Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 9/22 uku. 31
  • Ni Yenye Thamani Zaidi Kuliko Fedha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Yenye Thamani Zaidi Kuliko Fedha
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Watu Wanyoofu Humletea Yehova Sifa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Latvia Yaitikia Habari Njema
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Ninapaswa Kujua Nini Kuhusu Kutendewa Vibaya Kingono?​—Sehemu ya 2: Kupata Msaada
    Vijana Huuliza
  • Jinsi Matumaini Yangu Yalivyotimizwa
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 9/22 uku. 31

Ni Yenye Thamani Zaidi Kuliko Fedha

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA KANADA

“[Ali]mpa binti yake zawadi yenye thamani zaidi kuliko kiasi chochote kile cha fedha,” yakakiri maelezo ya uhariri katika gazeti la habari The Monitor la Bridgetown, Nova Scotia. Zawadi hiyo ilikuwa nini? Ilikuwa “kielelezo chake kizuri ajabu cha ufuatiaji wa haki.”

Anna na binti yake Tanya walitua kwenye mitumba na kununua kibeti cheupe cha kubebea Biblia ya Tanya. Walipofika nyumbani, Tanya alifungua zipu ndani ya kibeti na akashangaa kupata dola 1,000 za Kanada. Mara hiyo, mama na binti wakarudi kwenye mitumba na kumpatia fedha yule bibi aliyewauzia kibeti hicho. Kumbe, kibeti hicho ambacho hakikuwa kimetumiwa mara nyingi kilikuwa cha mama yake aliyekufa karibuni, aliyekuwa akiugua maradhi ya Alzheimer, nacho hakikuwa kimechunguzwa vizuri kabla ya kuuzwa. Akiwa mwenye shukrani sana, bibi huyo alisema hivi: “Inanifanya niamini watu tena . . . Inatia moyo kujua kwamba kungali kuna watu wenye kufuatia haki.”

Makala ya ukurasa wa mbele katika gazeti la habari la mahali hapo likitaja kisa hicho lilimnukuu Anna akisema hivi: “Tukiwa Mashahidi wa Yehova, hatungeweza kufanya jambo jingine zaidi ya hilo. Tuna [dhamiri] inayotegemea Biblia. Twataka kumfundisha Tanya lililo sawa.” Kwa Tanya, kibeti hicho kipya cheupe kitakuwa kumbukumbu ya pekee ya somo la ufuatiaji wa haki.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki