Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 10/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1999
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1999
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2000
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 10/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Uhuru wa Kidini Nimekuwa msomaji wa Amkeni! kwa miongo kadhaa sasa, nami naandika kuonyesha uthamini wangu kwa ule mfululizo wa makala “Uhuru wa Kidini—Je, Unatishwa?” (Januari 8, 1999) Nilijua kwamba kutovumiliana kwa kidini kulikuwapo Ulaya wakati wa ile iitwayo Enzi za Giza na kwamba Kanisa Katoliki lilifanikiwa kuongoza kwa hila wenye mamlaka wazuie watu kuwa na uhuru wao wa dhamiri na dini. Sasa kwa kuwa nimejua kinachotukia Ufaransa leo, najiuliza, ‘Kwa nini nchi hii inaaibisha jina lake kwa kukataza uhuru wa kidini uliohakikishwa?’ Tafadhali wajulisheni mamilioni ya wasomaji wenu matokeo ya hali hiyo. Natumaini kwamba Ufaransa itaonyesha uvumilivu na kuwekea nchi nyingine kielelezo chema.

C. C., Puerto Rico

Kulea Wana Saba Asanteni kwa jambo lililoonwa la Bert na Margaret Dickman kama lilivyosimuliwa katika toleo la Januari 8, 1999. Lilitutia moyo kulea watoto wetu katika njia ambayo itawapa urithi mwema wa kiroho. Watoto wetu watatu walifurahia makala hiyo pia. Sisi huwasikia wakikumbushana juu ya somo alilopata Doug, ambaye hakupata keki yake! Asanteni kwa kuchapisha jambo lenye kutia moyo kama hilo.

S. J., India

Roho Takatifu Ningependa kuwashukuru kwa makala “Maoni ya Biblia: Roho Takatifu ya Mungu Ni Nini?” (Januari 8, 1999) Ijapokuwa nimekuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova kwa miaka kadhaa, sikuzote nataka kujifunza mengi zaidi kuhusu Yehova Mungu. Makala hii ilijibu swali hilo vizuri na ilikuwa rahisi kuelewa. Kadiri ninapomwelewa Yehova na kazi zake, ndivyo ninapojawa na upendo kumwelekea.

Y. B., Urusi

Dhahabu Nilisoma makala yenu “Dhahabu—Uvutio Wake.” (Septemba 22, 1998) Mlisema kwamba majeshi ya Muungano yaligundua dhahabu nyingi mno katika machimbo ya chumvi ya Kaiseroda, Ujerumani, baada ya Ujerumani kusalimu amri mwaka wa 1945. Kwa kweli, majeshi ya Muungano yalichukua machimbo hayo majuma matatu kabla vita havijakoma.

J. S., Ujerumani

Asante kwa ueleweshaji huo. Machimbo ya Kaiseroda kwa kweli yalichukuliwa Aprili 4, 1945, zaidi ya mwezi mmoja kabla ya Ujerumani kusalimu amri Mei 8, 1945.—Mhariri.

Uchumba wa Mbali Ile makala “Vijana Huuliza . . . Naweza Kudumishaje Uchumba wa Mbali?” (Januari 22, 1999) ilinijia kwa kuchelewa sana. Natoka Marekani na nilianza kuandikiana na mwanamume mchanga kutoka Amerika ya Latini. Sijapata kamwe kuona jambo gumu kama hilo maishani. Kwa kweli huwezi kumjua mtu kupitia barua, hata uwe wafuatia haki kadiri gani. Kwa kuwa nyote wawili mko mbali, huelekea kuwazia-wazia tu. Kwa habari yetu, tamaduni zetu zilitofautiana. Uhusiano wetu ulipokwisha, nilikosa kusudi la kuishi. Kwa sababu ya familia yangu yenye upendo na yenye kutegemeza, nimestahimili jambo hilo.

S. H., Marekani

Nimekuwa nikimwandikia msichana mmoja niliyekutana naye kwenye mkusanyiko wa kimataifa wa Mashahidi wa Yehova. Ni vigumu kumweleza mtu mwingine mawazo yako wakati utamaduni na lugha zinapotofautiana. Kwa hiyo, nimeanza kujifunza lugha yake. Dokezo la kutumia ukanda uliorekodiwa ni zuri sana. Asanteni sana.

A. S., Ujerumani

Nilikutana na dada wa kutoka nchi za Mashariki kwenye mkusanyiko wa kimataifa katika Marekani. Nimekuwa nikitatanika jinsi ninavyoweza kuendelea kuwasiliana naye. Nilisali juu ya jambo hilo, na siku chache baada ya hapo, nikapokea makala hiyo yenye kupendeza. Nimeisoma tena na tena. Ilijibu maswali yangu yote.

G. R., Italia

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki