Wimbo 217
Kupata Urafiki wa Yehova
1. Nani atakuwa rafikiyo Mungu?
Nani atabaki hemani mwako daima?
Asiye na kosa Akuogopaye.
Mwenye moyo safi na asemaye ukweli.
Yehova, wamupa nani urafiki?
Nani ataishi nawe mulimani mwako?
Ni ambaye usemi wake haumuudhi jirani.
(Korasi)
2. Nani atakaa nawe, E Yehova?
Nani rafikiyo, utakayekaa naye?
Asiyegeuka, Hata iumize,
Aenda kinyofu na, anashika ukweli.
Urafiki nawe, Mungu tunataka.
Neno lako husema wazi matakwa yako.
Tunyoshe mapito yetu, tusipinde sheria zako.
(Korasi)
3. Twataka kukaa, nawe E Yehova.
Amani yako yazidi; na mawazo pia.
Kupitia Yesu, Umeirudisha
Ibada safi. Hivyo wengi wakuabudu.
Urafiki huo, Mungu tutalinda.
Maisha zetu wenyewe zisipate dhara.
Kama jeshi la umoja twasimama mlimani pako.
(KORASI)
Yehova, milele, tuwe rafikizo.