Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwwd makala 16
  • Uwezo wa Popo Kutambua Vitu Vilipo kwa Kutumia Mwangwi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uwezo wa Popo Kutambua Vitu Vilipo kwa Kutumia Mwangwi
  • Je, Ni Kazi ya Ubuni?
  • Habari Zinazolingana
  • Watunza-Bustani Wanaoruka Katika Misitu ya Mvua
    Amkeni!—2014
  • Popo Mdogo Zaidi Ulimwenguni
    Amkeni!—2010
  • Viumbe Wana Hisi za Ajabu
    Amkeni!—2003
  • Mabawa ya Viumbe Wanaoruka
    Amkeni!—2009
Pata Habari Zaidi
Je, Ni Kazi ya Ubuni?
ijwwd makala 16
Popo akiingia ndani ya pango.

JE, NI KAZI YA UBUNI?

Uwezo wa Popo Kutambua Vitu Vilipo kwa Kutumia Mwangwi

Ingawa wana uwezo wa kuona, aina nyingi za popo hutumia mwangwi kutambua mazingira yao wanaporuka usiku. Hilo linamaanisha kwamba wanatambua umbali wa kitu kwa kutegemea muda ambao sauti itawarudia. Kwa mfano, popo fulani wanaweza kutofautisha kati ya mbu na mbawakawa kwa kusikiliza mapigo ya mabawa ya wadudu hao.

Fikiria hili: Popo wengi hutokeza sauti katika zoloto na kuzitoa kupitia mdomo au pua zao. Kisha wanatumia masikio yao makubwa kutambua mwangwi wowote unaotokea baada ya mawimbi ya sauti kugonga kitu fulani. Mwangwi huo humwezesha popo kupiga picha akilini ya mazingira yake yote. Popo anaweza kutambua mahali, mwinuko, na umbali wa kitu, hata ikiwa kuna kelele nyingi zinazotokezwa na popo wengine.

Popo anahitaji kuwa sahihi kabisa anapotambua vitu vilipo kwa sababu kukosea hata kwa chini ya nusu sekunde kunaweza kumfanya akose shabaha yake kwa sentimita 17. Kulingana watafiti fulani, kulenga shabaha kwa usahihi kabisa wa chini ya nusu sekunde “ni jambo linaloonekana kuwa haliwezekani.” Hata hivyo, majaribio yaliyofanywa yanaonyesha kwamba popo wana uwezo wa kutoa mwangwi kwa usahihi kabisa wa muda wa mara 100,000,000 ya sekunde (10 nanoseconds) jambo linalowawezesha kukadiria umbali kwa usahihi wa milimita moja au hata chini ya hapo!

Watafiti wametengeneza fimbo ya umeme inayotumia mwangwi kutambua vitu vilipo ili kuwasaidia vipofu kupata picha akilini ya mazingira yao na kuwawezesha kuepuka vikwazo, kutia ndani vile ambavyo viko juu kama tawi la mti. Brian Hoyle na Dean Waters, ambao ni wawili kati ya wataalamu waliobuni fimbo hiyo ya umeme inayoitwa Batcane, wanasema hivi: “Tulichochewa kuitengeneza hasa baada ya kutambua uwezo wenye kustaajabisha wa popo kutambua vitu vilipo kwa kutumia mwangwi.”

Mwanamume kipofu akitembea huku akitumia fimbo ya umeme. Fimbo hiyo iliyo na uwezo wa kutambua vitu vilipo kwa kutumia mwangwi, inampa taarifa kwamba mbele yake kuna bomba la maji.

Una maoni gani? Je, uwezo wenye kustaajabisha wa popo kutambua vitu vilipo kwa kutumia mwangwi ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki