Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/15 kur. 14-15
  • Unayopaswa Kujua Kuhusu Malaria

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unayopaswa Kujua Kuhusu Malaria
  • Amkeni!—2015
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • 1 MALARIA NI NINI?
  • 2 MALARIA HUENEZWAJE?
  • 3 UNAWEZA KUJIKINGA JINSI GANI?
  • Kifo Katika Mabawa Mepesi
    Amkeni!—1993
  • Kuyarudia Mambo ya Msingi Katika Kupigana na MALARIA
    Amkeni!—1997
  • Silaha Mpya Dhidi ya Malaria
    Amkeni!—1993
  • Kwa Nini Maradhi “Yanayoponyeka” Yamerudi?
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2015
g 7/15 kur. 14-15

Unayopaswa Kujua Kuhusu Malaria

Shirika la Afya Ulimwenguni linakadiria kwamba katika mwaka wa 2013, zaidi ya watu milioni 198, waliambukizwa malaria na imekadiriwa kuwa watu 584,000 walikufa kutokana na ugonjwa huo. Karibu watu 4 kati ya 5 waliokufa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Ugonjwa huo unatishia mamia ya nchi na maeneo mbalimbali ulimwenguni, na watu bilioni 3.2 wanakabili hatari ya kuambukizwa.

1 MALARIA NI NINI?

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea. Dalili zake hutia ndani homa, kuhisi baridi, kutokwa na jasho, maumivu ya kichwa na mwili, kichefuchefu, na kutapika. Dalili hizo zinaweza kuonekana baada ya saa 48 hadi 72, ikitegemea aina ya vimelea na muda ambao mtu amekuwa na ugonjwa.

2 MALARIA HUENEZWAJE?

  1. Mchoro unaoonyesha jinsi vimelea vya malaria vinavyosambaa katika mwili wa binadamu

    Vimelea vya malaria vinavyoitwa Plasmodia, hungia katika mfumo wa damu kupitia kuumwa na mbu jike aitwaye Anopheles..

  2. Vimelea hivyo huenda katika chembe za ini la mtu aliyeambukizwa, na huko vimelea huzaliana..

  3. Wakati chembe za ini zinapopasuka, huruhusu vimelea, ambavyo hushambulia chembe nyekundu za damu ya mtu aliyeambukizwa. Huko, vimelea hivyo huzidi kuongezeka..

  4. Vimelea vya Malaria hushambulia chembe nyekundu za damu na kufanya zipasuke

    Wakati chembe nyekundu za damu zinapopasuka, huruhusu vimelea, ambavyo hushambulia kwa wingi zaidi chembe nyekundu za damu..

  5. Mzunguko wa chembe nyekundu za damu unapovamiwa na mipasuko hiyo huendelea. Kisha mtu aliyeambukizwa huanza kuonyesha wazi dalili za malaria kila baada ya chembe nyekundu ya damu kupasuka.

3 UNAWEZA KUJIKINGA JINSI GANI?

Ikiwa unaishi katika nchi ambazo malaria imeenea . . .

  • Tumia chandarua. Chandarua hicho kinapaswa

    • kuwekwa dawa ya kuua mbu.

    • kisiwe na shimo au tundu.

    • kuchomekwa vizuri kwenye godoro.

  • Puliza dawa ya kuua wadudu nyumbani mwako.

  • Ikiwezekana, weka wavu wa kuzuia wadudu katika madirisha na milango, na utumie kiyoyozi na feni ili kufukuza mbu.

  • Vaa nguo zenye rangi nyangavu na zinazofunika mwili vizuri.

  • Inapowezekana, epuka kuwa katika maeneo yenye mbu wengi, mabwawa yenye mbu, na maji yaliyotuama, mahali ambapo mbu huzaliana.

  • Ikiwa umeanza kuugua tafuta matibabu haraka.

Mzunguko wa Malaria unaohusisha mbu na wanadamu

Mtu anaweza kupata vimelea vya malaria kutoka kwa mbu mwenye vimelea hivyo. Kwa upande mwingine, mbu asiye na vimelea, anaweza kuvipata anapomuuma mtu aliyeambukizwa. Kisha, mbu huyo anaweza kupitisha vimelea vya malaria kwa mtu mwingine

Ikiwa unapanga kutembelea nchi ambayo malaria imeenea . . .

  • Kabla ya kusafiri, pata habari za karibuni kuhusu ugonjwa huo. Kwani aina ya vimelea vya malaria wa eneo moja huenda vikatofautiana na vya eneo jingine, jambo hilo litakusaidia kuamua aina ya dawa inayofaa zaidi. Pia, litakuwa jambo la hekima kuwasiliana na daktari wako ili kujua mambo unayopaswa kuepuka kwa kuzingatia hali ya afya yako.

  • Unapokuwa katika nchi hiyo, fuata maelekezo yaliyo katika makala hii kwa ajili ya watu wanaoishi katika nchi zenye ugonjwa wa malaria.

  • Ikiwa umeambukizwa, tafuta matibabu haraka. Kumbuka kwamba huenda dalili hizo zikaonekana kati ya juma moja hadi majuma manne baada ya kuambukizwa.

MAMBO MENGINE UNAYOWEZA KUFANYA

  1. Faidika na programu za huduma zinazotolewa na serikali au mashirika ya afya.

  2. Tumia dawa zilizothibitishwa na mamlaka. (Kutumia dawa zisizofaa au dawa bandia kunaweza kuzidisha ugonjwa na kuhatarisha uhai.)

  3. Ondoa vitu vyovyote vinavyoweza kuchangia mbu kuzaliana kuzunguka nyumba.

Ikiwa unaishi katika eneo lenye ugonjwa wa malaria au umewahi kutembelea eneo lenye ugonjwa huo, usipuuze dalili zifuatazo za malaria . . .

  • Kuhisi joto kali (homa)

  • Kutokwa jasho jingi

  • Kutetemeka kwa mwili

  • Maumivu ya kichwa

  • Maumivu ya misuli

  • Uchovu

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Kuharisha

Ugonjwa wa malaria usipotibiwa unaweza kusababisha upungufu wa chembe za damu na hivyo kuhatarisha uhai. Kabla ya dalili hizo kuwa mbaya hata zaidi, tafuta matibabu haraka, hasa inapohusu watoto na akina mama wajawazito.a

a Kwa habari zaidi, ona gazeti la Amkeni! la Novemba 2011, ukurasa wa 24-25, na Novemba 2009, ukurasa wa 26-29.

JE WAJUA?

Saa ya mfano iliyo katika ramani ya bara la Afrika

Barani Afrika pekee, mtoto mmoja hufa kila dakika kutokana na malaria

  • Watoto na wanawake wajawazito wako katika hatari kubwa zaidi iwapo watapata malaria.

  • Barani Afrika pekee, mtoto mmoja hufa kila dakika kutokana na malaria.

  • Katika visa vichache, watu fulani wameambukizwa malaria kupitia kuongezwa damu mishipani.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki