Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g16 Na. 3 uku. 3
  • Kushinda Kizuizi cha Tangu Zamani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kushinda Kizuizi cha Tangu Zamani
  • Amkeni!—2016
  • Habari Zinazolingana
  • Utangulizi
    Amkeni!—2016
  • Habari Njema Katika Lugha 500
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Kitabu “Kisemacho” Lugha Zilizo Hai
    Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
  • Lugha ya Watu Wote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2016
g16 Na. 3 uku. 3
Watu wa jamii na tamaduni mbalimbali

HABARI KUU | KUSHINDA KIZUIZI CHA LUGHA

Kushinda Kizuizi cha Tangu Zamani

LEO kuna lugha nyingi tofauti-tofauti duniani, karibu lugha 7,000 hivi. Hilo hutokeza changamoto katika nyanja ya usafiri, biashara, na serikali. Hali imekuwa hivyo tangu zamani. Kwa mfano, miaka 2,500 hivi iliyopita, katika utawala wa Mfalme Ahasuero (huenda ni Shasta wa I), Waajemi walituma ujumbe katika milki yote, “kutoka India mpaka Ethiopia, wilaya za utawala 127, kila wilaya ya utawala kwa mtindo wao wa kuandika na kila kikundi cha watu kwa lugha yao.”a

Leo, mashirika au hata serikali nyingi zimeshindwa kufanya jambo gumu kama hilo. Lakini kuna shirika moja ambalo limefaulu kufanya kazi hiyo kwa ustadi. Mashahidi wa Yehova huchapisha magazeti, rekodi za kusikiliza, video, na vitabu vingi kutia ndani Biblia katika lugha zaidi ya 750. Hilo linatia ndani lugha za ishara [alama] 80. Pia, Mashahidi wanatafsiri machapisho mbalimbali katika Maandishi ya vipofu.

Zaidi ya yote, Mashahidi wa Yehova hawapati faida ya kiuchumi kwa sababu ya jitihada zao. Kwa kweli, watafsiri na wafanyakazi wengine hufanya kazi kwa kujitolea. Kwa nini wanafanya kazi ngumu ya kutafsiri lugha nyingi, nao hufanya kazi hiyo jinsi gani?

a Soma Esta 8:9 katika Biblia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki