Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ti uku. 3
  • Je! Uuamini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Uuamini?
  • Je, Uamini Utatu?
  • Habari Zinazolingana
  • Sehemu ya 1—Je! Yesu na Wanafunzi Wake Walifundisha Fundisho la Utatu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Je! Kwa Wazi Hilo Ni Fundisho la Biblia?
    Je, Uamini Utatu?
  • Je, Mungu Ni Utatu?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Fundisho la Utatu Lilisitawi Jinsi Gani?
    Je, Uamini Utatu?
Pata Habari Zaidi
Je, Uamini Utatu?
ti uku. 3

Je! Uuamini?

JE! WEWE waamini Utatu? Watu walio wengi katika Jumuiya ya Wakristo huuamini. Ingawaje, limekuwa ndilo fundisho kuu la makanisa kwa karne nyingi.

Kwa sababu hiyo, wewe ungefikiri kwamba hakungeweza kuwa na shaka juu yalo. Lakini liko, na juzijuzi hata baadhi ya wenye kuliunga mkono wameongeza kuni katika kibishanio hicho.

Kwa nini habari kama hii iwe ya upendezi badala ya kuchukuliwa hivi hivi tu? Kwa sababu Yesu mwenyewe alisema hivi: “Uhai wa milele ni huu: kujua wewe, Mungu aliye wa kweli peke yake, na Yesu Kristo ambaye wewe umetuma.” Kwa hiyo wakati wetu wote ujao hutegemea kujua kwetu jinsi Mungu alivyo kikweli, na hiyo humaanisha kuufikia mzizi wa kibishanio cha Utatu. Kwa hiyo, kwa nini usijichunguzie wewe mwenyewe?—Yohana 17:3, Jerusalem Bible ya Katoliki (JB).

Kuna mawazo mbalimbali kuhusu Utatu. Lakini kwa ujumla fundisho la Utatu ni kwamba katika Uungu mna watu (nafsi) watatu, Baba, Mwana, na Mzuka (Roho) Mtakatifu; na bado, wote pamoja ni Mungu mmoja tu. Fundisho hilo husema kwamba watatu hao wako sawa, ni waweza yote, na hawakuumbwa, nao walikuwako tangu milele katika Uungu huo.

Hata hivyo, wengine husema kwamba fundisho la Utatu ni bandia, kwamba Mungu Mweza Yote yuko peke yake akiwa tofauti na wengine, aliye wa milele, na mwenye nguvu zote. Wao husema kwamba Yesu alipokuwako kabla ya kuwa binadamu alikuwa, kama vile malaika, mtu-roho aliyeumbwa na Mungu akiwa tofauti na wengine, na kwa sababu hiyo ni lazima awe alikuwa na mwanzo. Wao hufundisha kwamba Yesu hajapata kamwe kuwa mwenye usawa na Mungu Mweza Yote katika maana yoyote; sikuzote amekuwa akijitiisha kwa Mungu na angali ajitiisha. Pia wao huamini kwamba mzuka mtakatifu si mtu bali ni roho ya Mungu, kani yake ya utendaji.

Wenye kuunga mkono Utatu husema kwamba msingi wao si Biblia tu bali pia ni pokeo la kidini. Wachambuzi wa fundisho hilo husema kwamba si fundisho la Biblia, chanzo kimoja cha historia hata kikijulisha wazi hivi: “Awali ya [Utatu] ni ya kipagani kabisa.”—The Paganism in Our Christianity.

Ikiwa Utatu ni wa kweli, ni kumshushia Yesu cheo kusema kwamba yeye hakuwa kamwe sawa na Mungu akiwa sehemu ya Uungu. Lakini ikiwa Utatu ni bandia, ni kumshushia cheo Mungu Mweza Yote kuita mtu yeyote kwamba yuko sawa na yeye, na ni vibaya hata zaidi kuita Mariamu “Mama ya Mungu.” Ikiwa Utatu ni bandia, ni kuvunjia Mungu heshima kusema, kama ilivyoandikwa katika kitabu Catholicism: “[Watu] wasipoweka Imani hii ikiwa timilifu na bila kuchafuliwa, pasipo shaka [wao wataangamia] milele. Na Imani ya Katoliki ni hii: sisi huabudu Mungu mmoja katika Utatu.”

Basi, kuna sababu nzuri kwa nini wewe wapaswa utake kuujua ukweli juu ya Utatu. Lakini kabla ya kuchunguza awali yao na dai lao la kwamba ni ukweli, ingesaidia kufasili fundisho hili kihususa zaidi. Utatu ni nini hasa? Wenye kuuunga mkono huufafanuaje?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki