Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 10/8 kur. 3-4
  • Uvutano wa Muziki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uvutano wa Muziki
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Sababu Inayofanya Tuhangaike
  • Jilinde na Muziki Usiofaa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Muziki Waweza Kweli Kuniumiza?
    Amkeni!—1993
  • Ninaweza Kuwa na Usawaziko Jinsi Gani Kuhusu Muziki?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Je, Utafanya Maamuzi Yenye Hekima?
    Amkeni!—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 10/8 kur. 3-4

Uvutano wa Muziki

“Muziki peke yake wenye kuvutia kwa ghafula unaweza kutuliza hali ya kutangatanga, na kutuliza akili iliyovurugika.”

NDIVYO alivyoandika William Congreve katika kitabu chake Hymn to Harmony yapata miaka 300 iliyopita. Karne nyingi kabla ya hapo, maandishi ya kale ya Kigiriki yalidai kwamba “mazoezi ya muziki ni ala yenye uvutano mkubwa zaidi ya nyinginezo zote, kwa sababu mfuatano na upatano wa muziki hupenya kabisa ndani ya nafsi.”

Ukweli wa jambo hilo umeonwa na wazazi fulani ambao wamewaona matineja wao wakiwa na kinyongo na kukosa kuonyesha ushirikiano baada ya kusikiliza muziki wenye mdundo mzito. Jambo hilo lilionekana pia katika miaka ya 1930 na 1940 huko Ujerumani wakati Wanazi walipotumia muziki wenye kuamsha hisia ili kutayarisha halaiki za watu wasikilize hotuba za Adolf Hitler za kupumbaza akili.

Bila shaka, muziki unaweza kuathiri akili na mioyo na unaweza kutumiwa kuiongoza kwa hila ama kwa wema ama kwa ubaya. Kwa kielelezo, inaaminiwa kwamba watoto wachanga wanaposikiliza muziki wa aina fulani wanaweza kuboresha uwezo wao wa akili na wa hisia-moyo. Hata vigugumizi nyakati fulani wanaweza kuimba sentensi ambazo hawawezi kuzisema.

Tokeo la muziki kwa wagonjwa walio na maradhi ya mfumo wa neva yanayosababisha kasoro za kusogea, nyakati nyingine linashangaza, kulingana na Anthony Storr katika kitabu chake Music and the Mind. Storr ataja mfano wa mgonjwa mmoja mwanamke: “Akiwa amelemazwa kabisa na ugonjwa wa kutetemeka [Parkinson’s], hangeweza kusonga kwa vyovyote hadi pale alipokumbuka tuni fulani alizojua wakati wa ujana wake. Tuni hizo zingemfanya aweze kusonga tena.”

Sababu Inayofanya Tuhangaike

Kwa hiyo inaonekana kwamba uwezo wa muziki unaweza kunufaisha. Hata hivyo, kuna hatari kwamba watu wafisadi au wenye pupa waweza kutumia uwezo wa muziki kuwa chombo cha kufisha. Uchunguzi fulani umeonyesha uhusiano wa moja kwa moja uliopo kati ya tabia ya kujitenga na watu na aina fulani za muziki.

Kikiunga mkono madai hayo, kichapo Psychology of Women Quarterly charipoti: “Kuna uthibitisho fulani unaodokeza kwamba athari za kutazama vidio za roki ni sawa na kutazama ponografia katika maana ya kwamba wanaume walioonyeshwa vidio za roki zenye jeuri walidhihirisha mtazamo sugu na wa uhasama dhidi ya wanawake kuliko wanaume walioonyeshwa vidio za roki zisizo na jeuri.”

Si wanaume peke yao wanaoathiriwa. Wanawake wanaweza kuathiriwa pia. Ripoti hiyohiyo yaongezea: “Wanaume sawa na wanawake waweza kuanza kukubali jumbe zisizofaa za nyimbo hizo kuhusu kukosa thamani kwa wanawake.”

Jarida Sex Roles lakubaliana na mkataa huo, kwa kusema: “Uchunguzi wa hivi karibuni . . . ulifunua kwamba kutoka kwenye hali za familia zisizoridhisha na kutazama vidio za muziki wenye mdundo mzito kulihusiana sana na mitazamo ya kuendekeza ngono na tabia iliyoko miongoni mwa wasichana waliobalehe.” Jeuri iliyo wazi na maneno ya nyimbo yanayokazia ngono katika nyimbo fulani za rapu yalifanya hakimu mmoja mkazi wa Marekani aamue kwamba albamu fulani ya rapu ilikuwa “chafu kulingana na viwango vya jumuiya.”

Je, hakimu huyo alikuwa mkali kupita kiasi? La hasha! Jarida Adolescence lilifikia mkataa kwamba “vijana wanaobalehe pamoja na wazazi wao huripoti mvurugo zaidi katika maisha ya vijana wanaobalehe ambao husikiliza muziki wenye mdundo mzito na wa rapu.” Mvurugo huo unashirikishwa na “tabia ya uchokozi na ya uharibifu” na mafanikio madogo katika masomo.

Kwa kweli, uhusiano uliopo kati ya aina fulani za muziki na ngono, kujiua, na tabia ya kujitenga na watu umethibitishwa. Lakini je, hilo lamaanisha kwamba muziki wote unashirikishwa na matokeo hayo mabaya? Soma makala zifuatazo uone zinasema nini kuhusu habari hiyo.

[Blabu katika ukurasa wa 4]

Muziki unaweza kuathiri mioyo na akili ama kwa wema ama kwa ubaya

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki