Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 11/08 uku. 10
  • Mfumo Unaoongoza Safari ya Kipepeo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mfumo Unaoongoza Safari ya Kipepeo
  • Amkeni!—2008
  • Habari Zinazolingana
  • Safari ya Kipepeo Anayeitwa “Monarch”
    Je, Ni Kazi ya Ubuni?
  • Siku Moja Katika Maisha ya Kipepeo
    Amkeni!—1993
  • Msafiri Dhaifu Lakini Hodari
    Amkeni!—1996
  • Vipepeo Wazuri Hawa Ni Wenye Sumu?
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2008
g 11/08 uku. 10

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Mfumo Unaoongoza Safari ya Kipepeo

◼ Akitumia ubongo unaotoshana na ncha ya kalamu, kipepeo anayeitwa monarch anasafiri kilomita 3,000 hivi kutoka Kanada hadi kwenye msitu mdogo nchini Mexico. Mdudu huyo anajuaje njia atakayopitia?

Fikiria hili: Kipepeo huyo hutambua mahali anakoelekea kwa kutegemea mahali jua lipo. Lakini si hilo tu. Wadudu hao pia hutumia utaratibu sahihi sana wa kibiolojia wa saa 24 ili kujipatanisha na mwendo wa jua. Dakt. Steven Reppert, mtaalamu wa mfumo wa neva, anasema kwamba vipepeo hao “wana utaratibu tofauti wa kutambua wakati wakilinganishwa na wadudu na wanyama wengine ambao wamechunguzwa kufikia sasa.”

Kujifunza mengi zaidi kuhusu jinsi kipepeo anayeitwa monarch anavyotambua wakati, kunaweza kuwasaidia wanasayansi kuelewa jinsi wanadamu na wanyama wanavyotambua wakati kiasili. Pia kunaweza kuchochea kuanzishwa kwa matibabu mapya ya magonjwa ya mfumo wa neva. “Ninataka kuelewa jinsi ubongo unavyopokea na kutumia habari kuhusu wakati na mwelekeo,” anasema Reppert, “na kipepeo anayeitwa monarch anaweza kunisaidia sana kutimiza lengo hilo.”

Una maoni gani? Je, mfumo wa kipepeo unaomwongoza anaposafiri ulijitokeza wenyewe? Au unathibitisha kwamba kuna Mbuni mwenye akili?

[Mchoro/Ramani katika ukurasa wa 10]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa

Kipepeo anayeitwa “monarch” anasafiri kilomita 3,000 hivi kutoka Kanada hadi kwenye msitu mdogo nchini Mexico

[Ramani]

KANADA

MAREKANI

MEXICO

MEXICO CITY

[Picha katika ukurasa wa 10 zimeandilwa na]

Background: © Fritz Poelking/age fotostock

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki