1997, Kimbunga Pauline kikakumba pwani ya jimbo la Oaxaca kikiwa na pepo zenye kusafiri kwa mwendo wa kilometa 200 kwa saa moja. Kisha, mnamo Alhamisi, Oktoba 9, saa za alfajiri, kimbunga hicho kikaharibu jimbo la Guerrero, hasa jiji la Acapulco, kikiinua mawimbi kwa kimo cha meta 10 na kusababisha gharika ambayo ilipeleka nyumba, magari, wanyama, na watu. Kufikia wakati dhoruba ilipoendelea kusonga, kulikuwa na mitaro yenye kina kinachozidi meta 10 mahali palipokuwa na barabara. Kulingana na gazeti la habari The News, shirika la Msalaba Mwekundu katika Mexico lilitoa kadirio la ujumla la watu waliokufa kuwa angalau 400 na 20,000 hadi 25,000 waliachwa bila makao katika majimbo hayo mawili. Lakini, katika msiba huu, kulikuwa na wonyesho wenye kugusa moyo wa upendo wa Kikristo.

Watu wa Yehova Wachukua Hatua

Mara tu habari kuhusu Kimbunga Pauline zilipojulikana, ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika Mexico ilianza kupokea simu kutoka kwa Mashahidi nchini kote waliotaka kujua namna ambavyo wangeweza kusaidia. Msaada ulitolewa pia kutoka ng’ambo. Halmashauri ya kutoa msaada ilifanyizwa haraka, tani za vyakula, mavazi, na vitu vingine vikagawanywa.

Pia, vifaa vya ujenzi vililetwa, na kazi ya kurekebisha nyumba 360 na Majumba ya Ufalme kadhaa yaliyoharibiwa ikaanza mara moja. Maelfu ya akina ndugu na dada Wakristo walikuwa na shughuli za kutoa msaada, kuainisha, kupakia, kusafirisha, na kupeleka vifaa au kufanya kazi ya marekebisho.

Wenye maduka kadhaa walivutiwa sana na utendaji wa Mashahidi hivi kwamba walichanga kwa fadhili vyakula, vifaa vya ujenzi, na vitu vinginevyo. Wengine wakawauzia vifaa kwa bei ya chini. Mashahidi walioathiriwa waliguswa moyo sana na upendo walioonyeshwa, hasa waliposoma barua zenye kutia moyo zilizotiwa ndani ya maandalizi hayo.

Kwa ubaya, José Faustino—Shahidi mwenye umri wa miaka 18—na watu watatu waliokuwa wakijifunza Biblia pamoja na Mashahidi waliuawa na kimbunga hicho. Jamaa zao, hasa wazazi wa José, wamethamini sana sala zilizotolewa kwa niaba yao na kitia-moyo walichopewa na kutaniko.

Matokeo Mazuri

Baada ya Kimbunga Pauline kutokea watu wengi waliomba funzo la Biblia, kutia ndani jamaa wasioamini wa Mashahidi, na majirani wengi walikuwa tayari zaidi kusikiliza ujumbe wa tumaini wa Mashahidi. Pia, Mashahidi walishiriki ugawanyaji wa kawaida wa chakula cha kutuliza. Katika kisa kimoja, Shahidi alipomwuliza mtu mmoja kwa nini alichagua Mashahidi wa Yehova kugawanya chakula kilichotolewa na kampuni yake, mtu huyo alijibu: “Kwa sababu najua kwamba nyinyi ni watu wenye utaratibu na wenye kufuatia haki. Mbali na hilo, mnajua kwelikweli ni nani aliye na uhitaji mkubwa zaidi kwa msaada huu, kwa kuwa mnawajua watu katika eneo lenu.”

Mwisho ukaribiapo na misiba mingi zaidi iongezekapo ulimwenguni pote, sikuzote linakuwa jambo lenye kutia moyo kuona kanuni za Biblia zikitumika, hata majanga yanapotokea.

[Picha katika ukurasa wa 26]

Vijana wasaidia katika kazi ya kujenga upya

[Picha katika ukurasa wa 27]

Mashahidi wakijenga Jumba la Ufalme jipya katika Oaxaca baada ya Kimbunga Pauline

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki