Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 8/15 uku. 16
  • Mfumo wa Gia wa Panzi Anayeitwa Issus

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mfumo wa Gia wa Panzi Anayeitwa Issus
  • Amkeni!—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2015
  • Fumbo Kubwa la Kisayansi Lafumbuliwa
    Amkeni!—2009
  • Uwe Mwasiliani!
    Huduma Yetu ya Ufalme—2002
  • Mguu wa Farasi
    Amkeni!—2014
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2015
g 8/15 uku. 16
Panzi anayeitwa Issus

JE, NI KAZI YA UBUNI?

Mfumo wa Gia wa Panzi Anayeitwa Issus

Picha ya mfumo wa gia wa panzi anayeitwa Issus ulio kwenye miguu yake ya nyuma

KWA MUDA mrefu, imedhaniwa kwamba wanadamu ndio waliogundua mfumo wa gia. Hata hivyo, mawazo hayo yamethibitishwa kuwa si ya kweli! Hivi karibuni, mfumo wa gia zinazofanya kazi kwa pamoja umegunduliwa katika mdudu mchanga anayeitwa Issus, anayepatikana katika bustani nyingi barani Ulaya.a

Panzi huyo anapokuwa mchanga anaweza kuruka kwa mwendo kasi wa mita 3.9 kwa sekunde chache tu, na kujirusha karibu mara 200 zaidi ya nguvu za uvutano! Anaweza kutoroka kwenye upeo wa macho ukipepesa jicho tu. Ili aweze kuruka, miguu miwili ya nyuma ya mdudu huyo inahitaji kutokeza msukumo uleule sahihi na kwa wakati mmoja. Ni nini siri ya usahihi huo?

Fikiria hili: Wanasayansi wamegundua mifumo miwili ya gia zinazoungana chini ya miguu ya nyuma ya kiumbe huyo. Panzi huyo anaporuka, gia hizo husaidia miguu yake miwili ifanye kazi kwa usahihi na upatano. Isingekuwa hivyo, asingeweza kuruka kwa njia nzuri!

Viumbe wakubwa wanaporuka hutegemea mfumo wa neva kupatanisha miguu yao. Lakini, kwa panzi huyo, msukumo huo wa neva ungekuwa na kasi ndogo sana. Hivyo ndio sababu mdudu huyo ana mfumo wa gia. “Kwa kawaida sisi tunafikiria gia kuwa kitu fulani tunachokiona katika mashine ambazo mwanadamu ameunda,” alisema mtunzi na mtafiti Gregory Sutton. Kisha akaongezea sababu kwa kusema hivi: “Hatukuwa tumechunguza [kila mahali] kwa ukamili.”

Una maoni gani? Je, mfumo wa gia wa panzi anayeitwa Issus ulitokana na mageuzi? Au ulibuniwa?

a Gia hizo huacha kufanya kazi anapokomaa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki