Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 91
  • Yesu Anafundisha Juu ya Mlima

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Anafundisha Juu ya Mlima
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Kuchagua Mitume Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Kuchagua Mitume Wake
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Yesu Achagua Mitume Kumi na Wawili
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yesu Anachagua Mitume Kumi na Wawili
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 91
Yesu akifundisha watu katika Mahubiri yake ya Mlimani

HADITHI YA 91

Yesu Anafundisha Juu ya Mlima

MWONE Yesu ameketi hapa. Anafundisha watu wote hawa mlimani katika Galilaya. Hao walioketi karibu naye ni wanafunzi wake. Amechagua 12 wawe mitume. Mitume ni wanafunzi wa pekee wa Yesu. Unajua majina yao?

Kuna Simoni Petro na nduguye Andrea. Halafu Yakobo na Yohana, nao pia ni ndugu. Mtume mwingine pia anaitwa Yakobo, na mwingine anaitwa pia Simoni. Mitume wawili wanaitwa Yuda. Mmoja ni Yuda Iskariote, na Yuda mwingine anaitwa pia Thadayo. Kisha kuna Filipo na Nathanaeli (pia aitwa Bartholomayo), na Mathayo na Tomaso.

Baada ya kurudi kutoka Samaria, Yesu alianza kuhubiri mara ya kwanza hivi: ‘Ufalme wa mbingu umekaribia.’ Je! unajua maana ya ufalme huo? Ni serikali halisi ya Mungu. Yesu ni mfalme wa huo. Atatawala kutoka mbinguni alete amani kwenye dunia hii. Dunia yote itafanywa na ufalme wa Mungu kuwa paradiso nzuri.

Hapa Yesu anafundisha watu habari za ufalme huo. ‘Msali hivi,’ anaeleza. ‘Baba yetu mbinguni, jina lako liheshimiwe. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanywe duniani, kama mbinguni.’ Watu wengi wanaiita ‘Sala ya Bwana.’ Wengine wanaiita ‘Baba Yetu.’ Unaweza kutoa sala yote?

Umati wa watu ukisikiliza Mahubiri ya Yesu ya Mlimani

Yesu pia anafundisha watu namna ya kutendeana. ‘Watendee wengine unavyotaka wakutendee,’ asema. Unapenda wakati wengine wanakutendea vizuri, sivyo? Basi, Yesu anatuambia tuwatendee wengine vizuri. Je! haitakuwa vizuri sana wakati kila mtu atakapofanya hivyo katika dunia paradiso?

Mathayo sura za 5 mpaka 7; 10:1-4.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki