Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 10/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Mnara wa Babeli”
  • Wanyama Vipenzi—Je, Ni Bora kwa Afya Yako?
  • Maji Yanapungua
  • Waombaji Wanaojisingizia
  • Kutenda Vibaya Watoto Ulimwenguni Pote
  • Kufanya Kazi Isiyopendeza Ni Hatari kwa Afya
  • Ubongo wa Ndege na Usingizi
  • Hakuna Manufaa Yoyote
  • Baiskeli ya Buku
  • Kupunguza Maumivu ya Mgongo ya Wasafiri
  • Kudhihirisha Hasira
  • Je, Ulaya Itaungana Kweli?
    Amkeni!—2000
  • Sababu ya Mwili Wako Kuhitaji Usingizi
    Amkeni!—1995
  • Maadili Yakoje Leo?
    Amkeni!—2000
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 10/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

“Mnara wa Babeli”

Muungano wa Ulaya (EU) una lugha 11 rasmi, na huenda lugha 10 zaidi zikaongezwa baadaye, laripoti gazeti International Herald Tribune la Paris. Hivi sasa, Tume ya Ulaya, ambayo ni baraza kuu la EU, huajiri idadi ya watafsiri inayozidi mara nne ya idadi ya watafsiri katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, yanayotumia lugha tano tu zilizo rasmi. Japo jitihada za kuunganisha Ulaya na kupunguza utendaji wa EU zinafanywa, matatizo ya lugha hayashughulikiwi. Kila nchi yanachama inatetea lugha yake. “Mnara wa Babeli unashamiri,” gazeti hilo laeleza. Tume hiyo yakabili pia tatizo la “Eurospeak”—lugha isiyo rasmi isiyoeleweka na yenye msamiati mgumu. Kulingana na mtafsiri mmoja, kuwashauri wanasiasa wajieleze kwa ufasaha ni tatizo kwa kuwa “kwa kawaida lengo lao dhahiri ni kunena kwa utata.”

Wanyama Vipenzi—Je, Ni Bora kwa Afya Yako?

“Kupenda wanyama kwaweza kumsaidia mtu aepuke magonjwa mengi,” lasema The Toronto Star. Katika mwongo uliopita, uchunguzi mbalimbali umeonyesha kwamba “wanyama waandamani wanapunguza mkazo, uhitaji wa kumwona daktari na hata huboresha uwezekano wa kupona baada ya kupatwa na mshiko wa moyo. Wanyama waweza kuwasaidia waliopatwa na mshtuko wa akili wapate nguvu tena na huweza kupunguza mahangaiko ya wagonjwa wa akili.” Dakt. Alan Beck, wa Kitivo cha Madawa ya Mifugo katika Chuo Kikuu cha Purdue huko Indiana, Marekani, anaamini kwamba “wanyama hutuliza watu. Wao hukaziwa fikira sana, na kuguswaguswa.” Matokeo hayo yanaweza kuletwa hata ikiwa mnyama huyo si kipenzi cha familia, na hili limetokeza “tiba inayotegemea wanyama.” Hivyo wafanya-kazi fulani wa afya ya akili wamewatia moyo wagonjwa wa akili watumie wakati na mnyama kipenzi, na matokeo yamekuwa bora.

Maji Yanapungua

“Sasa tuna kiasi cha maji kinachopungua nusu ya kiasi tulichokuwa nacho miaka 50 iliyopita kwa kila mtu,” lataarifu The UNESCO Courier. Na inatarajiwa kwamba hifadhi za tufeni pote zitaendelea kupungua. Kupungua sana kwa maji kunaonyesha uhitaji mkubwa wa maji safi kwa sababu ya ongezeko la idadi ya watu, mahitaji ya kilimo, na ujenzi wa viwanda. Wanasayansi wanaochunguza ukosefu wa maji ulimwenguni kwa minajili ya kuchora ramani wameyaita maeneo fulani kuwa “yenye msiba mkuu.” Kwa mujibu wa gazeti Courier, hii yamaanisha kwamba maji yaliyohifadhiwa “hayawezi kutosheleza watu wakati wa tatizo kama ukame.” Laongezea hivi: “Miaka 50 tu iliyopita, hakukuwa na nchi hata moja ulimwenguni iliyokumbwa na tatizo kubwa la kupungua kwa maji. Leo, takriban asilimia 35 ya watu wote huishi bila maji ya kutosha.”

Waombaji Wanaojisingizia

Ingawa waombaji wengi ni fukara kikweli, ripoti moja katika gazeti The Week, linalochapishwa India, inaonyesha kwamba baadhi yao wanajisingizia tu. Katika jimbo la Maharashtra huko India, mwombaji mmoja akitumia mikongojo alisogelea gari lililosimama penye taa za barabarani. Dereva wa gari hilo aliendelea kuzungumza na mpenziwe msichana pasipo kujishughulisha na mwombaji huyo. Kwa hiyo mwombaji akazidi kuombaomba kwa sauti ya juu zaidi. Ndipo dereva huyo alipofungua dirisha la gari na kumsukuma mbali mwombaji, huku akiangusha sarafu zilizokuwa katika bakuli la mwombaji. Yule mwombaji “kiwete” alipona ghafula na kuanza kuvunjavunja kioo cha mbele cha gari kwa mikongojo yake. “Kikundi cha rafiki zake ‘vipofu,’ ‘walemavu’ na ‘viwete’ wenye kujisingizia waliokuwa wakiombaomba kwenye magari mengine wote wakaja kumsaidia,” huku wakivurumisha mawe, vijiti, na mikongojo na hatimaye wakamburuta yule kijana kutoka katika gari lake, likasema The Week. Kuwasili ghafula kwa gari la polisi kuliwafanya waombaji hao watifue vumbi.

Kutenda Vibaya Watoto Ulimwenguni Pote

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), katika Geneva, Switzerland, lakadiria kwamba ulimwenguni pote watoto milioni 40 hutendwa vibaya. Kama ilivyoripotiwa katika The New York Times, uchunguzi uliofanywa katika nchi 19 wa watoto wenye umri unaofikia miaka 14, ulionyesha kwamba asilimia 29 ya wavulana na asilimia 34 ya wasichana wote waliochunguzwa walikuwa wametendwa vibaya kingono. Katika nchi ya Marekani peke yake, likasema shirika la WHO, takriban watoto milioni mbili huumizwa kwa kutendwa vibaya kila mwaka.

Kufanya Kazi Isiyopendeza Ni Hatari kwa Afya

Uchunguzi wa waajiriwa 50,000 huko Ujerumani ulionyesha kwamba afya ya watu wanaofanya kazi ndogo sana iko hatarini kuliko wale wenye shughuli nyingi. “Imethibitishwa kwamba waajiriwa ambao kazi yao inahitaji kurudiwa-rudiwa au wasiokuwa na uhuru huugua mara mbili zaidi ya watu wenye kazi nyingi,” lasema gazeti Augsburger Allgemeine. Watu wanaopatwa na mikazo kazini na wanaokosa kufika kazini kwa muda mrefu ni wale wanaofanya kazi ndogo sana. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wale wanaofanya kazi ndogo sana isiyo ngumu mara nyingi hupatwa na matatizo ya “msongo wa damu, matatizo ya tumbo, na maumivu ya mgongo na viungo.”

Ubongo wa Ndege na Usingizi

Ripoti moja ya Toronto Star inaeleza kwamba kwa muda mrefu wanasayansi wamefahamu kwamba ndege huweza kutazama kwa jicho moja wakati wanapolala, zoea linalowalinda na hatari ya wanyama wanaowinda. Uchunguzi mpya unaonyesha kwamba ndege wanaweza kuamua iwapo watalala kwa ubongo wote au nusu ili kuelekeza jicho linalochungulia. Utafiti uliofanyiwa bata mwitu waliokuwa wakilala kwa mstari ulionyesha kwamba wale waliokuwa mwishoni mwa mstari walitumia thuluthi ya muda wao wa usingizi huku nusu ya ubongo wao ukiwa umeamka. Wale waliokuwa katikati ya mstari walilala kwa ubongo nusu asilimia 12 tu ya wakati. Inaonekana kwamba “hali inapokuwa hatari, ndipo ndege walalapo muda mrefu kwa ubongo nusu,” asema Profesa Niels Rattenborg wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Indiana.

Hakuna Manufaa Yoyote

“Kuvuta sigareti hakuwafanyi watu wawe wembamba,” charipoti kijarida cha University of California Berkeley Wellness Letter. “Wanawake wengi vijana, hasa, huanza kuvuta sigareti wakifikiri kwamba itawasaidia wabaki wembamba.” Lakini uchunguzi wa watu wazima 4,000 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 30 ulionyesha kwamba “baada ya miaka saba, kwa kawaida uzito uliongezeka (kwa kiasi cha wastani kinachozidi nusu kilogramu kwa mwaka), iwapo watu hao ni wavutaji au la.” Makala hiyo yamalizia hivi: “Kudhibiti uzito hakutokani na kuvuta sigareti. Hakuna manufaa yoyote.”

Baiskeli ya Buku

Kampuni moja ya Hong Kong inayouza wanyama vipenzi imebuni “baiskeli ya wanyama vipenzi,” laripoti gazeti New Scientist. Gurudumu la mbele la kichezeo hicho linashabihi kinu cha kuendeshwa kwa miguu, na mnyama kipenzi anapozunguka ndani ya gurudumu hilo, baiskeli husonga. Hata hivyo, endapo mmiliki anahofu kwamba mnyama wake huenda akaumia, anaweza kubonyeza kidude kwenye baiskeli ambacho kinainua gurudumu la mbele. Hivyo, mnyama kipenzi wake anaweza kufanya mazoezi, baiskeli ikiwa imesimama.

Kupunguza Maumivu ya Mgongo ya Wasafiri

Safari yaweza kuwa ngumu kwa wale wenye maumivu sugu ya mgongo. Hata hivyo, The Toronto Star lilitoa madokezo yafuatayo yenye kusaidia. Unapotembea, “vaa viatu vinavyofaa. Viatu vyenye visigino virefu huupinda mwili, na kuusonga uti wa mgongo. . . . Unaposafiri kwa gari, simamisha gari baada ya muda fulani ili ujinyooshe na kutembea-tembea. . . . Tumia mto wa kuuegemeza mgongo” kitini. Badilisha pia mkao unapoketi. Gazeti Star lasema kwamba maumivu yaletwayo na kubeba mizigo yaweza kupunguzwa kwa sababu “unaweza kupata kwa urahisi masanduku ya mizigo ya safari ya namna mbalimbali inayoweza kuburutwa badala ya kubebwa. Hakikisha kwamba sanduku lako lina kipete kirefu vya kutosha ili ulibebe kwa wepesi; haifaidi mgongo wako iwapo utaburuta mzigo ukiwa umeinama kwa kuwa kipete ni kifupi sana.”

Kudhihirisha Hasira

Kupoza hisia zilizochemka, “kwa kupigapiga vifaa kwa hasira—kwa mfano, kupiga mto makonde au kupiga gunia la kufanyia mazoezi ya ubondia—huzidisha badala ya kupunguza vitendo vya jeuri,” laripoti gazeti National Post la Kanada. Dakt. Brad J. Bushman, profesa mshiriki wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Iowa, alisema: “Vyombo vya habari vimeunga mkono kupoza hisia zilizochemka huku vikipuuza kabisa utafiti ulio katika vichapo.” Kwa mujibu wa Post, watafiti pia wamegundua kwamba “vitabu na makala zinazopendekeza ‘kupoza hisia’ kuwa njia inayofaa ya kukabiliana na hasira yamkini zaweza kuendeleza jeuri kwa kuwaruhusu watu wapuuze kujidhibiti kwao.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki