Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 10/14 kur. 12-13
  • Watunza-Bustani Wanaoruka Katika Misitu ya Mvua

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Watunza-Bustani Wanaoruka Katika Misitu ya Mvua
  • Amkeni!—2014
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kusambaza Mbegu
  • Maisha ya Familia
  • Uwezo wa Popo Kutambua Vitu Vilipo kwa Kutumia Mwangwi
    Je, Ni Kazi ya Ubuni?
  • Popo Mdogo Zaidi Ulimwenguni
    Amkeni!—2010
  • Mabawa ya Viumbe Wanaoruka
    Amkeni!—2009
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2010
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2014
g 10/14 kur. 12-13
Popo akila matunda mtini

Watunza-Bustani Wanaoruka Katika Misitu ya Mvua

KAMA watunza-bustani wanavyojua, ili mbegu iote vizuri inahitaji kupandwa mahali panapofaa na wakati unaofaa. Hata hivyo, inashangaza kwamba mbegu hupandwa kwa wingi sana na viumbe wanaoruka usiku katika misitu ya mvua. Watunza-bustani hao ambao hupanda mbegu ni popo aina ya Old World, na baadhi yao huitwa mbweha wanaoruka.a

Kusambaza Mbegu

Popo mla matunda

JE, WAJUA? Tofauti na popo wengine, popo wanaokula matunda hawategemei mawimbi ya sauti ili kutafuta chakula, badala yake wao hutumia uwezo wa kuona na kunusa. Macho yao makubwa huwasaidia kuona usiku

Popo wengi wanaokula matunda huruka usiku kwenye miti ili kutafuta matunda na nekta ya maua. Wakiwa angani, popo hao hula matunda na kuangusha kinyesi chenye mbegu na maganda. Pia, kazi yao ya kutunza bustani inahusisha kuchavusha maua wanapotafuta nekta wanayopenda sana.

Kwa kuwa popo hao husafiri mwendo mrefu usiku, wanaweza kusambaza mbegu kwenye eneo kubwa sana. Na kwa kuwa mbegu fulani hupatikana katika kinyesi chao, wanatokeza “mbolea” inayosaidia mbegu kukua. Haishangazi kwamba mimea mingi katika misitu ya mvua hutegemea popo ili kuchavusha maua au kusambaza mbegu.

Kwa kuwa wanasafiri mbali, popo wanaokula matunda wanahitaji ustadi wa kusafiri na uwezo wa kuona vizuri. Gizani popo hao wanaweza kuona vizuri kuliko wanadamu. Hata wanaweza kutofautisha rangi. Na wanaweza kusafiri mchana na pia usiku.

Maisha ya Familia

Popo aina ya Samoan flying fox (Pteropus samoensis) huwa na mwenzi mmoja maisha yote. Katika jamii fulani, popo wa kike humtunza vizuri sana mtoto wake, akimbeba kwa majuma kadhaa na kumnyonyesha mpaka anapokomaa. Aina fulani ya popo wa kike hutafuta huduma za “mzalishaji” wakati wa kujifungua.

Kwa kusikitisha, idadi ya popo wanaokula matunda inapungua kwa kasi sana hasa kwa sababu ya kukatwa kwa misitu. Katika visiwa vya Pasifiki Kusini, kutoweka kwa popo hao kutaleta matatizo makubwa kwa kuwa mimea fulani katika visiwa hivyo hutegemea popo ili kuchavusha maua. Kwa kweli, kazi ya watunza-bustani hao wanaoruka inapaswa kuthaminiwa sana.

a Popo aina ya Old World wanaokula matunda hupatikana Afrika, Asia, Australia, na Visiwa fulani vya Pasifiki.

KULINDA MISITU

Mbuyu

Mbuyu huchipusha maua ambayo hudumu kwa muda wa saa 24 tu! Lakini muda huo unatosha kwa popo wanaokula matunda kupata maua hayo makubwa yaliyojaa nekta na kusaidia miti ya mbuyu kuchavusha

Miti inapokatwa katika misitu ya mvua, popo husaidia sana kupanda miti katika eneo lililokatwa. Kazi yao ya ‘kutunza bustani’ husaidia kutokeza miti mipya. “Ili wafurahie maisha, wanadamu wanahitaji mazingira bora ulimwenguni, na popo wanahitajika ili kudumisha mazingira hayo,” kinasema kitabu Bats of the World, cha Gary L. Graham.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki