Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g19 Na. 1 uku. 3
  • Mambo Yanayohatarisha Usalama Duniani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mambo Yanayohatarisha Usalama Duniani
  • Amkeni!—2019
  • Habari Zinazolingana
  • Miamba ya Matumbawe Inayokufa—Je, Wanadamu Wanahusika?
    Amkeni!—1996
  • Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Matatizo ya Kiuchumi?
    Habari Zaidi
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2007
  • Ni Nini Kiwezacho Kufanywa ili Kuokoa Miamba ya Matumbawe?
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2019
g19 Na. 1 uku. 3

TATIZO

Mambo Yanayohatarisha Usalama Duniani

“Kizazi hiki ndicho kilichoendelea zaidi kiteknolojia, kisayansi, na kiuchumi . . . Hata hivyo, inaonekana kizazi hikihiki ndicho ambacho huenda kitaporomosha kabisa mifumo [ya siasa, uchumi, na mazingira].”​—The Global Risks Report 2018, World Economic Forum.

KWA NINI WATU WENGI WANAHANGAISHWA NA HALI YETU YA WAKATI UJAO NA JINSI DUNIA ITAKAVYOKUWA? ACHENI TUCHUNGUZE BAADHI YA CHANGAMOTO TUNAZOKABILI.

  • Kompyuta iliyofungwa

    UHALIFU WA MTANDAONI: “Kila siku inazidi kuwa hatari kutembelea vituo vya intaneti. Intaneti imekuwa uwanja wa watu walio na tamaa ya kufanya ngono na watoto, watu wakorofi, watu wanaochochea mabishano, na wezi wa taarifa mtandaoni.” Kutumia jina, namba ya siri, au namba ya kadi ya mtu mwingine bila ridhaa yake ili kujinufaisha, “ni aina ya uhalifu inayokua kwa kasi zaidi ulimwenguni. . . . Vilevile, kwenye intaneti watu hupata fursa ya kuonyesha roho ya kikatili, moja ya sifa mbaya zaidi za wanadamu.”—Gazeti The Australian.

  • Mikono inayotaka kuchukua pesa

    PENGO KATI YA MATAJIRI NA MASKINI: Ripoti ya karibuni ya shirika la Oxfam inaonyesha kwamba, mali zinazomilikiwa na watu nane walio matajiri zaidi duniani ni sawa na mali za watu bilioni 3.6 walio maskini zaidi. Kulingana na shirika hilo, “uchumi wetu unaelekeza mali kwa matajiri wakubwa kwa njia inayowadidimiza watu maskini zaidi katika jamii, wengi wao wakiwa ni wanawake.” Baadhi ya watu wanahofu kwamba huenda pengo hilo linalozidi kuongezeka litasababisha machafuko katika jamii.

  • Mabomu

    VURUGU NA UNYANYASAJI: Ripoti ya 2018 ya Tume ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Wakimbizi inasema: “Hatujawahi kushuhudia idadi kubwa ya watu wanaokimbia eneo moja kwenda lingine kama tunayoona sasa.” Zaidi ya watu milioni 68 wamelazimika kukimbia makazi yao, hasa kwa sababu ya vurugu au unyanyasaji. Ripoti hiyo inaendelea kusema: “Inakadiriwa kwamba kila baada ya sekunde mbili, mtu mmoja hulazimika kuhama.”

  • Hewa chafu inatoka kupitia bomba la kutolea moshi

    KUHARIBIWA KWA MAZINGIRA: Ripoti moja ya mwaka wa 2018, inasema kwamba “wanyama na mimea wanatoweka kwa kiwango kikubwa sana, . . . na uchafuzi wa hewa na bahari unazidi kuhatarisha afya ya wanadamu.” Pia, idadi ya wadudu inazidi kuporomoka katika baadhi ya nchi. Kwa sababu wadudu huchavusha mimea, wanasayansi wanahofu kwamba hivi karibuni mifumo ya asili itaangamia. Matumbawe nayo yako hatarini. Wanasayansi wanakadiria kwamba nusu ya matumbawe duniani imetoweka katika miaka 30 iliyopita.

Je, tuna uwezo wa kufanya mabadiliko yanayohitajika ili ulimwengu uwe salama zaidi? Baadhi ya watu wanahisi kwamba njia moja ya kuleta mabadiliko hayo ni kutoa elimu. Ikiwa ndivyo, ni aina gani ya elimu inayohitajika? Makala zinazofuata zitajibu maswali hayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki