Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g22 Na. 1 kur. 7-9
  • 2 | Linda Mapato Yako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • 2 | Linda Mapato Yako
  • Amkeni!—2022
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • KWA NINI NI MUHIMU?
  • Unachopaswa Kujua
  • Unachoweza Kufanya Sasa
  • Jinsi ya Kuishi Ukiwa na Pesa Kidogo
    Habari Zaidi
  • Jinsi ya Kujiepusha na Deni
    Amkeni!—1996
  • Kupanga Matumizi ya Pesa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Kukabiliana na Madeni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2022
g22 Na. 1 kur. 7-9
Seremala akipigilia msumari kwenye kipande cha mbao.

ULIMWENGU WENYE MISUKOSUKO

2 | Linda Mapato Yako

KWA NINI NI MUHIMU?

Watu wengi huhangaika kila siku ili kupata mahitaji ya msingi. Kwa kusikitisha, misukosuko ya ulimwengu huu inaweza kufanya hali iwe ngumu zaidi. Kwa nini?

  • Gharama za vyakula na makazi huongezeka sana katika maeneo yenye misukosuko.

  • Majanga yanaweza kusababisha ukosefu wa ajira, au kupungua kwa mishahara.

  • Majanga yanaweza kusababisha uharibifu wa nyumba, biashara, au mali nyingine na kuwalazimisha watu wengi wawe maskini.

Unachopaswa Kujua

  • Kadiri unavyojua kupanga vizuri matumizi ya pesa, ndivyo utakavyoweza kujitayarisha vizuri kwa ajili ya majanga.

  • Kumbuka kwamba unaweza kupoteza kipato, akiba ya pesa, na mali.

  • Kuna vitu ambavyo pesa haiwezi kununua kama vile, furaha na umoja katika familia.

Unachoweza Kufanya Sasa

Biblia inasema hivi: “Tukiwa na chakula na mavazi, tutaridhika na vitu hivyo.”​—1 Timotheo 6:8.

Kuridhika kunatia ndani kudhibiti tamaa ya vitu tunavyotaka na kutosheka na mahitaji yetu ya kila siku. Ni muhimu kufanya hivyo hasa ikiwa tumepoteza kazi.

Ili kuridhika, huenda ukahitaji kurekebisha mtindo wako wa maisha. Ukitumia pesa nyingi kuliko kipato chako, huenda hali ikawa mbaya zaidi.

JINSI YA KUKABILIANA NA HALI​—Madokezo Yanayofaa

Wakati wa misukosuko, linda mapato yako kwa kuchukua hatua hizi zinazofaa

PUNGUZA GHARAMA

  • Mwanamke mwenye umri mkubwa akivuna karoti katika bustani ya mboga.

    Punguza gharama

    Usinunue vitu usivyohitaji. Jiulize: ‘Je, kweli ninahitaji kutumia gari yangu? Je, ninaweza kuwa na bustani ya mboga?’

  • Kabla ya kununua kitu, jiulize: ‘Ninakihitaji kweli? Nina pesa za kukinunua?’

  • Omba msaada kutoka kwa serikali au mashirika ya kutoa msaada, ikiwa unatolewa.

“Tukiwa familia tulichunguza na kuzungumzia mtindo wetu wa maisha. Tulisitisha au kupunguza burudani zozote ambazo zilitugharimu kiasi kikubwa cha pesa. Pia, tulianza kupika vyakula ambavyo havikugharimu kiasi kikubwa cha pesa.”​—Gift.

PANGA BAJETI

Mwanamke akipiga hesabu na kuandika taarifa zilizo kwenye risiti.

Panga bajeti

Biblia inasema hivi: “Mipango ya wenye bidii hakika huleta mafanikio, lakini wote walio na haraka kwa hakika watakuwa maskini.” (Methali 21:5) Bajeti itakusaidia kuhakikisha kwamba matumizi hayazidi kipato chako.

  • Kwanza, orodhesha mapato unayotarajia kupata kila mwezi.

  • Kisha, orodhesha matumizi yako ya kila mwezi, na uchunguze kwa makini jinsi unavyotumia pesa.

  • Halafu, linganisha mapato na matumizi yako, na ikihitajika chunguza mambo unayohitaji kupunguza au kuyaondoa, ili matumizi yako yalingane na kipato chako.

“Kila mwezi, sisi huorodhesha mapato na matumizi yetu. Tunajitahidi kuwa na akiba ya pesa kwa ajili ya dharura na kupanga matumizi ya wakati ujao. Tunashukuru kwamba kufanya hivyo kumetupunguzia mahangaiko kwa sababu, tunajua mapema jinsi tutakavyotumia pesa zetu.”​—Carlos.

EPUKA MADENI / WEKA AKIBA

  • Mama akimsaidia binti yake kuhifadhi pesa kwenye chupa.

    Epuka madeni / weka akiba

    Weka mkakati mzuri wa kulipa deni. Ikiwezekana epuka madeni. Badala yake, weka akiba ya pesa ikiwa unataka kununua kitu.

  • Weka akiba ya kiasi fulani cha pesa kila mwezi, kwa ajili ya gharama za wakati ujao unazotarajia au usizotarajia.

FANYA KAZI KWA BIDII / DUMISHA KAZI YAKO

Biblia inasema hivi: “Kila aina ya kazi ngumu ina faida.”​—Methali 14:23.

  • Seremala akipigilia msumari kwenye kipande cha mbao.

    Fanya kazi kwa bidii / dumisha kazi yako

    Dumisha mtazamo mzuri kuhusu kazi yako. Hata kama huipendi kazi hiyo, bado inakupatia kipato.

  • Fanya kazi kwa bidii na uwe mwenye kutegemeka. Hilo linaweza kukusaidia kudumisha kazi yako au kufanya iwe rahisi kwako kupata kazi wakati ujao.

“Mimi hufanya kazi yoyote inayopatikana hata ikiwa siipendi au ninalipwa mshahara mdogo. Sikuzote mimi hujitahidi kufanya kazi vizuri kama kazi yangu binafsi.”​—Dmitriy.

Ikiwa unatafuta kazi . . .

  • Chukua hatua ya kwanza. Wasiliana na kampuni ambazo huenda zina kazi unazoweza kufanya, hata kama hawajatangaza nafasi ya kazi. Waeleze marafiki na watu wa familia kwamba unatafuta kazi.

  • Uwe mwenye kubadilika. Huenda usipate kazi unayoitaka.

Wazazi wakizungumzia hali yao ya kiuchumi huku watoto wao wakicheza nje.

JIFUNZE MENGI ZAIDI. Soma makala yenye kichwa, “Jinsi ya Kuishi Ukiwa na Pesa Kidogo.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki