Wimbo 165
Sifu Yah Pamoja Nami!
1. Tusifu Yah, ’Falme wetu.
Wenye pumuzi walete sifa.
Asubuhi na usiku,
Waambie watu ’weza wake.
Ndiyo, waambie ’weza wake.
2. Tusifu Yah. Mwenye pendo
Yeye si mwepesi wa hasira.
Wa ajabu na mukuu;
Shangwe kusema matendo yake.
Shangwe kusema matendo yake.
3. Tusifu Yah. Hushibisha
Haja za wote za kila siku.
Hupa nguvu kwa wanyonge.
Mbona watu wasiseme wema?
Ndiyo, watu waseme wemake.
4. Tusifu Yah, Yu karibu,
Maombi yetu atasikia.
Na waovu ’taharibu,
Huwahifadhi wamupendao.
Huwahifadhi wamupendao.