Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 11/22 kur. 26-27
  • Je, Nyumba Yako Ni Salama?—Mambo 20 ya Kuchunguza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Nyumba Yako Ni Salama?—Mambo 20 ya Kuchunguza
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Linda Mtoto Wako na Aksidenti
    Amkeni!—1999
  • Moto! Je, Utatumia Kizima-Moto Kipi?
    Amkeni!—2001
  • Jikoni Kwaweza Kuvutia
    Amkeni!—1997
  • Wazazi—Chagueni Vichezeo vya Mtoto Wenu kwa Hekima
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 11/22 kur. 26-27

Je, Nyumba Yako Ni Salama?—Mambo 20 ya Kuchunguza

“NYUMBANI, hatimaye!” Labda unashusha pumzi baada ya kurudi kutoka kwenye kazi inayochosha, ukifurahi kuwa salama nyumbani. Lakini je, uko salama kweli? Kwa kushangaza, watu fulani hukabili hatari kubwa ambazo huenda wasizitambue. Hasa wale walio na watoto wadogo wanapaswa kutahadhari ili kupunguza idadi ya aksidenti nyumbani. Kwa kutumia orodha ya ukaguzi inayofuata, kwa nini usichunguze nyumba yako na kuona mabadiliko yoyote yanayohitaji kufanywa?

✔ Mimea. Ikiwa una watoto wadogo, hakikisha kwamba hakuna mmea wowote ulio na sumu. Kumbuka, watoto wanaotambaa wenye udadisi wataingiza mdomoni mwao karibu kitu chochote.

✔ Mapazia. Weka mbali kamba za pazia. Zinaweza kutatanisha—na hata kuwanyonga—watoto wadogo.

✔ Saraka na kabati. Fikiria kuweka komeo za usalama. Komeo hizo zitazuia watoto wasishike vyombo vinavyoweza kukata na kemikali hatari za kusafishia.

✔ Ngazi. Je, zina nuru ya kutosha bila takataka? Je, umeweka malango ya usalama ili kuzuia watoto wanaotambaa wasianguke?

✔ Jiko. Weka mikono ya masufuria na vikaango ikielekea upande wa nyuma wa jiko, hasa unapopika.

✔ Kaango. Isafishe mara nyingi. Kaango iliyojaa mafuta inaweza kusababisha moto jikoni.

✔ Kizimamoto. Weka angalau kimoja nyumbani, na hakikisha kwamba kila mtu mwenye umri wa kuchukua mambo kwa uzito anajua namna ya kukitumia.

✔ Vitanda vya watoto. Vibao vyembamba vyapasa kukaribiana. Nafasi iliyo kandokando ya godoro haipasi kuwa kubwa kiasi cha kwamba kichwa cha mtoto chaweza kunaswa.

✔ Madirisha. Pao za usalama zitalinda watoto wasianguke na zaweza kuondolewa kwa urahisi na mtu mzima moto unapozuka.

✔ Vitamini na dawa. Ziweke katika kabati iliyofungwa mahali ambapo watoto hawawezi kuzifikia.

✔ Hodhi. Usiache kamwe mtoto mdogo akiwa peke yake kwenye hodhi. Mtoto anaweza kufa maji kwa muda mfupi, kunapokuwa na maji machache.

✔ Oveni za wimbi mikro. Kumbuka kwamba chakula hupata joto haraka zaidi kikiwa ndani ya wimbi mikro. Kwa mfano, mchanganyiko wa maziwa ya mtoto, unaweza kuunguza hata ingawa chupa yenyewe ina joto la kadiri.

✔ Tanuri. Hakikisha kwamba tanuri yako inakaguliwa pindi kwa pindi ili kuona kwamba haivuji kaboni monoksidi.

✔ Jiko la kuchomea nyama. Hakikisha kwamba watoto wako mahali salama mbali na jiko la kuchomea nyama linapokuwa moto.

✔ Mlango wa gereji. Waagize watoto wasikimbie kamwe chini ya mlango wa gereji unaposonga, hasa ikiwa unaendeshwa na umeme.

✔ Vifaa vya kugundua moshi. Visafishe daima, na kuvikagua kwa ukawaida. Badili betri zake kila mwaka.

✔ Nyaya za umeme na soketi. Tupa nyaya za umeme zilizochakaa. Ni bora ikiwa soketi zisizotumiwa zina vifuniko vya usalama au nyongeza.

✔ Vifaa vya umeme. Weka vifaa hivyo mbali na hodhi au sinki. Vifaa vinavyokata mzunguko wa umeme wa nyaya zilizo ardhini vyaweza kumzuia mtu asipigwe na stima.

✔ Masanduku ya vichezeo. Toboa shimo moja au mashimo zaidi kwenye sanduku la vichezeo na kuweka bawaba za kuzuia kifuniko kisianguke kwa ghafula.

✔ Pasi. Weka pasi yako—kutia ndani kamba yake inayoning’inia—mbali na watoto.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki