Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 9/22 kur. 18-20
  • Ni Nini Kiwezacho Kufanywa ili Kuokoa Miamba ya Matumbawe?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Nini Kiwezacho Kufanywa ili Kuokoa Miamba ya Matumbawe?
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Mataifa Yote Yatajiunga na Pambano Hilo?
  • Matumbawe—Yamo Hatarini na Yanakufa
    Amkeni!—1996
  • Miamba ya Matumbawe Inayokufa—Je, Wanadamu Wanahusika?
    Amkeni!—1996
  • Tumbawe Kubwa la Belize—Eneo Linalostahili Kuhifadhiwa
    Amkeni!—2007
  • “Dhahabu Nyekundu” ya Mediterania
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 9/22 kur. 18-20

Ni Nini Kiwezacho Kufanywa ili Kuokoa Miamba ya Matumbawe?

WANASAYANSI wengi ulimwenguni pote huamini kwamba kuongezeka kwa joto duniani kunaathiri wanadamu na kwamba kutaendelea kuwa kubaya zaidi nchi zenye kuendelea zifanyapo maendeleo ya viwanda. Tani za metriki zipatazo bilioni tatu za kaboni dioksidi huingizwa katika anga kupitia kuchoma fueli, kama vile makaa-mawe, mafuta, na kuni, kwa ajili ya nishati, na kupitia kuchoma misitu. Kulingana na wanasayansi fulani, ile iitwayo athari ya kuongezeka kwa joto duniani, inayotokana na gesi za kuchomeka kwa fueli, hutisha kuongeza joto la anga kwa digrii 3 hadi 8 za Fahrenheit kufikia katikati ya karne ijayo. Ongezeko hilo laweza kuua matumbawe na jumuiya za miamba ya matumbawe.

Lakini kufa kwa miamba ya matumbawe kwaweza pia kuathiri vibaya maisha ya barani. Gazeti Natural History lilionelea hivi: “Hata hivyo, miamba yenyewe ya matumbawe inatimiza fungu kubwa katika hali ya kuongezeka kwa joto duniani nayo yaweza kuwa muhimu kama misitu ya tropiki katika kupunguza gesi zenye kuongeza joto duniani. Miamba ya matumbawe yawekapo akiba za kalsiamu kabonati kwa ajili ya viunzi vyayo, matumbawe huondoa kiasi kikubwa cha kaboni dioksidi kutoka kwenye bahari-kuu. Bila zooxanthellae [miani inayoishi kwenye matumbawe], kiasi cha kaboni dioksidi ambacho matumbawe hufyonza hupunguka sana. Kwa kushangaza, uharibifu kwa mfumo huu wa mazingira ya chini ya bahari waweza kuharakisha kufa kwayo.”

Wanasayansi wengine huamini kwamba gesi nyinginezo ambazo hutokezwa kwa kuchoma vitu huongezea hali ya kuongezeka kwa joto duniani. Oksidi nitrasi ni moja ya gesi hizo, na kloroflorokaboni (CFC) ni gesi nyingine. Kwa hakika, kila molekuli ya CFC ni bora mara 20,000 katika kunasa joto kuliko molekuli moja ya kaboni dioksidi. Gesi za CFC zimetajwa kuwa kisababishi kikuu cha kupunguka kwa tabaka ya ozoni, ambayo hukinga uhai ulioko duniani dhidi ya miale yenye kudhuru ya urujuanimno. Ozoni katika Ncha ya Kaskazini na Ncha ya Kusini imepunguka sana kiasi cha kutokeza mashimo. Hizo ni habari mbaya zaidi kwa matumbawe. Majaribio yaliyoweka miamba midogo ya matumbawe ambayo tayari ilikuwa chini ya mkazo katika maji yasiyo baridi kwa maongezeko madogo sana ya nuru ya urujuanimno yaliongeza hali ya matumbawe kupoteza rangi. Gazeti Scientific American lilisema hivi kwa masikitiko: “Hata kama mitoko ya kloroflorokaboni ingekoma leo, utendano wa kikemikali wenye kuharibu ozoni ya angastrato ungeendelea kwa angalau karne moja. Kuna sababu sahili: Gesi za floroklorokaboni hudumu muda huo wote katika anga nazo huendelea kupenya angastrato kutokana na akiba zilizopo katika angatropo muda mrefu baada ya mitoko hiyo kukoma.”

Kila mtu mmoja-mmoja aweza kutenda kwa njia ya kujali kwa kutochafua bahari au maeneo ya mwambao kwa takataka au vichafuzi. Ukizuru mwamba wa tumbawe, fuata maagizo ya kutogusa au kutosimama juu ya tumbawe. Usichukue wala usinunue vikumbusho vya matumbawe. Ukiendesha boti karibu na matumbawe ya tropiki, tia nanga katika sehemu zenye mchanga au tumia nanga zenye kuelea zinazotolewa na wenye mamlaka wa bahari. Usiende kwa kasi au kuvuruga chini kwa majembe ya boti yako. Usitupe takataka za boti katika bahari-kuu; tafuta gudi litakalokubali kuzichukua. Bill Causey, meneja wa Hifadhi ya Kitaifa ya Viumbe vya Maji ya Looe Key (Florida, Marekani), alisema hivi: “Labda mwanadamu anafanyiza tatizo ambalo hutokeza ukosefu wa usawaziko. Ni lazima tutambue jambo hilo duniani pote. Tukiendelea kujulisha umma juu ya tisho la kupoteza mfumo mkubwa wa ikolojia, basi labda twaweza kuboresha hali.”

Kwa kiwango cha kimkoa, sheria za kulinda miamba ya matumbawe zinapitishwa na kutekelezwa. Jimbo la Florida hushtaki wenye meli zinazoharibu miamba ya matumbawe. Wenye meli iliyoharibu hektari kadhaa za matumbawe ilipoyakwamia walitozwa faini ya dola milioni 6 [za Marekani]. Sehemu ya pesa hizo zilitumiwa kurekebisha makao hayo ya viumbe vya bahari. Kwa wakati huu, wanabiolojia wakitumia gundi za kipekee, wanajaribu kushikanisha tena tumbawe lililoharibiwa na meli katika 1994. Kampuni nyingine ilitozwa faini nyingine ya dola milioni 3.2 kwa sababu ya madhara yaliyopata miamba ya matumbawe ya Florida yaliyofanywa na mojawapo meli zayo. Nchi nyinginezo pia zinatekeleza vizuizi kama hivyo. Sehemu zipendwazo za kupiga mbizi, kama vile Visiwa vya Cayman katika Karibea, zina sehemu chache ambazo watu wanaruhusiwa kupiga-mbizi. Australia ilianzisha Hifadhi ya Viumbe vya Bahari ya Great Barrier Reef ili kudhibiti utendaji uliokuwa ukiendelea huko. Lakini kama vile wote wameona, kadiri kunavyokuwa na wapiga mbizi zaidi ndivyo uharibifu wa miamba ya matumbawe unavyozidi.

Je, Mataifa Yote Yatajiunga na Pambano Hilo?

Ulimwenguni pote, wanasayansi na viongozi wenye hofu wakata kauli kwamba suluhisho haliwezi kupatikana na taifa moja au hata kikundi cha mataifa. Uchafuzi huenezwa duniani kwa mikondo yenye kuzunguka ya hewa na maji, ikiathiri miamba ya matumbawe. Mataifa moja-moja hayana udhibiti nje ya bahari za kwao. Vichafuzi vinavyotupwa katika bahari-kuu mara nyingi huishia ukingoni. Jitihada za kuungana na suluhisho zinahitajika.

Bila shaka watu wengi wanyoofu na wenye uwezo ulimwenguni wataendelea kujitahidi kuokoa hazina kubwa za matumbawe. Kwa wazi na kwa hima, serikali ya ulimwenguni pote yenye kujali na kutunza mazingira ya dunia inahitajika. Kwa furaha, Muumba mwenyewe ataokoa mazingira ya dunia. Mungu alipoumba wanadamu wa kwanza, alisema hivi: “Wakatawale samaki wa [na viumbe vyote vya] baharini.” (Mwanzo 1:26) Kwa kuwa Mungu hakutumia vibaya viumbe vya bahari, amri yake kwa mwanadamu ni lazima ilimaanisha kwamba mwanadamu alipaswa kutunza mazingira ya dunia. Biblia yatabiri hivi: “Kama ilivyo ahadi yake, [tu]natazamia mbingu mpya [Ufalme wa kimbingu wa Mungu] na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.” (2 Petro 3:13) Katika wakati ujao ulio karibu, serikali hiyo ya kimbingu itasafisha kabisa dunia hii iliyochafuliwa, kutia ndani bahari-kuu. Kisha, wakazi wa Ufalme wa Mungu watatunza na kufurahia kikamili bahari-kuu zilizo maridadi na viumbe vyazo.

[Picha katika ukurasa wa 18]

Mandhari-nyuma: Mwamba maridadi wa matumbawe katika Bahari-Kuu ya Pasifiki, karibu na Fiji

Picha za ndani: 1. Picha ya karibu ya juhabahari, 2. tumbawe lifananalo na meza, 3. ushimbu asafishaye kwenye tumbawe

[Hisani]

Ukurasa 18 mandhari-nyuma: Fiji Visitors Bureau

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki