Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/09 uku. 27
  • Jani Lisilolowa Maji la Yungiyungi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jani Lisilolowa Maji la Yungiyungi
  • Amkeni!—2009
  • Habari Zinazolingana
  • Kuna Jani Katika Utando wa Buibui!
    Amkeni!—2002
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2009
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2001
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2009
g 4/09 uku. 27

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Jani Lisilolowa Maji la Yungiyungi

◼ Eti vikombe vya plastiki vinavyojisafisha vyenyewe, madirisha yasiyopata maji wakati wa mvua, mashini ndogo sana zinazofanya kazi bila kusuguana? Wanasayansi wanasema kwamba hizo ni baadhi tu ya faida tunazoweza kupata kwa kutumia muundo wa jani la yungiyungi.

Fikiria hili: Sehemu ya juu ya jani la yungiyungi lina mabonge madogo sana ambayo yamefunikwa kwa fuwele zenye nta. Matone ya maji yanapoanguka juu ya majani hayo yanakwama kwenye mirija hiyo ambayo huzuia jani lisilowe maji. Mwinamo wa jani hufanya maji yamwagike hata kabla hayajagusa sehemu ya juu ya jani. Matokeo ni nini? Jani la yungiyungi halilowi maji na pia linadumu likiwa safi kwa kuwa uchafu na vumbi husafishwa na maji hayo.

Wanasayansi wanataka kubuni vitambaa ambavyo havilowi maji kamwe kwa kuiga jani la yungiyungi. Hata mashini ndogo sana, ambazo zinaweza kuharibiwa na maji zitafaidika na muundo huo wa jani la yungiyungi. “Kuna njia nyingi sana za kutumia [muundo wa jani hilo],” linaripoti gazeti Science Daily.

Una maoni gani? Je, jani la yungiyungi lilijitokeza lenyewe? Au lilibuniwa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki