Mabingwa Wadogo Mno wa Kuruka Angani
SHSS! Mgwisho wazunguka hewani kwenye nzi aliye angani. Lakini nzi huyo akwepa mgwisho huo, ajirusha kwa muda mfupi katika mvurugo huo, ajisimamisha wima mwenyewe kisha, kwa kujirusha na kuanguka akiangalia juu kwenye dari, akudhihaki kwa kukosa ustadi wa kumwua. Kwa kweli hizo ni mbinu za kupuruka zinazostaajabisha! Kwa kweli, jamii ya nzi ambayo imeenea kila mahali ina wanasarakasi wengi zaidi wanaopuruka katika milki ya wadudu, kwa sehemu, ni kwa sababu ya sehemu mbili za mwili zilizobuniwa kwa njia ya kustaajabisha zinazoitwa haltere.
Kama tete mbili ndogo sana zenye vifundo kwenye ncha, haltere hizo mbili hujitokeza kwenye kidari cha nzi, nyuma tu ya mabawa yake. (Ona picha kwenye ukurasa ufuatao.) Mabawa ya nzi yanapoanza kupiga-piga, haltere nazo huanza kupiga-piga—kwa marudio yaleyale, mamia ya mara kila sekunde. Kwa kweli haltere ni kama magurudumu tuzi madogo ambayo husaidia mdudu huyo kupuruka. Hupeleka ujumbe kwenye ubongo wa nzi wakati wowote ule nzi ageuzapo mwelekeo, kwa mfano wakati mdudu huyo mdogo anapogongwa na dharuba ya upepo au na mvumo wa mgwisho au wa gazeti linalovurumishwa kwa ukaribu kwa njia hatari. Nzi hupashwa habari mara moja na haltere kwamba mwili wake umekwenda mrama, umebingirika, au kusukasuka kama vile gurudumu tuzi la ndege humweleza rubani mambo kama hayo, hata ingawa si kwa njia kamilifu kabisa. Nzi hurekebisha mwendo wake haraka na kwa urahisi.
Tofauti na magurudumu tuzi ya kawaida yanayozunguka, haltere hufanana na pinduli. Lakini hazining’inii au kusimama wima kuhusiana na nzi; hujitokeza kwenye upande. Zinapoanza mwendo, haltere, kama vile pinduli, huendelea kubembea, katika mwendo uleule kwa kupatana na sheria za mwendo. Kwa hiyo wakati mwili wa nzi unapojipinda akiwa angani, kani zilizo nje hupinda haltere zinazobembea kwenye sehemu yake ya chini, ambapo neva huhisi mpindo huo. Ubongo huchanganua ishara hizi za neva na kwa njia yake yenyewe huelekeza mabawa ya nzi upande wa kuume—zote kwa mwendo wa kasi sana.
Kwa kweli, haltere ni mojawapo ya viungo vya kipekee kwa nzi, jamii ya wadudu wenye mabawa mawili ya aina zipatazo 100,000 zinazotia ndani nzi wakubwa wasumbua farasi, nzi, blowflie (nzi wanaotaga mayai), nzi-tunda, mbung’o, usubi, na crane fly. Magurudumu tuzi yao ya hali ya juu huwapa nzi kiasi fulani cha uwezo wa kipekee wa angani ambao unashinda kwa mbali jamii yoyote ya wadudu wanaopuruka. Kwa kweli, mdudu huyu anayedharauliwa mara nyingi hutoa uthibitisho wa akili ya kisayansi ya hali ya juu sana ya Muumba.
[Picha katika ukurasa wa 24]
Kwenda mrama
[Picha katika ukurasa wa 24]
Kubingirika
[Picha katika ukurasa wa 24]
Kusukasuka
[Picha katika ukurasa wa 25]
“Soldier fly” (ameongezwa ukubwa), “haltere” zimeonyeshwa
[Hisani]
© Kjell B. Sandved/Visuals Unlimited
[Picha katika ukurasa wa 25]
Nzi
“Crane fly”
[Hisani]
Animals/Jim Harter/Dover Publications, Inc.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]
Century Dictionary