Sura ya 6
Yesu Kristo, Yeye Ambaye Kupitia Kwake Mungu Hubariki Wanadamu
1. Ni katika nini ni lazima kabisa kwetu kuwa na imani ikiwa tutapokea baraka za uzima wa milele?
JINSI ulivyo mpango wa upendo ambao Yehova amefanya kupitia kwa Mwanawe kwa kuwabariki watu wa kabila zote na mataifa yote! Yeye ameahidi ukombozi wa kudhulumiwa, dhambi na mauti. Lo! tumaini tukufu namna gani! Walakini, ni lazima kwetu sisi kuthamini kwamba baraka hizi zitakuja kwa wanadamu kupitia kwa Yesu Kristo peke yake. Kwa sababu hii, Mungu alimwongoza kwa roho yake mtume Petro kusema habari ya Yesu: “Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” (Matendo 4:12) Kwa kupata maarifa yaliyo sahihi ya mpango huu na kwa kutumia imani katika kusudi la Mungu kuhusiana na Yesu, unaweza kujiweka mwenyewe katika njia ya kupokea baraka za ajabu za uzima wa milele.
2. (a) Ni ahadi gani ya baraka ambayo Mungu alifanya kwa Ibrahimu, na ni nani aliyethibitishwa kuwa “uzao” wake? (b) Ni kwa nani ukuhani na dhabihu chini ya sheria ya Musa zilielekeza? (c) Biblia huonyeshaje nani angekuwa mfalme wa ufalme wa Mungu?
2 Kwa maelfu ya miaka wanadamu wenye imani wamengojea utimizo wa tumaini hili, na ahadi za Mungu ziliwapa sababu nzuri kwa kufanya hivyo. Kwa Ibrahimu kichwa cha jamaa ya Kiebrania, Yehova alifanya ahadi kwamba “mataifa yote ya, dunia” yangebarikiwa kupitia kwa “uzao” wake. “Uzao” huo zaidi ulionekana kuwa ni Yesu Kristo. (Mwanzo 22: 18; Wagalatia 3:14-16, 28, 29) Mungu pia alifanya mpango kwa ukuhani na dhabihu chini ya Sheria iliyopewa kwa Israeli. Hivi pia vilionyesha mbele kwa Yesu. Vilielekeza kwake kama Kuhani Mkuu aliye juu na kwenye dhabihu ya uhai wake mwenyewe wa kibinadamu kama njia ya kuondoa dhambi milele na kuleta ukombozi hata wa mauti. (Wagalatia 3:24; Waebrania 9:11, 12; Yohana 1:29) Tena, Yehova alitabiri kwamba yeye ambaye kupitia kwake amani ya milele ingeletwa kwa wanadamu angetoka katika ukoo wa Mfalme Daudi naye angekuwa mfalme wa ufalme wa Mungu, kutawala juu ya dunia nzima. Malaika Gabrieli, katika kutangaza uzaliwa wa kibinadamu wa Yesu, akasema: “Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na [Yehova] Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.” (Luka 1:32; tazama pia Isaya 9:6, 7; Danieli 7:13, 14) Naam, Neno zima la Mungu huelekeza kwa Yesu Kristo kama yeye ambaye kupitia kwake Yehova Mungu atatoa baraka za uzima wa milele kwa wanadamu.—Luka 2:25-32; Wafilipi 2: 9-11.
KUWAKO KABLA YA KUWA BINADAMU
3. (a) Jinsi gani Yesu ni Mwana “mzaliwa wa kwanza” wa Mungu? (b) Kwa nini Biblia husema Yesu ni Mwana “pekee” wa Mungu?
3 Je! unajua kwamba Yesu alikuwa na kuwako kwa utukufu zamani kabla hajazaliwa kama binadamu ha-pa duniani? Biblia hutupasha sisi habari kwamba ye-ye ni Mwana “mzaliwa wa kwanza” wa Mungu. Maana yake ni kwamba yeye aliumbwa kabla ya wana wengine wa jamaa ya Mungu. Yeye pia ni Mwana “pekee wa Mungu,” kwa vile yeye ndiye peke yake kuumbwa moja kwa moja na Yehova Mungu; vitu vyote vingine vilipata kuwako kupitia kwa yeye kama Wakili Mkuu wa Mungu. Hivyo, kabla ya kuzaliwa duniani kama mtoto wa kiume yeye alitumikia mbinguni, ali-kojulikana kama “Neno,” mneni wa Mungu.—Yohana 1:3, 10, 14; Wakolosai 1:15-17.
4. Yesu alisema nini kushuhudia, kwamba alikuwa ameishi
4 Kwahiyo Yesu angeweza kusema kwa kufaa: “Ibrahimu asijakuwako, mimi niko,” na, “Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni.” (Yohana 8:58; 6:51) Akitaja cheo cha juu alichokuwa anacho mbinguni, alisali: “Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.”—Yohana 17:5.
MAISHA YAKE DUNIANI
5. (a) Ulipofika wakati wa Mungu kwa Mwanawe kuwa mwanadamu duniani, Mungu alitimizaje jambo hili? (b) Jinsi gani mtoto Yesu angeweza kuzaliwa bila dhambi ya Admu?
5 Kupatana na kusudi la Mungu kwa kubariki wanadamu wenye imani, uliwadia wakati uliowekwa kwa Mwana huyu wa mbinguni kuwa mwanadamu duniani. Hii ilihitaji mwujiza wa Mungu. Kwa njia ya roho yake takatifu au nguvu ya utendaji, Yehova alihamisha uhai wa Yesu kutoka mbinguni kuuleta katika tumbo la uzazi la msichana bikira wa Kiyahudi jina lake Mariamu. Akitangaza jambo hili kwa Mariamu kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, malaika Gabrieli akasema: “Roho takatifu itakuja juu yako wewe, na nguvu za Aliye Juu sana zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hiyo pia kizaliwacho kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.” (Luka 1:35, NW) Basi iliwezekana kwa Muumba kufanya jambo hili. Hakika Yeye aliyemfanya mwanamke wa kwanza kuwa na uwezo wa kuzaa watoto angeweza kumechukulisha mimba mwanamke pasipo baba wa kibinadamu, Mungu mwenyewe akichukua madaraka moja kwa moja kwa uhai wa mtoto. Mtoto huyu, Yesu, alikuwa si Mungu, bali Mwana wa Mungu. Yeye alikuwa binadamu mkamilifu, aliye huyu na dhambi ya Adamu. Jambo hilo liliwezekanaje? Kwa sababu, kama malaika alivyosema, “nguvu za Aliye Juu sana” ndizo zilizokuwa na madaraka; hata zikaongoza ukuzi wake alipokuwa katika tumbo la uzazi la Mariamu.
6. (a) Kama ilivyotabiriwa katika unabii, Yesu alizaliwa wapi? (b) Kwa nini Yesu alibatizwa?
6 Kama ilivyotabiriwa karne nyingi zamani, Yesu alizaliwa katika mji wa Mfalme Daudi, Bethlehemu ya Uyahudi. (Mika 5:2) Yeye aliishi pamoja na mamaye na babaye mlezi Yusufu, akifanya kazi ya useremala mpaka alipokuwa karibu mwenye umri wa miaka thelathini. Ndipo ukaja wakati kwake kufanya kazi nyingine. Basi alimwendea Yohana Mbatizaji ili abatizwe au azamishwe kabisa chini ya maji ya Mto Yordani. Jambo hili lilionyesha kwamba yeye alikuwa akijitoa mwenyewe kwa Mungu ili kuifanya kazi ambayo Mungu alikuwa amemtuma duniani aifanye. Kwa kubatizwa Yesu aliweka mfano kwa wote watumiao imani katika yeye, na baadaye akaamuru kwamba wote waliogeuka kuwa wanafunzi wake ingewapasa kubatizwa.—Mathayo 28:19, 20.
7. Mungu alifanya nini wakati wa ubatizo wa Yesu?
7 Walakini, kukatukia jambo jingine kwa Yesu Yordani. Mbingu ilifunuka, roho ya Mungu ikaja juu yake, na Mungu mwenyewe akasema kutoka mbinguni, akisema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” (Mathayo 3:16, 17) Kulikuwa hakuna kukosea juu yake; huyu alikuwa ndiye ambaye manabii wote wa Mungu walikuwa wamemtabiri! Pale Yordani, kwa njia ya roho takatifu, Yesu alitiwa mafuta na Mungu kuwa ndiye kuhani mkuu aliye juu aliyetabiriwa, mfalme wa ufalme wa Mungu, na kuhubiri wakati alipokuwa hapa duniani. (Luka 4: 16-21) Kulikuwako kazi kwake kuifanya.
8. Je! Yesu aliacha kutumia jina la peke yake la Mungu au kutosema kweli? Basi imetupasa tufanye nini?
8 Kwa miaka mitatu na nusu alilihubiri Neno la Mungu katika nchi yote, na akafundisha wanafunzi wake kufanya lilo hilo. (Luka 8:1) Ijapokuwa wengine katika siku hizo kwa hofu ya uongo ya Mungu waliepuka kutumia jina la peke yake la Mungu, Yesu hakuacha kulijulisha. (Yohana 17:26) Sikuzote alisema kweli, kwamba iliwapendeza watu wote au sivyo. Katika jambo alilolifanya alitoa mfano kwamba nasi tufuate ikiwa tunataka kumpendeza Mungu. Lakini yeye alitimiza pia zaidi kuliko hilo.
ONDOLEO LA DHAMBI NA MAUTI
9. (a) Kupatana na Mathayo 20:28, kwa sababu gani nyingine Yesu alikuja duniani? (b) Ni nini bei ya ukombozi ambayo Yesu alilipa kwa kutufungua sisi na dhambi na mauti?
9 Yesu alijua kwamba kuja kwake duniani kama mwanadamu ilikuwa ni sehemu ya moja kwa moja ya mpango wa Mungu kwa kuwafungua wanadamu katika dhambi na mauti. Hivyo akasema: “Mwana wa Adamu alikuja . . . kuitoa nafsi yake lye ukombozi badala ya wengi.” (Mathayo 20:28, NW) Hasa jambo hilo lilimaanisha nini? Naam, ukombozi ni bei inayolipwa ili kupata ukombozi wa utumwa. Katika habari hii, uhai mkamilifu wa kibinadamu wa Yesu uliotolewa katika dhabihu ulikuwa ndiyo bei iliyolipwa ili kupata kufunguliwa kwa wanadamu katika utumwa wa dhambi na mauti. (1 Petro 1:18, 19) Kwa nini kufunguliwa kwa namna hiyo kulihitajiwa?
10. Kwa nini tungeweza kupokea kutoka kwa Adamu urithi wa dhambi na mauti tu?
10 Hii ilikuwa kwa sababu Adamu, babu wa sisi sote, alikuwa amemkosea Mungu. Hivyo, Adamu akawa asiyekamilika na akapoteza haki kwenye uzima. Kama mvunjaji mwenye kukusudia wa sheria ya Mungu, yeye alikuja chini ya adhabu ya mauti. Mungu pia alikuwa ameweka sheria za urithi, zinazohakikisha kwamba sisi sote tulipokea tabia za kimwili na tabia nyingine kutoka kwa wazazi wetu. Kupatana na sheria hizi, Adamu angeweza kupeleka tu kwa watoto wake kile ambacho yeye mwenyewe alikuwa nacho; basi tulipokea kutoka kwa yeye urithi wa dhambi na mauti. (Warumi 5:12) Kwa hiyo wanadamu wote wamekuwa wakifa kwa kulipa adhabu ya dhambi. Adhabu hii ya mauti ingeondolewaje na matakwa ya haki bado yatimizwe?
11. Kwa kutayarisha ondoleo kwa watoto wa Adamu, jinsi gani Mungu alionyesha heshima inayofaa kwa sheria?
11 Mungu hakudhoofika na kuridhiana kwa habari ya sheria yake mwenyewe. Jambo hili lingalitia moyo tu uvunjaji zaidi wa sheria kwa mfano mbaya. Lakini hakuwapa wanadamu kisogo na kuwaacha bila tumaini. Huku akishikamana na sheria zake, kwa upendo Mungu alitayarisha ondoleo, si kwa mkosaji mwenye kukusudia Adamu, bali kwa watoto wa Adamu, ambao, bila hiari yo yote katika shauri, walipatwa na matokeo ya kosa lake. Mungu alifanya hivi kupatana na kanuni ya halali ambayo baadaye aliitia katika sheria ya Musa, yaani, “uzima kwa uzima.” (Kumbukumbu la Torati 19:21) Ebu tuone jinsi kanuni hiyo ilivyotumika katika ukombozi uliotayarishwa kupitia kwa Yesu.
12. Nani peke yake angeweza kutayarisha bei ya ukombozi kwa ambacho Adamu alipoteza? Basi kwa nini ilimpasa Yesu azaliwe kama binadamu?
12 “Nafsi hai” Adamu, aliyewapotezea wanadamu uzima, alikuwa binadamu mkamilifu. Badala ya kile alichopoteza, nafsi nyingine ya kibinadamu, iliyo sawa na Adamu, ilihitajiwa, yeye ambaye angetoa uzima wake mwenyewe mkamilifu kama dhabihu kwa ajili ya wanadamu. (1 Kor. 15:45) Hapana mmoja wa watoto wa Adamu aliyestahili kwa jambo hili, kwa sababu wote walizaliwa bila kukamilika. Kama matokeo wote hufa kwa sababu wao ni wenye dhambi, na hawana haki kwenye uzima wa kibinadamu kwamba wanaweza kutoa dhabihu kwa ajili ya wengine. (Zaburi 49:7) Hivyo Mungu alimtuma Mwanawe mwenyewe duniani. Yesu alizaliwa kama binadamu, kwa sababu ilikuwa ni uzima wa kibinadamu uliotakiwa. Lakini yeye alizaliwa pasipo msaada wa baba ya kibinadamu, hata angekuwa mkamilifu kama Adamu alivyokuwa. Mungu peke yake alikuwa ndiye Baba ya binadamu Yesu, kama vile alivyokuwa amekuwa pia Baba ya Adamu. (Luka 3:38, NW) Hivyo Yesu alistahili kabisa kutoa uzima wake kama “ukombozi unaolingana.”—1 Timotheo 2:6, NW; Waefeso 1:7.
13. Kwa nini Yesu aliutoa uhai wake kwa nia na asipinge?
13 Nisani 14 ya mwaka wa 33 C.E. adui za Yesu walimwua penye mti wa mateso. Yeye angaliweza kupinga, lakini hakupinga. (Mathayo 26:53, 54) Kwa nia yeye aliutoa uhai wake katika dhabihu kwa ajili yetu. Kama mtume wake Petro atuambiavyo: “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; ili, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.”—1 Petro 2:24; tazama pia Waebrania 2:9.
14. Ni nini Biblia hutuambia juu ya upendo wa Mungu kwa wanadamu katika Yohana 3:16? Basi imetupasa tuitikieje?
14 Hilo lilikuwa kweli onyesho la ajabu la upendo wa Mungu kwa wanadamu! Biblia hutusaidia sisi kulithamini, ikisema: “Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16) Ikiwa wewe u mzazi aliye na mtoto mwenye kupendwa sana, bila shaka unaweza kuthamini, hata kwa kiasi fulani, jambo hilo lilimaanisha nini kwa Mungu. Bila shaka lazima lifurahishe mioyo yetu kuelekea yeye kujua kwamba yeye hutuangalia sisi sana.—1 Yohana 4:9-11.
15. (a) Je! Yesu alifufuliwa na mwili wa kibinadamu? (b) Baada ya kufufuka kwake, kwa nini Yesu aliwatokea kwa kuonekana wanafunzi wake? (c) Je! ilikuwa lazima kwa Yesu kurudia mbinguni? Kwa nini?
15 Yehova Mungu hakumwacha Mwanawe hali amekufa katika kaburi, bali alimfufua kwenye uhai siku ya tatu. Hakupewa uhai wa kibinadamu tena, kwa sababu hiyo ingalimaanisha kwamba alikuwa akirudisha tena bei ya ukombozi. Lakini alifanywa “hai katika roho.” (1 Petro 3:18, NW) Wakati wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake aliwatokea kwa kuonekana wanafunzi wake mara nyingi, katika miili yenye umbo, kuthibitisha kwamba kweli alikuwa amefufuka kutoka kwa wafu. Ndipo, na wanafunzi wakitazama, alipopaa kuelekea mbinguni na akafichwa katika wingu. Alirudia mbinguni, “aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu” kule akichukua thamani ya dhabihu yake ya ukombozi kama kuhani mkuu aliye juu. (Waebrania 9:12, 24) Matakwa ya haki ya kimungu yalikuwa yametimizwa; sasa ondoleo lilipatikana kwa wanadamu.
16. (a) Eleza jinsi gani tunafaidika hata sasa na mpango wa
16 Hata sasa twaweza kufaidika sana na ukombozi. Kwa kutumia imani ndani yake twaweza kujifurahisha hali iliyo safi mbele za Mungu na kuja chini ya uangalizi wake wa upendo. (Ufunuo 7:9, 10, 13-15) Wakati, kwa sababu ya kutokukamilika, tunafanya dhambi, twaweza kutafuta msamaha kutoka kwa Mungu bila kupita juu ya msingi wa ukombozi, tukitumaini ya kwamba yeye atatusikia sisi. (1 Yohana 2:1, 2) Tena, ukombozi umefungua njia kwa kuhifadhiwa kupita katika mwisho wa taratibu hii mbovu iliyopo ya mambo. Huwezesha ufufuo wa wafu. Na hutoa msingi kwa kupata uzima wa milele katika taratibu mpya ya mambo ya Mungu, ambamo utatumiwa kwa wanadamu ili kufutilia mbali matokeo yote ya dhambi iliyorithiwa.—1 Wakorintho 15:25, 26; Ufunuo 7:17.
MTAWALA WA UFALME WA MUNGU
17. (a) Ni kuelekea nini Yesu kila mara alivuta nia, akikifanya kuwa ndicho kichwa cha kuhubiri kwake? (b) Yesu alionyesha nini kwa miujiza yake ya kuponya na kufufua wafu?
17 Wakati wa huduma yake ya kidunia Yesu kila mara alielekeza kwenye ufalme wa Mungu. Aliwafundisha wafuasi wake kuomba: “Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.” Tena aliwatia moyo kutafuta “kwanza ufalme.” (Mathayo 6:9, 10, 33) Mingi ya mifano yake ilivuta nia kwenye Ufalme. Aliufanya kuwa kichwa cha kuhubiri kwake. (Mathayo 9:35) Kwa miujiza yake ya kuponya na kufufua wafu, alionyesha kwa kiasi kidogo yatakayotokea duniani chini ya ufalme wa Mungu. Wakati huo maradhi yatakoma, macho yaliyopofuka yatafumbuliwa, masikio ya viziwi yatazibuliwa, na mikono na miguu iliyolemaa itaponywa. Lo! hiyo itakuwa baraka namna gani!—Ufunuo 21:3, 4.
18. (a) Je! Yesu alitumia mamlaka ya, kifalme mara aliporudia mbinguni? Kwa nini? (b) Kupatana na Mathayo 25:31, 32, ni
18 Yesu mwenyewe ndiye aliyetiwa mafuta na Mun-gu kama mtawala wa Ufalme. Walakini, wakati Yesu aliporudi mbinguni haukuwa wakati kwake kutumia mamlaka hiyo ya kifalme. Lazima angojee wakati uliowekwa na Baba yake. (Matendo 2:34-36) Lakini, alionyesha mbele kwa wakati ambao angerudi na mamlaka ya Ufalme, akisema: “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi.” (Mathayo 25:31, 32) Tunaishi katika wakati huo sasa. Upesi Kristo penye kiti chake cha enzi cha kimbinguni atatumia mamlaka yake ya kifalme kuwaharibu waovu na kuwaokoa watu walio mfano wa kondoo ambao watarithi makao ya kidunia ya Ufalme.—Mathayo 25:34, 41, 46.
19. Kujifurahisha baraka kupitia kwa Yesu Kristo, lazima tufanye nini?
19 Kwa njia ya Yesu Kristo baraka zinapatikana kwa wanadamu wote, lakini lazima tutumie imani katika yeye ili tuzipokee. (Yohana 3:36) Lazima tuwe wanafunzi wake na kujinyenyekeza wenyewe kwake kama mfalme wetu wa mbinguni. Je! wewe utafanya hivyo? Wako wapinzani wanaotaka kukuzuia, lakini ukiweka tumaini kamili katika Yehova haikosi utapokea baraka ambazo Mungu amewawekea akiba wale wampendao.—Zaburi 62:7, 8.
mbinguni kabla ya kuja dunlani?
ukombozi. (b) Tufikiriapo wakati ujao, ukombozi huwezesha nini kwetu na kwa wafu?
nini Yesu alisema angefanya wakati aliporudi na mamlaka ya Ufalme?