Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 115
  • Paradiso Mpya Duniani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Paradiso Mpya Duniani
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • “Utakuwa Pamoja na Mimi katika Paradiso”
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Ni Nani Watakaofufuliwa? Nao Wataishi Wapi?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Ni Nini Kusudi la Mungu kwa Dunia?
    Mungu Anataka Tufanye Nini?
  • “Tutaonana Paradiso!”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2018
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 115
Watu wakifurahia wanyama katika Paradiso duniani

HADITHI YA 115

Paradiso Mpya Duniani

TAZAMA miti ile mirefu, maua mazuri na milima mirefu. Je! hapa si pazuri? Angalia yule paa anavyokula katika mkono wa kivulana huyu. Watazame tena simba wale na farasi waliosimama pale katika shamba la majani. Ungependa kukaa katika nyumba mahali kama hapa?

Mungu anataka wewe ukae milele duniani katika paradiso. Hataki upate maumivu na uchungu unaosumbua watu leo. Biblia inaahidi hivi wale watakaokaa katika paradiso mpya: ‘Mungu atakuwa pamoja nao. Hakutakuwa tena kifo wala kulia wala maumivu. Mambo ya kale yamekwisha.’

Msichana mdogo katika Paradiso ameshika na maua aliyoyachuma

Yesu atatokeza badiliko zuri hilo. Unajua litakea wakati gani? Baada ya kuondoa mabaya na waovu wote duniani. Kumbuka, Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya watu magonjwa yote, hata akafufua wafu. Yesu alifanya hivyo ili aonyeshe atakavyofanya duniani pote akiwa Mfalme wa ufalme wa Mungu.

Ebu fikiri itakuwa vizuri kama nini katika paradiso mpya hapa duniani! Yesu, pamoja na wengine ambao anachagua, watakuwa wakitawala mbinguni. Watawala hao wataangalia wote duniani na kuhakikisha kwamba wanafurahi. Na tuone yanayotupasa kufanya ili tuhakikishe kwamba Mungu atatupa uzima wa milele katika paradiso yake mpya.

Ufunuo 21:3, 4; 5:9, 10; 14:1-3.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki