Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 6/15 kur. 14-15
  • Samaki Aina ya Pono–Mashine ya Kutengeneza Mchanga

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Samaki Aina ya Pono–Mashine ya Kutengeneza Mchanga
  • Amkeni!—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Unapokuwa Mgonjwa kwa Kula Samaki
    Amkeni!—2006
  • Matumbawe—Yamo Hatarini na Yanakufa
    Amkeni!—1996
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2015
  • Maajabu ya Bahari Nyekundu Chini ya Mawimbi
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2015
g 6/15 kur. 14-15
Samaki aina ya pono

Samaki Aina ya Pono​— Mashine ya Kutengeneza Mchanga

Mchanga hutoka wapi? Kuna vyanzo vingi mbalimbali. Lakini huenda ukashangazwa na moja ya chanzo kinachoelezwa katika makala hii. Ni samaki anayesaga tumbawe na kuwa mchanga laini—samaki aina ya pono!

Pono (parrot fish) wanaishi katika maji ya kitropiki ulimwenguni pote. Baada ya kumeza kipande cha tumbawe, wanatafuta chembechembe za chakula na kutema mabaki, ambayo ni mchanga. Ili kufanya kazi yake, samaki huyo anatumia taya za midomo yake imara na meno yake magumu. Baadhi jamii za samaki hao wanaweza kuishi miaka 20 bila meno yake kupukutika.

Katika maeneo yenye matumbawe yaliyokufa, samaki huyo hutafuna kwa urahisi na kutokeza mchanga kwa wingi kuliko chanzo kingine chochote cha asili. Watafiti fulani wanakadiria kwamba samaki huyo huzalisha mamia ya kilogramu za mchanga kwa mwaka.

Samaki aina ya pono

Pono mweusi

Pono hufanya kazi nyingine muhimu. Anapokula matumbawe yaliyokufa, miani iliyo kwenye tumbawe na majani, jambo hilo hudumisha usafi wa tumbawe. Tumbawe ni chakula muhimu kwa pono, na hii ndiyo sababu huyatunza matumbawe. Sehemu ambazo hakuna pono na viumbe wengine wanaofanya hivyo, matumbawe huharibiwa na miani na magugu-maji. “Wengine hudai kwamba matumbawe yaliyopo sasa yasingekuwa katika hali hiyo ikiwa kusingekuwa na viumbe kama hao,” kinaeleza kitabu Reef Life.

Kutokana na shughuli zote hizo za mchana, pono wanahitaji kupumzika vizuri wakati wa usiku, pindi hiyo pono hufanya jambo lisilo la kawaida. Wakati wa usiku ni hatari kuwa katika matumbawe, kwa sababu kuna viumbe wengi wanaowinda. Kwa kawaida pono hulala mafichoni chini ya mwamba, lakini sehemu hiyo iliyofichika haiwezi kuwalinda wakati wote kutokana na papa mwenye njaa.

Ili kuwa salama zaidi, baadhi ya samaki hao hujifunika wakati wa usiku. Wao hutoa ute wenye utelezi ambao hufunika kabisa miili yao, na kuwa kama gauni jangavu la usiku. Wanasayansi wa viumbe vya majini wanaamini kwamba harufu mbaya inayotoka kwenye ute huo huwalinda kutoka kwa viumbe wanaowawinda.

Pono ni miongoni mwa samaki wanaovutia na wale wanaoonekana kwa urahisi kwenye matumbawe. Mara nyingi pono jike na dume huwa na rangi zinazong’aa, ambazo hubadilika kwa kadiri wanavyoendelea kukua. Lakini jambo zuri hata zaidi ni kwamba pono hupatikana kwa wingi katika maeneo ambayo hawavuliwi kupita kiasi. Hivyo, ni samaki wanaoonekana kwa urahisi.

Unapomtazama kwa karibu pono na kumsikiliza anapotafuna juu ya tumbawe, ni baadhi ya mambo ambayo watafiti wa miamba ya matumbawe hawawezi kusahau. Pia, pono wanapofanya kazi yao, huboresha mazingira kwa viumbe wengine katika matumbawe na ili kufurahisha wanadamu.

UKWELI KUHUSU SAMAKI ANAYEITWA PONO

Pono, samaki (anayejulikana na wanasayansi kwa jina la Scaridae) ni jamii kubwa yenye aina mbalimbali 80 ambazo hupatikana kwenye miamba ya matumbawe katika maeneo ya Kitropiki. Mdomo wa samaki huyo unafanana na mdomo wa kasuku. Pono ana urefu kati ya sentimeta 50 hadi 100.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki