Wimbo Na. 104
Msifu Yah Pamoja Nami
Makala Iliyochapishwa
1. Tusifu Yah;
Kwa sauti!
Uhai na vyote anatupa.
Kila siku,
Tumusifu.
Ni mwenye ’pendo na nguvu zote.
Twamwimbia na kumutangaza.
2. Tusifu Yah,
Hushibisha.
Husikiliza maombi yetu.
Huinua
Wadhaifu;
Roho yake huwaimarisha.
Jina lake na tulitangaze.
3. Tusifu Yah.
Mungu wetu;
Atufariji kukiwa shida.
Asamehe;
Na kuponya.
Baraka za ’falme tutapata.
Njooni tumusifu kwa shangwe!
(Ona pia Zab. 94:18, 19; 145:21; 147:1; 150:2.)