Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g01 1/8 uku. 31
  • Kutumia Vyema Vidio Yenye Uwezo Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutumia Vyema Vidio Yenye Uwezo Sana
  • Amkeni!—2001
  • Habari Zinazolingana
  • Alifanikiwa Kuliko Alivyotarajia
    Amkeni!—2003
  • Ninawezaje Kuwa na Uhusiano Mzuri na Mwalimu Wangu?
    Vijana Huuliza
  • Ninaweza Kufanya Nini ili Nielewane na Mwalimu Wangu?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
  • Walitimiza Ahadi Yao!
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2001
g01 1/8 uku. 31

Kutumia Vyema Vidio Yenye Uwezo Sana

ALIPOKUWA na umri wa miaka 12 tu, Tillie alitumia vyema fursa ya kutoa ushahidi shuleni. Darasa lao lilikuwa likisoma kuhusu Vita ya Ulimwengu ya Pili, na habari kuhusu yale Maangamizi Makuu ilizuka. Tillie alimwambia mwalimu wake kwamba mbali na Wayahudi, Mashahidi wa Yehova pia waliteswa na kuuawa katika enzi hiyo yenye kuogofya. Mwalimu alimruhusu Tillie aje na vidio ya Purple Triangles darasani. Kabla ya kuonyesha vidio hiyo, mwalimu huyo aliliambia darasa hivi: “Kwa sababu ya idadi kubwa ya Wayahudi waliouawa kwenye Maangamizi hayo Makuu, watu wengine wengi walionyanyaswa wamepuuzwa. Mashahidi wa Yehova wako miongoni mwa vikundi hivyo.”

Mwalimu huyo alivutiwa sana na vidio hiyo hata akamwazima mwalimu mwingine ili aitumie katika darasa lake. Tillie alikumbuka kwamba ndugu mkubwa wa mwalimu wake wa kidato cha nne alikuwa ameuawa na Wanazi kwenye Maangamizi hayo Makuu. Alimpelekea pia mwalimu huyo vidio hiyo, naye akaitazama jioni hiyohiyo.

Kwa ujumla, zaidi ya watu 60 waliitazama vidio ya Purple Triangles, na ilichochea upendezi mkubwa sana. Yote hayo yalitukia kwa sababu msichana mdogo alikuwa na ujasiri wa kueleza waziwazi kuhusu dini yake.—Zaburi 8:2.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki