Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 3/08 uku. 26
  • Jicho Lenye Lenzi Nyingi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jicho Lenye Lenzi Nyingi
  • Amkeni!—2008
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Maana ya “Jicho kwa Jicho”?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Je, Jicho Lako Ni “Rahisi”?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Tumia Jicho kwa Hekima
    Amkeni!—2012
  • Maswali kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2008
g 3/08 uku. 26

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Jicho Lenye Lenzi Nyingi

◼ “Lina tabaka nyingi zilizo na mpangilio wa hali ya juu.” Hivyo ndivyo Profesa Luke Lee wa Chuo Kikuu cha California, Marekani alivyofafanua jicho lenye lenzi nyingi la wadudu wengi.

Fikiria hili: Wadudu fulani, kama vile nyuki wa asali na kereng’ende, wana jicho lenye lenzi nyingi na kila lenzi imeelekezwa upande tofauti. Picha zinazotokezwa na kila lenzi huwezesha jicho lote kuona eneo kubwa na hivyo kuwa na uwezo wa kutambua kitu chochote kinachosonga.

Wanasayansi wanatafuta njia za kuiga jicho hilo ili kutengeneza vifaa vya hali ya juu vya kutambua kitu chochote kinachosonga na kamera nyembamba sana zinazoweza kupiga picha upande wowote. Vifaa hivyo vinaweza kuwa na matumizi mengi. Huenda zikatumiwa katika matibabu, kwa mfano, zinaweza kutumiwa kuchunguza ndani ya tumbo. Kifaa hicho kinachotarajiwa kutumiwa katika matibabu kinasemwa kuwa “mfumo mdogo sana” hivi kwamba kinaweza kumezwa na mgonjwa. Kinapokuwa ndani ya tumbo, kifaa hicho kitakusanya habari kwa kutumia jicho lake lenye lenzi nyingi na kuziwasilisha.

Kikundi cha wataalamu fulani tayari kimebuni jicho lenye lenzi zaidi ya 8,500 lenye ukubwa wa kichwa cha pini. Hata hivyo, teknolojia hiyo ni duni sana inapolinganishwa na jicho lenye lenzi nyingi la wadudu. Kwa mfano, kereng’ende ana lenzi 30,000 hivi katika kila jicho!

Jiulize: ‘Je, jicho hilo la ajabu la wadudu lenye lenzi nyingi lilijitokeza lenyewe? Au lilibuniwa?’

[Picha katika ukurasa wa 26]

Sehemu fulani ya jicho la nyuki wa asali lililoongezwa ukubwa

[Picha katika ukurasa wa 26]

Background: © Stephen Dalton/Photo Researchers, Inc.; close-up: © Raul Gonzalez Perez/Photo Researchers, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki