Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g04 4/22 kur. 23-24
  • Je, Wanataka Tu Kujirembesha?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wanataka Tu Kujirembesha?
  • Amkeni!—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Manyoya—Ubuni wa Ajabu
    Amkeni!—2007
  • Walipataje Manyoya ya Kupendeza Jinsi Hiyo?
    Amkeni!—1991
  • Vitu vya Asili Vilitangulia vya Wanadamu
    Amkeni!—2010
  • Kuwatazama Ndege—Je, Kwavutia Kila Mtu?
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2004
g04 4/22 kur. 23-24

Je, Wanataka Tu Kujirembesha?

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI HISPANIA

JE, UMEWAHI kuona kwamba ndege hutumia muda mrefu kujisafisha? Wao hutumia saa nyingi kila siku wakiyachana-chana manyoya yao. Wawe ni kasuku, mwari, shorewanda, au flamingo, wote hufanya hivyo kila siku. Kwa nini? Je, wanataka tu kujirembesha?

Kuna sababu muhimu zaidi ya kufanya hivyo. Ndege wanahitaji vipindi hivyo vya kujisafisha kama vile eropleni inavyohitaji kurekebishwa. Kwa hakika kudumisha manyoya katika hali nzuri ni muhimu kwa maisha ya ndege. Manyoya yao huharibika sana, na kuyasafisha hakuyafanyi tu yawe safi na bila vimelea, bali pia huwasaidia wanaporuka.

Desturi hiyo ya kujisafisha kila siku hutia ndani kuunganisha ndaka za manyoya ya ndege ambazo zimeachana. Ndaka zinapounganishwa vizuri, manyoya humsaidia ndege kuruka. Kitabu Book of British Birds kinaeleza hivi: “Vikundi viwili vya manyoya vinahitaji kutunzwa zaidi, manyoya ya kuruka yaliyo kwenye mabawa na manyoya ya kuongoza yaliyo kwenye mkia.”

Ndege pia hupambana na vimelea. Mbali na kudhoofisha afya ya ndege, vimelea hao hula manyoya yake. Wataalamu wa maumbile wamegundua kwamba ndege wenye midomo iliyoharibika hawawezi kujisafisha vizuri, hivyo wanakuwa na vimelea wengi kwenye manyoya kuliko ndege wa kawaida. Ili kuondoa vimelea, aina fulani za ndege hujifunika kwa chungu ambao hutoa asidi inayoua vimelea.

Hatimaye manyoya yanahitaji kupakwa mafuta. Mafuta huwasaidia ndege wanaoishi karibu na maji kwa kuzuia maji yasipenye, nayo huwalinda ndege wote kutokana na hali ya hewa. Mafuta hayo yanatoka wapi? Tezi maalum iliyo juu ya mkia hutoa mafuta na nta, ambayo ndege hupaka kwenye manyoya yake. Manyoya ya kuruka hupakwa pia mafuta wakati huo.

Kwa hiyo hatupaswi kufikiria kwamba ndege anapoteza wakati anaposafisha manyoya yake. Ni kweli kwamba hilo humsaidia ndege kujirembesha, lakini linamsaidia pia awe na afya. Ndege wanahitaji kujisafisha ili waendelee kuishi.

[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 24]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Kikonyo

Ndaka

Vijindaka

Kiunganishi cha vijindaka

[Picha]

Kwa kujisafisha, ndege huunganisha sehemu ndogo za manyoya yao

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 23]

Cortesía del Zoo de la Casa de Campo, Madrid ▸

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

Pelican: Foto: Loro Parque, Puerto de la Cruz, Tenerife; parrot: Cortesía del Zoo de la Casa de Campo, Madrid

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki