Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 18 kur. 75-78
  • Sababu Watu Wanafanya Mabaya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sababu Watu Wanafanya Mabaya
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Watu Wanaofanya Mabaya Wanaweza Kubadilika?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Yesu Amchagua Sauli
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Mnyanyasaji Aona Nuru Kubwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Wakienda Damasko
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 18 kur. 75-78

Sura ya 18

Sababu Watu Wanafanya Mabaya

ISINGEKUWA ajabu ikiwa kila mtu angekuwa mzuri?— Ndipo hakuna ambaye angemwumiza mwingine.

Lakini kuna ye yote ambaye kweli ni mzuri wakati wote? Unaonaje?— Biblia inatuambia kwamba Yehova Mungu ni mzuri sikuzote. Na Yesu, Mwalimu Mkuu, anafanya mazuri sikuzote. Lakini hakuna mtu katika sisi afanyaye mazuri wakati wote.

Huenda tukajaribu kuwa wazuri. Lakini kuna nyakati ambapo tunafikiri mabaya, sivyo?— Na kufanya mabaya nyakati nyingine. Mtu wa kwanza Adamu, hakumtii Mungu kwa kusudi. Alilofanya lilikuwa baya sana. Matokeo yake, sisi sote tulizaliwa wasiokamilika. Sisi sote ni watoto wa Adamu. Ndiyo sababu watu wanafanya mabaya, ingawa hawataki kuwa wabaya.

Lakini watu wengine wanafanya mabaya kwa kusudi. Wanachukia watu wengine na wanafanya mambo ili wawaumize. Unafikiri mtu kama huyo angeweza kugeuka akajifunza kuwa mzuri?—

Biblia inatupa mifano ya watu wabaya waliogeuka. Nitakuambia juu ya mmoja wao. Na pamoja, na tuone ikiwa twaweza kujua sababu gani alikuwa mbaya.

Jina la mtu huyo ni Sauli. Sauli alikuwa mtu wa dini sana. Alikuwa wa kikundi cha kidini kiitwacho Mafarisayo. Walikuwa na Neno la Mungu, lakini walifuata zaidi mafundisho ya wengine wa viongozi wao wenyewe. Unafikiri hiyo ilikuwa hekima?— Ingeongoza kwenye taabu nyingi.

Siku moja wakati Sauli alipokuwa Yerusalemu mwanafunzi wa Yesu jina lake Stefano alikamatwa. Wakampeleka kortini. Wengine kati ya mahakimu kortini walikuwa Mafarisayo. Hata ingawa mabaya yalisemwa juu yake, Stefano hakuogopa. Alisema kwa nguvu akawapa mahakimu ushuhuda mzuri juu ya Mungu na juu ya Yesu.

Lakini mahakimu hao hawakupenda waliyosikia. Walikasirika sana. Wakamshika Stefano kwa nguvu wakamtoa nje ya mji. Wakamwangusha chini, wakamtupia mawe mpaka akafa.

Sauli alikuwa pale pale akitazama Stefano akiuawa. Yeye alifikiri ili-kuwa vizuri kumwua. Lakini angewezaje kufikiri jambo hilo baya?—

Basi, Sauli alikuwa amelelewa kama Farisayo. Katika maisha yake yote alikuwa amefundishwa kwamba wao walikuwa wa kweli. Alifuata mfano wa watu hawa. Hivyo akawa kama wao.

Sasa kwa kuwa Stefano alikufa, Sauli alitaka kumaliza wanafunzi waliobaki wa Yesu. Akaanza kuwaingilia katika nyumba zao akiwavuta wanaume na wanawake. Ndipo angeagiza watupwe kifungoni. Wengi wa wanafunzi walihama kutoka Yerusalemu wawe mbali na Sauli. Lakini hawakuacha kuhubiri juu ya Yesu.—Matendo 8:1-4.

Jambo hili lilimfanya Sauli achukie wanafunzi wa Yesu hata zaidi. Basi akaenda kwa kuhani mkuu akapata ruhusa awakamate Wakristo katika mji wa Dameski. Lakini alipokuwa akielekea Dameski ajabu ikatukia.

Nuru ilimulika kutoka mbinguni kwa kung’aa sana hata ikampofusha Sauli. Na sauti ikasema: “Sauli, Sauli, mbona waniudhi?” Huyo alikuwa Bwana Yesu aliyekuwa akisema kutoka mbinguni! Basi Sauli aliongozwa akiwa kipofu mpaka Dameski.

Siku tatu kutoka hapo Yesu alionekana katika njozi kwa mmoja wa wanafunzi wake jina lake Anania. Yesu alimwambia Anania amfikie Sauli akamwondolee upofu na kusema naye. Sauli alikuwa na nia ya kusikiliza. Wakati Anania aliposema naye, Sauli alikubali kweli juu ya Yesu. Macho yake yalipata kuona tena. Njia yake ya maisha iligeuka. Akawa mtumishi mwaminifu wa Mungu.—Matendo 9:1-22.

Sasa unaelewa sababu gani Sauli alikuwa mbaya sana?— Alikuwa amefundishwa makosa. Alikuwa akifuata wanadamu ambao hawakuwa waaminifu kwa Mungu. Alikuwa wa kikundi cha watu walioweka mawazo ya wanadamu mbele ya Neno la Mungu. Lakini Sauli aligeuka kwa sababu hakuichukia kweli.

Kuna watu wengi leo walio kama Sauli. Wanaweza kugeuka, lakini si vyepesi. Sababu moja ni kwamba mtu fulani anafanya bidii ili kumfanya kila mtu afanye mabaya. Unamjua ni nani huyo?— Yesu alizungumza juu yake aliposema na Sauli kutoka mbinguni. Alimwambia Sauli: ‘Ninakutuma ukawafumbue watu macho yao, waache giza na nguvu za Shetani wamwelekee Mungu.’—Matendo 26:17, 18.

Ndiyo, ni Shetani Ibilisi ambaye amesababisha mafundisho yote ya mabaya. Yeye anataka watu wawe wabaya. Basi tukifanya mabaya, ndipo lbilisi anapendezwa. Lakini tunataka tumpendeze Yehova, sivyo?— Twawezaje kuwa na hakika ya kufanya hivi?—

Tutampendeza Mungu ikiwa sikuzote tunaangalia Biblia na kufanya ambayo inasema. Wakati Biblia inapoonyesha kwamba tumekuwa tukifanya jambo baya, imetupasa tuache kulifanya. Tunapojifunza kutoka katika Biblia juu ya mambo ambayo Mungu anataka tufanye, yatupasa tuwe na moyo wa kuyafanya. Tunapofanya yanayompendeza Mungu tunafanya mazuri, kwa sababu Mungu ni mwema.

(Kwa kusaidia kuepuka kufanya mabaya, someni pamoja Mithali 3:5-7; 12:15; 2:10-14; Zaburi 119:9-11.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki