Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 16 kur. 67-70
  • Mtu Aliyekuwa Maiti Siku Nne

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtu Aliyekuwa Maiti Siku Nne
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Inakuwaje Tunapokufa?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Inakuwaje Wakati wa Kufa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Yesu Amfufua Lazaro
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Kwa Nini Yesu Alikawia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 16 kur. 67-70

Sura ya 16

Mtu Aliyekuwa Maiti Siku Nne

JE! SI vizuri sana kuwa hai? Je! unajifurahisha uhai?— Mimi najifurahisha kuishi. Tunapokuwa hai twaweza kufanya mambo mengi sana yenye kupendeza.

Lakini ulijua kwamba hapana mtu ambaye ameishi milele?— Imewapasa watu wote wafe. Unamjua mtu ambaye amekufa?—

Siku moja rafiki mzuri wa Yesu alikufa. Rafiki huyu aliishi katika Bethania, mji mdogo si mbali na Yerusalemu. Jina lake alikuwa Lazaro, naye alikuwa na dada zake wawili, majina yao waliitwa Martha na Mariamu.

Siku moja Lazaro akawa mgonjwa sana. Wakati huo Yesu alikuwa mbali. Basi Martha na Mariamu wakatuma habari kwake kwamba ndugu yao Lazaro alikuwa mgonjwa. Kwa sababu gani walifanya hivi? Kwa sababu walijua kwamba Yesu angeweza kumponya ndugu yao. Yesu hakuwa daktari, lakini alikuwa na nguvu kutoka kwa Mungu hata aliweza kuponya kila aina ya ugonjwa.

Lakini wakati Yesu hajafika, Lazaro akawa mgonjwa sana hata akafa. Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba Lazaro alikuwa akilala usingizi. Lakini Yesu akasema kwamba angekwenda akamwamshe. Wanafunzi wake hawa-kufahamu Yesu alikuwa na maana gani. Basi, ndipo Yesu akasema waziwazi kwamba Lazaro alikuwa amekufa. Mauti ni kama usingizi mzito, usingizi mzito sana hata mtu haoti ndoto.

Sasa Yesu akaenda kumwona Martha na Mariamu. Walikuwako vile vile rafiki wengi huko wa jamaa. Walikuwa wamekuja kufariji Martha na Mariamu kwa sababu ndugu yao alikuwa amekufa.

Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa akija, akatoka nje kumlaki. Ndipo naye Mariamu akatoka kumlaki Yesu. Alikuwa mwenye huzuni sana na alikuwa akilia, akaanguka miguuni pake. Rafiki wengine, waliokuwa wamemfuata Mariamu, walikuwa wakilia vile vile. Yesu alipoona watu wote wakilia, alihuzunika akaanza naye kulia.

Mwalimu Mkuu akauliza mahali walipokuwa wamemweka Lazaro. Ndipo watu wakamwongoza Yesu kwenye pango ambapo Lazaro alikuwa amezikwa. Ndipo Yesu akawaambia wanaume huko: ‘Liondoeni jiwe mbele ya pango.’ Je! ilifaa wafanye hivyo?—

Martha hakufikiri ilifaa. Akasema: ‘Bwana, kwa sasa bila shako ananuka, maana amekuwa maiti siku nne.’ Na ni kweli maiti zinanuka ukipita muda mchache.

Lakini Yesu akamwambia: “Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?” Yesu alikuwa na maana ya kwamba Martha angeona jambo fulani ambalo lingeleta heshima kwa Mungu. Yesu alitaka kufanya nini?

Wakati jiwe lilipokwisha kuondolewa, Yesu alisali kwa sauti kuu kwa Yehova. Kisha Yesu akasema kwa sauti kuu: “Lazaro, njoo huku nje.” Angetoka nje? Angeweza?—

Basi, je! waweza kumwamsha mtu fulani ambaye yuko usingizini?— Ndiyo, ukiita kwa sauti kuu, ataamka. Lakini waweza kumwamsha mtu ambaye yuko katika usingizi wa mauti?— Hapana. Hata ukiita kwa sauti kuu, yule mfu hatasikia. Hakuna jambo ambalo wewe au mimi twaweza kufanya ili tumwamshe mfu.

Lakini Yesu ni tofauti. Ana nguvu ya pekee kutoka kwa Mungu. Basi, Yesu alipomwita Lazaro, kulitukia ajabu. Yule mtu aliyekuwa maiti siku nne akatoka pangoni! Akawa amerudishwa kwenye uhai! Aliweza kupumua na kutembea na kusema tena! Ndiyo, Yesu alimfufua Lazaro akiisha kuwa maiti siku nne! Haikuwa ajabu hiyo?— —Yohana 11:1-44.

Lakini labda utauliza, Alikuwa wapi Lazaro wakati wa siku nne alipokuwa maiti? Je! Lazaro alikwenda mbinguni alipokufa? Je! alikuwa hai huko juu pamoja na Mungu na malaika watakatifu?—

Fikiri sasa: Ikiwa Lazaro angalikuwa mbinguni wakati wa siku nne hizo, je! asingalisema jambo fulani juu yake?— Na ikiwa angalikuwa mbinguni, je! Yesu angalimrudisha atoke mahali hapo pazuri?— Biblia haisemi Lazaro alikuwa mbinguni.

Kumbuka, Yesu alisema kwamba Lazaro alikuwa akilala. lko kama nini unapokuwa katika usingizi?—

Unapokuwa katika usingizi mzito sana, hujui linalotukia karibu nawe, sivyo?— Na uamkapo hujui umekuwa ukilala kwa muda gani mpaka utazame saa.

Ndivyo ilivyo na wafu. Hawajui lo lote. Hawasikii lo lote mwilini. Na hawawezi kufanya lo lote.

Lakini watu wengine wanaogopa wafu. Hawataki kwenda karibu na makaburi, kwa sababu labda huenda wafu wakawaumiza. Unaweza kuwazia hilo? Mtu aliyekufa aweza kumwumiza aliye hai?— Hapana, Biblia inasema kwamba wafu hawawezi kufanya lo lote hata kidogo.

Umepata kumsikia ye yote akisema kwamba siku fulani wafu walirudi kama mizimu ili kuwatembelea walio hai?— Watu wengine wanaamini hivyo. Basi wanawawekea wafu chakula. Au labda kuwa na karamu za pekee katika siku hizo. Lakini unafikiri watu wafanyao mambo hayo kweli wanaamini ayasemayo Mungu juu ya wafu?—

Wewe unaamini ayasemayo Mungu?— Tukiamini, hatutaogopa wafu, bali tutafurahi kwa vile sisi tuko hai. Na ikiwa tu wenye kushukuru kwa Mungu kweli kweli kwa uhai, tutaonyesha hivyo kwa namna tunavyoishi maisha zetu kila siku. Tutafanya mambo ambayo Mungu anakubali.

(Ili kutia mkazo ubora wa maisha ya kila siku, kulinganisha na hali ya wafu, soma Mhubiri 9:5, 10, Ezekieli 18:4 na Zaburi 115:17.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki