Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 5/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • ‘Yehova Ameufanya Uso Wake Ung’ae Kuwaelekea’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Lugha Ambayo Waiona!
    Amkeni!—1998
  • Wathamini Ndugu na Dada Zako Viziwi!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Jinsi Mungu Anavyowajali Viziwi
    Habari Zaidi
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 5/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kujiua kwa Vijana Ningependa kuwashukuru kwa ajili ya makala mfululizo “Vijana wa Leo Wana Tumaini Gani?” (Septemba 8, 1998) Niliguswa sana hadi nikalia. Nimejaribu kujiua mara kadhaa. Lakini ninafurahi kwamba sikufaulu.

A. Z., Jamhuri ya Cheki

Hizi zilikuwa makala zenye kutoa uelewevu juu ya habari inayohitaji kushughulikiwa kwa busara. Mapema mwaka huu nilijaribu kujiua nilipoelezwa na daktari kuwa nilikuwa na mshuko-moyo. Asanteni kwa habari hii ya wakati wake. Iliokoa uhai wangu.

R. P., Uingereza

Inasikitisha sana kwamba, wanadarasa wenzangu wawili wamejaribu kujiua. Mmoja wao alifanya hivyo kwa sababu alipofikiri juu ya wakati ujao, yeye hakuona jambo lolote lenye kutumainisha—ila tu magumu yaliyohitaji kushindwa. Kwa hiyo makala hii ilikuwa yenye kutumika, kwa kuwa ilieleza kwa njia ya wazi sana na hususa jinsi wakati wetu ujao unavyoweza kuwa na kusudi.

R. D., Hispania

Makala yenu iliugusa moyo wangu. Ilikuwa kana kwamba Yehova alikuwa akiongea nami kama Baba mwenye upendo. Nilipokuwa mtoto, nilitendwa vibaya na baba yangu. Nimekuwa nikihisi sifai na mara nyingi nimefikiria kujiua. Lakini sasa, kama makala yenu ilivyodokeza, ninakuza tamaa ya “uhai ulio halisi.”—1 Timotheo 6:19.

S. R., Brazili

Asanteni, hasa kwa sababu ya manukuu kutoka kwa vijana, mengi yake yakiwa na utatuzi wa matatizo kwa maneno machache tu.

W. H., Ujerumani

Kuchuma Pesa Asanteni sana kwa ajili ya wakati mliotumia kuchapisha makala yenye kuelimisha yenye kichwa “Vijana Huuliza. . . Naweza Kuchumaje Pesa?” (Agosti 22, 1998) Ilikuwa vigumu kwangu kupata kazi ya kuajiriwa. Lakini nilifuata mapendekezo yenu na ndipo nilipopata kazi hatimaye!

S. D., Ghana

Lugha ya Ishara Baada ya kusoma makala yenu “Lugha Ambayo Waiona!” (Septemba 8, 1998), ilinilazimu kuwaandikia ili kuwashukuru. Makala kama hii hutusaidia kuwaelewa wengine walio katika hali zinazotofautiana na zetu. Nina rafiki aliyezaliwa akiwa kiziwi, na nimekuwa nikitaka kujifunza lugha ya ishara. Lakini kwa sababu moja au nyingine, sijafaulu kamwe kupata wakati wa kujifunza. Sitaahirisha tena kamwe kujifunza lugha hiyo!

M. E., Uingereza

Ningependa kuwashukuru kwa ajili ya jitihada yenu kubwa ya kuwategemeza viziwi. Niliwapa maofisa wa serikali nakala kadhaa za makala yenu. Waliomba nakala zaidi, kwa sababu makala hiyo iliandikwa kwa njia bora sana! Nilimwonyesha pia mwanamke aliyempinga binti yake kiziwi kujifunza Biblia pamoja na Mashahidi wa Yehova. Baada ya kusoma makala hiyo, alitokwa na machozi ya shangwe. Sasa anaunga mkono jitihada za binti yake za kuhudhuria mikutano na hata ameahidi kumlipia nauli ya kwenda kwenye mkusanyiko wa Kikristo!

E. R., Mexico

Nimelazimika kuwajulisha jinsi ambavyo nilithamini makala hiyo. Nilikuwa na mradi wa kujifunza Lugha ya Ishara ya Marekani ili nisaidie katika kutaniko la Mashahidi wa Yehova la mahali hapa la lugha ya ishara. Lakini nilikuwa nimevunjika moyo. Makala hiyo ilinipa kitia-moyo nilichohitaji ili kufikia mradi wangu!

N. D., Marekani

Ilivutia sana kujifunza kwamba Viziwi kwa hakika hufikiri katika lugha yao ya ishara. Kwa kuwa nina uwezo wa kusikia, nitakuwa mwangalifu kutafuta njia zinazofaa zaidi za kuwasiliana na Viziwi.

P. H., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki