Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g05 7/8 uku. 3
  • Kupoteza Kazi Ghafula!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kupoteza Kazi Ghafula!
  • Amkeni!—2005
  • Habari Zinazolingana
  • Kabla na Baada ya Kujifunza Biblia—Neno la Mungu Lina Matokeo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Pigo la Ukosefu wa Kazi ya Kuajiriwa
    Amkeni!—1996
  • Ukosefu wa Kazi ya Kuajiriwa?—Kwa Nini Upo?
    Amkeni!—1996
  • Endelea Kumtumikia Yehova kwa Shangwe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2005
g05 7/8 uku. 3

Kupoteza Kazi Ghafula!

“Nilifadhaika sana nilipopoteza kazi yangu. Jambo hilo lilifanya nihisi kuwa sifai kabisa.”—Tony, Ujerumani.

“Nilihisi kana kwamba nimewekelewa mzigo mzito kichwani. Nikiwa mzazi asiye na mwenzi, nilikuwa na wasiwasi kuhusu jinsi ambavyo ningewalisha watoto wangu wawili na kugharimia mahitaji yetu.”—Mary, India.

“Nilivunjika moyo sana nilipopoteza kazi yangu, na nilikuwa na wasiwasi sana ikiwa ningeweza kupata kazi nyingine.”—Jaime, Mexico.

ULIMWENGUNI pote, watu wengi wanakabiliana na tatizo lilelile kama Tony, Mary, na Jaime. Karibu mwanzo wa karne hii, ilikadiriwa kwamba asilimia 10 ya watu wanaoweza kufanya kazi huko Ulaya na Asia ya Kati, yaani, watu milioni 23 hivi, walikuwa wakitafuta kazi. Katika nchi fulani ambazo hazijaendelea sana kiviwanda, zaidi ya robo ya watu wanaoweza kufanya kazi, hawana kazi. Gazeti The New York Times la Julai 2003 lilisema kwamba nchini Marekani, “karibu watu milioni 2.6 wamepoteza kazi katika miezi 28 iliyopita.”

Katika nchi nyingi si rahisi kupata kazi. Kwa mfano, kila mwaka watu wengi waliohitimu shule za upili na vyuo hung’ang’ania nafasi za kazi zilizopo. Isitoshe, kuwa na digrii au kusomea kazi fulani hakumhakikishii mtu kwamba atapata kazi aliyosomea. Kwa hiyo, sasa ni jambo la kawaida watu kubadili kazi mara kadhaa maishani mwao. Hata wengine wanalazimika kufanya kazi tofauti kabisa na zile walizosomea.

Ukipoteza kazi, unaweza kufanya nini ili ufanikiwe kupata kazi nyingine? Na baada ya kuipata, unaweza kufanya nini ili uidumishe?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki