Silaha Mpya Dhidi ya Malaria
KAMA ilivyoripotiwa katika Amkeni! la Mei 8, 1993, malaria inarudi ikiwa pigo la ulimwenguni pote. Gazeti The New York Times (Machi 23, 1993) liliripoti kwamba “mwaka uliopita, Brazili ilirekodi visa 560,000 vya malaria.” Wabrazili 8,000 hufa kutokana na malaria kila mwaka. Sasa mtafiti wa Kolombia, Dakt. Manuel Elkin Patarroyo, amepata njia tofauti—dawa ya chanjo iliyotengenezwa kikemikali yenye kugharimu senti 30 tu za U.S. inayotumiwa mara tatu. “Ni bei rahisi kuliko Coca-Cola [katika Kolombia],” akasema Dakt. Patarroyo. Kufikia sasa imethibitika kuwa yenye matokeo kwa asimilia 67 ya matibabu yaliyotolewa. Ingawa hiyo si jibu kamili kwa malaria iliyo hatari, inaonekana kuwa hatua kubwa katika vita dhidi ya malaria.