Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 1 kur. 7-10
  • Yesu, Mwalimu Mkuu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu, Mwalimu Mkuu
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Yesu Alikuwa Mwalimu Mkuu?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Namna ya Kumwambia Mungu, ‘Mimi Nakupenda’
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Yesu Kristo Ni Nani?
    Biblia Inatufundisha Nini?
  • Sikiliza Sauti ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 1 kur. 7-10

Sura ya 1

Yesu, Mwalimu Mkuu

UNAPENDA kusikia hadithi? Basi, nitakusimulia moja juu ya mtu aliyesimulia hadithi bora kuliko ye yote ambaye ameishi duniani. Jina lake ni Yesu Kristo.

Yeye aliishi katika dunia hii karibu miaka 2,000 iliyopita. Hiyo ni zamani sana. Ni zamani mbele ya kuzaliwa nyanya na babu yako. Na ni zamani mbele ya watu kuwa na motokaa au garimoshi au radio na vitu vingine vya leo.

Yesu aliposimulia hadithi ilifanya mtu afikiri. Ikiwa mtu angeifikiria sana, mambo ambayo Yesu alisema yangeweza hata kugeuza maoni au mawazo yake juu ya mambo. Yangeweza kugeuza maoni yake yote ya maisha. Na kila kitu ambacho Yesu alisema kilikuwa kweli.

Yesu alijua zaidi kuliko mtu mwingine ye yote. Yeye alikuwa mwalimu bora ambaye alipata kuishi. Tunajifunza mambo mengi kwa watu wengine. Lakini twaweza kujifunza mambo ya maana zaidi sana kwa Yesu.

Sababu moja Yesu alikuwa mwalimu mkuu sana ni kwa vile alisikiliza. Alijua namna lilivyo jambo la maana kusikiliza. Lakini Yesu alimsikiliza nani? Nani alimfundisha? Ni Baba ya Yesu. Na Baba ya Yesu ni Mungu.

Mbele ya kuja duniani kama mwanadamu, Yesu alikuwa ameishi mbinguni na Mungu. Basi Yesu alikuwa tofauti na wanadamu wengine. Maana hapana mwanadamu mwingine aliyeishi mbinguni mbele ya kuzaliwa duniani. Mbinguni Yesu alikuwa amekuwa Mwana mzuri aliyemsikiliza Baba yake. Basi Yesu aliweza kufundisha watu yale aliyojifunza kwa Mungu. Kwa kumsikiliza baba yako na mama yako unaweza kuwa kama Yesu.

Sababu nyingine Yesu alikuwa mwalimu mkuu ni kwamba aliwapenda watu. Alitaka awasaidie wajifunze juu ya Mungu. Yesu aliwapenda watu wazima. Lakini je! aliwapenda watoto?— Ndiyo. Nao watoto walipenda kukaa na Yesu kwa sababu angesema nao na kuwasikiliza.

Siku moja wazazi waliwapeleka watoto wao kwa Yesu. Lakini rafiki za Yesu walifikiri Mwalimu Mkuu hakuwa na nafasi ya kusema na watoto wadogo. Basi wakawaambia waondoke. Lakini je! Yesu alikubali?— Sivyo. Alisema: ‘Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwakataze.’ Hata ingawa alikuwa mtu mwenye hekima na mtu mkubwa sana, Yesu alipata nafasi ya kufundisha watoto.— Mathayo 19:13, 14.

Yesu alikuwa mwalimu mkuu kwa sababu alijua namna ya kufanya mambo yapendeze. Alisema juu ya ndege na maua (fleurs) na mambo mengine kusaidia watu wafahamu juu ya Mungu. Siku moja alitoa mahubiri au hotuba kwa watu wengi waliokuja kwake alipokuwa upande wa mlima. Yanaitwa Mahubiri juu ya Mlima.

Yesu aliwaambia watu: ‘Watazameni ndege angani. Hawapandi mbegu. Hawaweki chakula katika ghala. Lakini Mungu mbinguni anawalisha. ninyi si bora kuwapita?’

Yesu akasema tena: ‘Jifunzeni kwa maua ya shambani.’ Unafikiri twaweza kujifunza nini kwa maua? Vema, Yesu alisema: ‘Hayatengenezi nguo. Na tazama ni mazuri kama nini! Hata Mfalme Sulemani tajiri hakuvaa vizuri zaidi kuliko maua ya shambani. Basi ikiwa Mungu anaangalia maua yanayomea, je! hataangalia ninyi vile vile?’

Je! unafahamu somo ambalo Yesu alikuwa akifundisha hapo?— Yeye hakutaka wasumbuke wangepata wapi chakula au nguo za kuvaa. Mungu anajua lazima watu wawe na vitu hivi. Yesu hakusema tusifanye kazi tupate chakula na nguo. Bali alisema tumweke Mungu kwanza. Tukifanya hivyo, Mungu atahakikisha tunacho chakula na nguo za kuvaa. Je! wasadiki hilo?— —Mathayo 6:25-33.

Watu walipenda namna Yesu alivyofundisha. Walistaajabu. Ilipendeza kumsikiliza. Na mambo ambayo alisema yalisaidia watu wafanye mema.

Ni jambo la maana na sisi tumsikilize. Lakini twaweza kufanya hivyo namna gani? Tuna maneno ya Yesu yameandikwa katika kitabu. Unakijua ni kitabu gani? Ni Biblia Takatifu. Basi twaweza kumsikiliza Yesu kwa kusoma Biblia.

Mungu mwenyewe anasema tumsikilize Yesu. Siku moja Yesu alipokuwa na rafiki zake watatu juu katika mlima mrefu, sauti kutoka mbinguni ilisema:.”Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.” Unajua hiyo ilikuwa sauti ya nani?— Ilikuwa ya Mungu! Mungu alisema tumsikilize Mwana wake.​—Mathayo 17:1-5.

Je! utamsikiliza Mwalimu Mkuu?— Ndivyo imetupasa sote tufanye. Tukifanya hivyo tutakuwa wenye furaha. Tena itatuletea furaha tukiwaambia rafiki zetu mambo mema tunayojifunza.

(Kwa mawazo mazuri zaidi juu ya faida zitokanazo na kumsikiliza Yesu, fungua Biblia yako msome pamoja Yohana 8:28-30; 3:16; Matendo 4:12.1)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki