Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 5/06 kur. 2-3
  • Je, Unaweza Kuepuka Kuzeeka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Unaweza Kuepuka Kuzeeka?
  • Amkeni!—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Watu Wazee Wanaongezeka ulimwenguni
    Amkeni!—1999
  • Kwa Nini Sisi Huzeeka?
    Amkeni!—2006
  • Kutafuta-tafuta Maisha Marefu
    Amkeni!—1990
  • Kwa Nini Tunazeeka na Kufa?
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2006
g 5/06 kur. 2-3

Je, Unaweza Kuepuka Kuzeeka?

“Tuna miaka sabini tu—ikiwa tuna nguvu, themanini; . . . uhai unakoma upesi, nasi tunatoweka.”—ZABURI 90:10, TODAY’S ENGLISH VERSION.

HEBU wazia ukiishi katika upeo wa maisha daima. Wazia ukiwa na afya bora na akili chonjo wakati wote. Je, tarajio hilo zuri ni ndoto tu? Basi fikiria jambo hili lisilo la kawaida: Jamii fulani za kasuku wanaweza kuishi miaka mia moja hivi, hata hivyo, ni vigumu sana kwa panya kuishi kwa zaidi ya miaka mitatu. Tofauti hiyo kubwa ya muda ambao viumbe huishi imefanya wanabiolojia fulani wakate kauli kwamba kuzeeka husababishwa na jambo fulani, na kama ni hivyo, basi huenda kukawa na tiba.

Kampuni nyingi za kutengeneza dawa zimetumia pesa nyingi kutafuta tiba inayofaa ya kuzuia kuzeeka. Isitoshe, hangaiko kuu la watu waliozaliwa baada ya Vita vya Pili vya Ulimwengu ambao sasa wana miaka 60 na kitu, limekuwa kutafuta dawa ya kuzuia kuzeeka.

Pia utafiti kuhusu kuzeeka umekuwa jambo kuu kwa wataalamu wengi wanaochunguza chembe za urithi, molekuli, wanyama, na kuzeeka na athari zake. Kitabu Why We Age, cha Steven Austad, kinasema: “Siku hizi kunakuwa na msisimko mwingi wataalamu wanaochunguza kuzeeka na athari zake wanapokutana. Tunakaribia kuelewa sababu za msingi za kuzeeka na jinsi ambavyo uzee hutukia.”

Watu wana maoni mengi kuhusu visababishi vya kuzeeka. Watu fulani wana maoni ya kwamba kuzeeka husababishwa na kuchakaa kwa chembe; nao wengine wanaamini kwamba kumepangwa kimbele. Baadhi ya watu wanasema kwamba maoni yote mawili ni sawa. Hata hivyo, je, watu wanaelewa kabisa jinsi ambavyo uzee hutukia? Je, kuna sababu yoyote ya kutazamia tiba inayofaa ya kuzuia kuzeeka?

[Chati/Picha katika ukurasa wa 2, 3]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

APPROXIMATE LIFE SPANS

Nyuki

Siku 90

↓

Panya

Miaka 3

↓

Mbwa

Miaka 15

↓

Tumbili

Miaka 30

↓

Aligeta

Miaka 50

↓

Tembo

Miaka 70

↓

Mwanadamu

Miaka 80

↓

Kasuku

Miaka 100

↓

Kobe-jitu

Miaka 150

↓

Mti mkubwa unaoitwa sequoia

Miaka 3,000

↓

Msonobari aina ya bristlecone

Miaka 4,700

[Picha katika ukurasa wa 3]

Jamii fulani za kasuku wanaweza kuishi miaka 100, lakini wanadamu huishi miaka 80 hivi. Watafiti hujiuliza: “Ni nini husababisha kuzeeka?”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki